Kwako MNYIKA: CHADEMA andaeni kongamano la kitaifa kuhusu Tanzania after 2015

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,780
3,227
Leo nimesoma gazeti la Mwananchi kuna habari kuu kwamba tishio la urais CDM ni Dr.Slaa.baada ya kusoma sasa nimeamini kwamba CCM tayari wameridhika kushindwa kabla ya uchaguzi 2015, Mh. Sitta kathibitisha hilo ila hofu yake ni kwamba iwapo CDM mtashinda mtawezaje kuunda serikali. Lakini pia nimemuona Mh. Sitta anaupeo mdogo kuhusu mfumo wa vyama vingi, kwa kutokujua kwamba serikali inabaki kuwepo na ndiyo maana watumishi wanaaswa kuwa tayari kupokea serikali mpya kwa maaana CHAMA KIPYA TAWALA.

Mada yangu kwako Mnyika ni kwamba, tumeridhika na operation zenu kama OP SANGARA, M4C na zingine tunaamini mmepitia karibu tanzania nzima na sasa kwa hii operation yenu yenye timeframe ya kuishia MAY2013 mtakuwa mmepata mafanikio makubwa.

Tunachoomba kwenu CDM muandae kongamano la kitaifa litakalozungumzia mustakabri wa serikali mpya chini ya CDM, kwa kushirikisha wawakilishi maalumu wa makundi ya wakulima, wafanyakazi, wasomi na wanaharakati. Makongamano haya yatakuwa na jina la mikutano ya ndani.

Nawashauri mteue kanda tano ili kila kanda yafanyike hayo makongamano, mfano kanda ya ziwa centre ikawa MWANZA, kanda ya kasikazini centre ikawa ARUSHA, kanda ya kusini centre ikawa Mbeya, Kanda ya kusini mashariki centre Mtwara, n.k

Mada kuu iwe ni kupata ushauri kutoka kwa wadau namna bora ya kuja kuunda a new internal control government system, sytem ambayo itadhibiti rushwa, utawala bora, udhibiti wa rasilimali na pia kongamano hilo litatoa mapendekezo ya ukubwa wa serikali.

Ni hayo tu
 
sisi ccm hatuwezi kukubali mpange?
kwani mmeshashinda tutawaoiga maboom mpaka mkome!
 
Leo nimesoma gazeti la mwananchi kuna habari kuu kwamba tishio la urais CDM ni Dr.Slaa.baada ya kusoma sasa nimeamini kwamba CCM tayari wameridhika kushindwa kabla ya uchaguzi 2015, mh.sitta kathibitisha hilo ila hofu yake ni kwamba iwapo CDM mtashinda mtawezaje kuunda serikali.Lakini pia nimemuona mh.sitta anaupeo mdogo kuhusu mfumo wa vyama vingi, kwa kutokujua kwamba serikali inabaki kuwepo na ndiyo maana watumishi wanaaswa kuwa tayari kupokea serikali mpya kwa maaana CHAMA KIPYA TAWALA.....
ccm wanaamini serikali inaundwa na genge la wezi kama wao walivyo,sasa wakiangalia cdm wanaona wezi hawapo au waliopo ni wachache sana.ndiyo maana sita amepatwa na wasiwasi kwani haamini kama tz bila mafisadi itawezekana???

Hebu imagine,kama masele,makongoro,januaria makamba, matayo dvid na vimeo wengine wote simsau mwini na naibu wake,wameweza kubeba zamana za wizara za sreikali, watu ambao ni vilaaaaaza kabisa, sembuse majembe tulionao CDM?? acha utani bana, mwache Sitta aamini anachoamini.
 
Ninakubaliana na wewe kwa asilimia zote.
kimsingi sitta amejidhalilisha sana na kujishushia heshima yake katika hilo alilolisema.

Ninaunga mkono hoja ya kuwa na makongamano kwani matatizo yalioko tanzania ni ya kimfumo zaidi. mambo tunayoyaona ni kutokana na mfumo mbovu uliopo kwa sasa.

Huwa ninasema hata kama kikwete angefanya mabadiliko katika mfumo wa kiutawala na uongozi basi tunaweza kumwona kama kiongozi mzuri.

Therefore hata kama chadema watashinda na kutokubadili mfumo wa kiongozi tusitegee mapya tofauti na haya ya CCM
 
Ni lazima CDM ije na kitu kipya siyo siku zote siasa za majukwaani, wenzetu ulaya ndiyo siasa zao siku hizi, kwa watanzania walioko marekani wataniunga mkono kwamba kwa sasa wale republican wanendelea na makongamano ili kupata mawazo mapya nje ya chama chao, kuna wasomi wazuri, watu wenye maono mazuri lakini hawapendi siasa ila wanapenda makongamano kwa pale ni mahali brainstorming is the major take.

Nakusihi sana Mnyika mimi sijawahi kufika ulaya lakini kupitia TV and other media iko poa na yanayotokea huko na sisi we must re-engineer our system of running politics by imitating the contemporary approach zaidi ya kuendela na traditional approach.

Kwa kufanya hivyo mtapata new ways of doing things

baadae washikaji
 
Together we can.naunga hoja.baada ya m4C tujadili kitblamu namna ya kutawala kitalamu zaidi.
 
Naunga mkono hoja, nyongeza yangu pia chadema waandae utaratibu wa kuzungumza na watanzania kila mwanzo wa mwezi kuhusu mambo mbali *2 yakitaifa. napendekeza sio lazma iwe ni mwenyekiti bali yeyote atakaekuwa ameteuliwa kutoka nec ya chadema. vipindi hivyo virushwe hewani ktk Tv (S) garama tushirikishwe tutalipa watanzania
 
Naunga mkono hoja, nyongeza yangu pia chadema waandae utaratibu wa kuzungumza na watanzania kila mwanzo wa mwezi kuhusu mambo mbali *2 yakitaifa. napendekeza sio lazma iwe ni mwenyekiti bali yeyote atakaekuwa ameteuliwa kutoka nec ya chadema. vipindi hivyo virushwe hewani ktk Tv (S) garama tushirikishwe tutalipa watanzania
 
Sidhani kama CCM itaruhusu muendelee kuwa-frustrate itatumia matawi yake kama vile Polisi kuhakikisha hakuna kongamano litakalo ruhusiwa na mkilazimisha lazima watu wafe kutokana na kupigwa na kitu chenye ncha kali (Risasi) kama Morogoro.
 
ITS AGOOD IDEAS ,kwa mfano utaratibu wa kumuhoji bungeni waziri mkuu ,huu uliigwa kutoka kule uingereza kwenye bunge la mabwenyenye ,house of common,na unafanya kazi vizuri hapa .
 
Kuogoza Nyumbu hadi raha , unawaletea maigizo ya kushika UKUTA ili wakuachie nafasi ujigawie ruzuku ya chama hovyo.

Chadema mpaka Leo hawajapeleka gharama walizotumia kwenye uchaguzi mkuu.

Wizi mtupu.
 
Back
Top Bottom