Kwako rev kishoka

MaMkwe

JF-Expert Member
Sep 5, 2007
284
21
Heshima yako Mzee,

Awali ya wote ningependa ufahamu jinsi ninavyokupenda na kukuheshimu kama vile Maria Magdalena kwe Yesu. Kinachonifanya nikupende Mchungaji wa Kondoo za Bwana ni uadilifu wako. Wewe ni msema kweli. Hupendi unafiki. Kutokana na hilo mimi na wanakondoo wenzangu tunaomba utfahamishe kuhusu yaliyomo katika katiba hii ya sasa na mapungufu yake. Naamini kuna mazuri pia usiache kutufahamisha. Kisha utufahamishe yanayotakiwa kuwamo katika Katiba mpya. Nimeamua kukuuliza wewe kwa sababu naamini kuwa wewe si mnafiki. Utatueleza ukweli. Nina hofu kwamba huu wimbo wa Katiba mpya sisi walalahoi mambumbumbu tusipouelewa vizuri tunaweza kubisha au kukubali tu kububusa kisha tuje kujuta baadaye. Jirani yangu amerudi juzi toka Mombasa kumtembelea mtoto wa shangazi yake aliyeolewa huko. Anasema maisha ya Wakenya yamezidi kuwa magumu ingawa wakati wa kupiga kura waliambiwa kuwa KAtika mpya itawaletea ustawi mkubwa kiuchumi na kijamii. Walitarajia kupata mabadiliko mara moja baada ya KAtiba mpya kupitishwa. Lakini lo, wanazidi kuumia kila kukicha.

Mchungaji wa kondoo za Bwana

Tufahamishe vizuri
 
Back
Top Bottom