Kwako mh. Spika, mama makinda: Umetupandishia gharama za muda wa hewani watanzania

AUTOMATIC

Member
Feb 23, 2012
11
4
Huku akijua kabisa kuwa idadi ya wabunge walioitikia hoja ya mheshimiwa wenje ya kutaka gharama za malipo ya muda wa hewani kubaki kama awali ilikuwa kubwa, mama Makinda alidai kuwa idadi ya wabunge walioitikia ndiyoooo kukubaliana na ongezeko hilo walikuwa wengi. Hali hii ilijidhihilisha hapo jana wakati wa kupitisha "financial bill" kwa wizara ya fedha.
MY TAKE: Watanzania wote tunaotumia mitandao ya simu hasa walalahoi, huyu ndiye ndiye adui yetu katika hili na utaratibu wa "ndiyooooooo" upigwe marufuku ili kuruhusu upigaji kura
 
Aiseee baba yangu huyu mama ana anachokijuwa yeye si anawekewa laki 10 na serekali

ngoja nikalime na jembe langu la mkono
 
Ndo tujifunze kufanya uchaguzi sahihi,maana tumezoea kulalamika tu.2015 piga chini magamba wote.
 
Kwani hamjiulizi kwanini Vodacom walienda kabla ya bunge kuanza na wakagawa simu bure
Pia jiulizeni kwanini mtambo wa kuangalia idadi ya simu haujanunuliwa mpaka sasa badala makampuni ya simu ndiyo yanasema tulipata kiasi hiki kutokana na simu hizi zilizopigwa
Hakuna cha january makamba wala nani huu ni mchezo wa makusudi kwani badala ya serikali kuzibana hizi kampuni zilipe kodi zimeendelea kuwakandamiza wananchi
 
huyu mama alinikera kupita kiasi siku hiyo! halafu ukiangalia macho yake utadhani anakaanga sumu halafu anajichekeshachekesha kama mjinga!
 
Makinda is just a rubber stamp, she never decide on the side of tanzanian's where the poor are the majority. Always makinda sides with minority richest businessmens (mafisadi) or big companies.

I will blame ccm for overthrowing Sita who at least dared to putfoward and give consideration on matters would harm poor mostly or the nation at large.

Ccm kazi mnayo 2015 maana kila kiongozi anachimba kaburi kwa mtindo wake.
 
bunge letu ifikie hatua ya kuwa linapiga kura za maandishi mambo ya ndiooo, Hapanaaaa Kama watoto wa chekechea.
 
Nasikia ni mwenyekiti wa bodi ya wakuregenzi wa kampuni fulani ya mawasiliano hapa nchini.
 
Wakati nchi zote zinapigana kupunguza gharama za mawasliano sisi ndio tunapandisha licha ya umaskini tulionao. Tuna upungufu wa viongozi wa watu waliowengi kwa maana ya maskini. Viongozi wetu wanaotoka katika familia maskini sana na kuchaguliwa na watu maskini ili wakawapiganie kupunguza ugumu wa maisha wamekuwa wasaliti wakuu kwani badala yake wanaenda kujiattach kwenye class ya wafanyabiashara na watu mashuhuri na kutafauta kukubalika na tabaka hilo ambalo lipo kimasrahi zaidi na kusahau kabisa halihalisi ya kule walikotoka. Nchi hii masikini wataendelea kuwa madaraja na ngazi za mafanikio ya watu mpaka watakapoamka. Siongelei tabaka la watanzania kama mliomo humu angalau mnaona hovyo hovyo inayoendelea, am talking about wanavijiji wa njombe, namanyere, na vijiji vingene ambako mtu anaweka shilingi 500 kwenye sim kwa wiki na kubeep ndio kupiga.
 
Huku akijua kabisa kuwa idadi ya wabunge walioitikia hoja ya mheshimiwa wenje ya kutaka gharama za malipo ya muda wa hewani kubaki kama awali ilikuwa kubwa, mama Makinda alidai kuwa idadi ya wabunge walioitikia ndiyoooo kukubaliana na ongezeko hilo walikuwa wengi. Hali hii ilijidhihilisha hapo jana wakati wa kupitisha "financial bill" kwa wizara ya fedha.
MY TAKE: Watanzania wote tunaotumia mitandao ya simu hasa walalahoi, huyu ndiye ndiye adui yetu katika hili na utaratibu wa "ndiyooooooo" upigwe marufuku ili kuruhusu upigaji kura
Huyu mama ni picha ya spika tu na sio Spika
Huenda ana maslahi na hizi kampuni na hata kuwa alishakatiwa mzigo wake.sielewi sababu ya kukubali magari makuukuu yaendelee kuingia kwa kumsaidia mlalahoi lakini hapo hapo kumuongezea kodi katika air tyme.

Ikumbukwe watanzania wanaoweza kumiliki magari ni wachache lakini simu ni kitu ambacho asilimia kubwa ya watanzania wanaweza kukimiliki,mathalani huko vijijini SIMU,TOCHI na RADIO mara nyingi ndio asset za thamani mtz anazoweza kumiliki

sasa kumkaba katika hili ni sawa na kukamua maji katika ndoo na kumwagia mtoni..yeye huyu mama anatumia Postpaid inalipiwa na bunge,hafikirii mtz anayeishi kwa wastani wa dola moja kwa siku atamudu vipi hizo gharama

Tumekuwa tukilalamika na kulalamikiwa kila siku kuwa tz gharama za simu ni kubwa ukilinganisha na wenzetu lakini badala ya kuzishusha au kustabilise zilizopo tunazipandisha wakati huo huo makampuni ya simu yanakwepa kodi na hayana monitoring yoyote

Walitudanganya kuwa oooh Optic Fibre ikiungwa gharama za simu zittashuka,Je wewe mama semambba ndio kushuka huku? kwa utaratibu ule labda kawafanyie watu wa njombe na sio watz wote
 
Huku akijua kabisa kuwa idadi ya wabunge walioitikia hoja ya mheshimiwa wenje ya kutaka gharama za malipo ya muda wa hewani kubaki kama awali ilikuwa kubwa, mama Makinda alidai kuwa idadi ya wabunge walioitikia ndiyoooo kukubaliana na ongezeko hilo walikuwa wengi. Hali hii ilijidhihilisha hapo jana wakati wa kupitisha "financial bill" kwa wizara ya fedha.
MY TAKE: Watanzania wote tunaotumia mitandao ya simu hasa walalahoi, huyu ndiye ndiye adui yetu katika hili na utaratibu wa "ndiyooooooo" upigwe marufuku ili kuruhusu upigaji kura

Mkuu wa kulaumiwa ni wabunge kwani wanamuendekeza huyu mwanamke namna ambavyo anawaburuza.Mimi mwenyewe nilishuhudia wakati wanapitisha hicho kifungu.Ni wazi waliopinga walikuwa wengi na kuna sauti kama sikosei ilikuwa ya Zitto alietaka ipigwe kura ya siri lakini yule mwanamke bila aibu alikataa.

Sasa mimi nawashangaa hawa wabunge kwanini wasilete hoja ya kumkataa huyu spika kwani wao ndio wanaoweza kumuondoa.Vinginevyo watakuwa wanafiki.Huyu mama anawaburuza sana na wao wamebaki kuwa kama watoto wa chekechea wanaokubali kuburuzwa badala ya kupaza sauti kumkataa.

Binafsi simpendi kabisa huyu mama kwani huwa anaonekana dhahiri kuchukia pale anapoona serikali inabanwa.Sasa sijui kama anajua wajibu wa bunge.Kweli huyu mama hafai kabisa kuwa spika kwani mara nyingi anatumia madaraka yake kuilinda na kuitetea serikali.

Tatizo wamekuwa kwenye madaraka miaka mingi kiasi kwamba hawajui tena ugumu wa maisha kwani wao kila kitu serikali inawagharamia hata hizo simu zao na ndio maana akaburuza wenzake wapitishe ule uamuzi.

Wabunge huyu mama hawafai na mumkatee kama mko serious na kazi yenu.
 
[h=3]Uongozi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Wakutana na Spika Wa Bunge Anne Makinda na Kamati Ya Miundombinu Mjini Dodoma[/h]
Spika wa Bunge Bi. Anna Makinda kulia akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza na Ofisa mahusiano Mkuu wa Vodacom Mwamvita Makamba. Viongozi wa Vodacom walipomtembelea Spika ofisini kwakwe mjini Dodoma leo.
_MG_7911.jpg
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (wa kwanza kulia) akifuatiwa na Ofisa Mkuu wa Mahusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba wakiwa pamoja na wajumbe wa kamati ya Bunge ya miundombinu. Vodacom ilikutana na kamati hiyo leo mjini Dodoma kujitambulisha na kuzungumzia uwekezaji wa Vodacom nchini.
_MG_7904.jpg
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Peter Serukamaba akiongoza kikao cha pamoja kati ya kamati yake na uongozi wa kampuni ya Vodacom Tanzania iliyotembelea kamati hiyo leo mjijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumzia uwekezaji wa Vodacom nchini. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza akifuatiwa na Ofisa Mkuu Mahusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba
 
https://www.jamiiforums.com/habari-...950-vodacom-yahonga-wabunge-blackberry-2.html

Katika hatua ambayo imeibua mjadala mzito katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti, Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom imemwaga Blackberry kila moja ikiwa na thamani ya Shilingi laki 7 na muda wa maongezi wa Shilingi 100, 000 ka wabunge 23 wa kamati ya Miundombinu akiwemo Spika wa Bunge Anna Simamba Makinda.

Baadhi ya Wabunge wameripotiwa kukataa simu hizo huku Mwenyekiti wa Kamati hiyo Peter Serukamba na Spika Anna Makinda wakidaka ofa hiyo kiulaini.

Source; Gazeti la MWANAHABARI la leo

My Take:
Si kwamba huu ni mkakati wa Vpdacom kuzima kelele za Wabunge ambao wamekuwa wakidai kuwa makampuni ya simu yamekuwa yakiwakamua wananchi vya kutosha na yamekuwa yakilipa kodi kiduchu?
 
Makinda haendagi sokoni,haendi buchani,hapandi daladali,hapingi foleni kununua luku,
zaidi makinda simu yake hajawahi kuomba nipige TAFU ya jero unategemea amtetee nani?
Dr slaa aliwaasa kuwa ccm ni janga la kitaifa hamkumwelewa?
 
https://www.jamiiforums.com/habari-...950-vodacom-yahonga-wabunge-blackberry-2.html

Katika hatua ambayo imeibua mjadala mzito katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti, Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom imemwaga Blackberry kila moja ikiwa na thamani ya Shilingi laki 7 na muda wa maongezi wa Shilingi 100, 000 ka wabunge 23 wa kamati ya Miundombinu akiwemo Spika wa Bunge Anna Simamba Makinda.

Baadhi ya Wabunge wameripotiwa kukataa simu hizo huku Mwenyekiti wa Kamati hiyo Peter Serukamba na Spika Anna Makinda wakidaka ofa hiyo kiulaini.

Source; Gazeti la MWANAHABARI la leo

My Take:
Si kwamba huu ni mkakati wa Vpdacom kuzima kelele za Wabunge ambao wamekuwa wakidai kuwa makampuni ya simu yamekuwa yakiwakamua wananchi vya kutosha na yamekuwa yakilipa kodi kiduchu?

Mkuu, umeanika hadi maini yameonekana. KUMBE ndo source ya kamchezo kote!!!!!!!!!!............ Haya bana Ngoja voda waziri kututengenezea voucher za tsh. 450.
 
Back
Top Bottom