Kwako Mh Cyril Chami

subash

Member
Dec 30, 2011
75
36
Mh Sirily Chami mbunge wa Moshi vijijini, heri ya mwaka mpya, kaka sisi wanakijiji wa Old Moshi hasa Mdawi tunapata taabu maana ahadi zako haujatimiza hata moja, barabara ya Mdawi mpaka Mengeni kaka ikipiga hata tone la mvua tunapata taabu kupita maelezo.

Tafadhali tekeleza ahadi zako otherwise 2015 ubunge chora chini mana hatuwezi kurudia makosa. Hata moram unashindwa kutuwekea?? Hainiingii kwa akili mimi.

Barabara ya Kiborloni inapitika throughout the year Sango hali kadhalika, Shia kama kawaida, iweje barabara ya Mdawi ni tatizo??? Kaka jitahidi ukweli wana Mdawi hatuna hamu na ubunge wako kama vipi tema mzigo CDM wafanye kweli kaka, mana ukiwa na maiti then kuna mvua lazima kubeba kichwani.

Kero nyingine ni shule; hatuna maabara vijana toka Mdawi lazima waende mpaka Komakya hiyo ni Shia kwanini hautuwekei shule ya sekondari pale Mdawi??

Wana jf naomba kuwasilisha
 
Subash bhai huenda bado yuko apolo, ila kiukweli mnapata taabu mana mdawi hakupitiki wkt wa mvua kilio chenu kimemfikia, diwani ni wa ccm au cdm, yabidi ajulishwe nyumbani ni nyumbani na inabidi akupe first priority
 
huyu mh labda yupo busy anazichanga za ubunge 2015 maana kero zp nying shule hazina vifaa+walimu mfano shule inafelisha wanafunzi wote wa mwaka jana kidato 4 MSIRIWA sekondari IKO URU KASKAZN DIWAN NI MAGAMBA na sidhan kama kuna juhudi za makusudi kuokoa
vijana,pia maji ni tatizo ilhali ni kilmanjoro vyanzo vya maji tele yeye na timu yake yuko busy kuwakomoa upinzani na kuwanunua wahame mfano aliyekuwa mkiti kijiji mrawi
 
Wa-old moshi tunapata taabu sana Mr Chami tafadhali sikia kilio chetu
 
Nimesikia huyu jamaa kajenga barabara ya Kibosho kirima je kuna kaukweli hapo?
Ila nadhani huyu mtu hawajui watu wa Moshi vijiji ni, niwanamapinduzi wa kweli.....huwa hawachagui chama wanachagua mtu. Ila kusema ukweli Mboye nduiye aliyesababisha huyu kilaza aendelee kuwa mbunge.......Bila Mboye tungekuwa tunaongea mengine wakati huu......
 
Bora hata sisi wa komang'oro kuna mzee mmoja wa kwa ringo ana kaescudo kake anaifanyia marekebisho ile barabara kwa hela yake.yule ndo mbunge wangu.
 
Back
Top Bottom