Kwako marehemu baba wa taifa mwl. JK Nyerere

Baba, Mchina kagoma kumsikiliza waziri Magufuli...yani ile barabara ya mbagala kama watoto wa chekechea ndo wamejenga baba!
 
27. Baba siku hizi bilioni moja inaitwa vijisent kina chenge hao
28. kipindi kimoja tuu cha uongozi wa baba yake na yeye bilionea baba inatisha wakati tunawaona wanao kina makongoro na wengine wakihaha mitaani ina shangaza sana baba
 
Baba siku hizi mafisadi wanaambiwa na mkuu wa kaya (JK ) warudishe fedha za umma walizoiba huku akichekacheke kama anaangalia Ze Comedy.
 
Baba nashukuru onyo ulilotoa la kumpiga marufuku ndg lowassa yd kwamba hafai hata kuwa mwnyekiti wa mtaa na wakakukaidi baba na wakamchagua kiranja wa mawaziri leo hii baba aliaibika kwa kujiuzulu kwa kashfa kubwa sana baba nadhani laana uliocha inamtafuna baba yetu mpendwa lala salama na nakuomba baba endelea kuwashushia gharika wale wote waendao kinyume na matakwa yako baba
 
Baba huko uliko jua ya kwamba CCM uliyoiacha si ya siasa ya jenga nchi tena baba imebaki ya Chukua Chako Mapema baba yaani ccm yabomoa nchi baba watu si wasafi tena baba hawafuati maadili uliYowaachia baba wanafisadisha mpaka kwenye kilimo baba eti wanatumia mwavul wa kilimo kwanza baba yaani wafikia hatua hata kuwapora vijana wa ule u bongo wa fleva jina lao la wakali kwanza baba utuombee na nguvu ya umma ipate chukua wake mkondo baba
 
baba udini umetawala na wewe uliukemea lakin sasa hv baraza zima la mawaziri wamejaa dini moja tuu
 
Hii ya baba nanihii kua na nyumba ndogo nyingi imeniacha hoi! Perhaps ni za kuchunga viwanja ili mamlaka wasiuze kwa wengine na siku moja atajenga nyumba moja kuuubwa!...Heko baba mkubwa sana,kwa upande wa mama mdogo,babu upande wa mama mkubwa anakukumbusha kumalizia mahari na shangazi upande wa mama mdogo zaidi anasema kitenge ulichomrubuni nacho akakuunganisha na mtoto wa dadake kimetoboka!
 
Back
Top Bottom