Kwako Dr Kigwangalla: Sahihi yako hatujaiona

uwe unafunga hilo domo lako katika mambo yoote yenye tija dhidi ya ubadhirifu wa rasilimali zetu maana hujielewi Bwana Mheshimiwa na jaribu kutembelea Mirembe kidogo khaaa....! :A S angry:
 
Binfsi nimem_PM kumualert kuhusu hii thread, na kumpa link ya uzi.
He cannot claim unawaress of the thread.
Simply ignored it.
He is haunted from within.

safi sana, you've gone an extra mile, chukua mobile thanks hiyo.
 
Mh.Kigwangalla bado una fikra mgando hata wewe?Yani kuwa mbunge wa ccm ndo uache hata maovu yafanyike kisa ni chama chako na ndicho chenye serikali!Kama unaamini hoja ya zitto ilikuwa ni kupressurize mawaziri wang'oke mbona sasa hukuweka sahihi au we nawe unaamini mawaziri hawapaswi kuchukuliwa hatua?Wabunge wa CCM hiyo cauccus yenu wala sio bunge mtambue!Mmechaguliwa muwe wabunge wala sio wa'caucuss'.Inashangaza mnapoacha kutumia chombo rasmi mnapowakilisha wananchi wenu na nyinyi kukiacha na kutumia hiyo caucuss ambayo kimsingi haitambuliki kikatiba wala kisheria!Mnaogopa nini kutumia bunge?Yani kuwa majority ndiko kuifanya serikali i'enjoy' majority yenu hata kwenye mambo ya kipuuzi kama hayo i'enjoy' tu?Kwa nini msitumie majority yenu kuwafanya wananchi wa'enjoy' jinsi mnavyoiadabisha serikali?
Haya,mpaka sasa hakuna taarifa za hata waziri mmoja kujiuzulu achilia mbali hao nane 'caucus' yenu iliyoaminishwa.Bado unadhani hoja hii ya Zitto haina uzito wowote wa kuungwa mkono ili hatimaye maovu ya mawaziri na serikali yaweze kukomeshwa?
 
Ndugu zangu wanabodi,

Mimi sijawahi kuwa mnafiki, at least kwa alama tatu za mnafiki kama tunavyofundishwa sisi waislamu. Kwa faida ya mjadala huu, niseme alama zenyewe. Moja ni kuwa akitoa ahadi hatekelezi. Mbili, ni akiaminiwa anahalifu na tatu, akizungumza husema uongo. Namshukuru Mungu sina hata moja ya alama hizi na hivyo kushindwa mtihani wa kuwa 'mnafiki'. Ungeniita mnafiki kama nisingekuwa tayari kutoa maelezo ya maamuzi yangu, ama kama ningewasaliti CCM na kupeleka siri za huku kule, ama kama ningeahidi kuunga mkono hoja hiyo kisha nikakimbia. Leo hii mimi niko chama kimoja tu, CCM, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya CCM. Siku nikihamia CHADEMA/CUF/NCCR basi nitafanya ya huko bila kusaliti kule na kurudisha CCM ama kupeleka kokote kule kinyume na utaratibu. Huo ndiyo msimamo wa ukweli na siyo unafiki.

Wakatabahu,
HK.

Mh HK, comment hizi nilikurushia kule kwenye uzi wako ila nimeona pia nizilete hapa kwenye uzi husika


Shukrani kwa kuja na majibu haya.

Kwanza kabisa nakubaliana na hoja yako kwamba ndani ya baraza la Mawaziri, wapo ambao kweli ni wasafi na ni ukweli usiopingika.
Ila napingana na wewe kwa kauli yako kwamba unapokua ndani ya CCM lazima ufanye mambo yanayokubalika ndani ya CCM. Does this mean kwamba hata kama kuna mabovu wewe utayasupport tu? I think umuhimu wa kua ndani ya chama ni kukijenga chama, na chama kunajengeka kwa kuambiana ukweli na wakati mwingine kuwawajibisha wale wanaoenda kinyume na matwakwa ya wananchi ambao chama kinawatetea. Hiki ndio kiini cha mjadala wa kuwataka mawaziri wasio wajibikia wajiondoe.

Ni ukweli usiopingika kwamba ndani ya CCM hakuna mwenye uwezo wa kumfunga paka kengele. Wote ndani ya CCM wanaishi kwa mawazo kama yako, ya kufanya na kufuata yale yote ambayo chama kinawata kufanya, bila kuweka your value judgement. Hiki unachotuambia kwamba ndani ya vikao vyenu kuna Mawaziri 8 waliojitolea kujiuzulu sio cha ukweli na kitatokea tu kwa shinikizo kutoka vyama vya upinzani na wananchi ila sio kwa shinikizo ndani ya CCM yenyewe. Wanachama wa CCM mnaogopana na huu ni ukweli.
Kuhusu hoja yako ya kwamba kuna mawaziri ambao wanautendaji mzuri na usingependa nao wawajibishwe kwa kumshinika PM ajiuzulu, sidhani kama hili ni tatizo. Kama kuna mawaziri ambao unadhani wana utendaji mzuri sio wewe peke yako ambao umewaona. Rais ambae amewateua pia anao uwezo wa kutambua utendaji wa mawaziri wake. Hivyo kuvunjwa kwa baraza la mawaziri hakuzuii kuchaguliwa tena kwa wale mawaziri wenye utendaji mzuri. Kinachoshinikizwa hapa ni kwa PM kujiuzulu ili hao mawaziri ambao utendaji wa sio mzuri waondolewe. Imeonekana wazi kwamba hawa Mawaziri corrupt wana nguvu sana ndani ya CCM na ni lazima itafutwe sababu ambayo itamuwezesha Rais kuitumia kuwaondoa hao mawaziri, na sababu yenyewe ni PM ajiuzulu na baraza zima la mawaziri lifutike wachaguliwe upya, period.

Baadhi ya wana CCM mmefunga Rais mikono na hawezi tena kutoa maamuzi ya msingi kwa kuogopa aidha lawama au nguvu walizo nazo wana CCM wenye hela. Tumsaidie Rais katika hili. Mshinikizeni PM ajiuzulu kama hao mawaziri corrupt hawataki kujiondoa wenye. Hili ndilo jambo ambalo wapenda nchi kama wewe mnatakiwa kuliangalia na sio kuangalia tu kwamba wewe ni CCM na lazima ufuate kila ambalo CCM inalisema. Mmepewa uwezo wa utambuzi kutambua yaliyo mema na mabaya. Kwa hiyo uwingi wenu (CCM) ndani ya bunge usiwafanye kusaua karama yenu ya utambuzi wa mema na mabaya na kuendelea kuyalea yaliyo maovu.

Ni hayo tu kwa sasa.
 
HK umejisahau. Ukiwa bungeni huwakilishi chama bali wananchi wote wa jimbo lako kwa kifupi ni Watanzania wenye itikadi tofauti tofauti za kisiasa kwa ajili ya kutetea maislahi yao.

Saini yako ilitakiwa kutetea maslahi ya wanyonge wanaoonewa na wezi na pia viongozi wasiowajibika.

Kushindwa kutekeleza hayo ambayo unayaamini ndio UNAFIKI wenyewe huo!
 
Kigwangala kama ungekuwa unakeep records za mambo unayoyaongea, usingekurupuka jinsi hii.
 
Back
Top Bottom