Kwahisani ya watu wa Marekani-Tutafika kweli?

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Ndugu wana bodi,nimekuwa nikijiuliza sana juu ya hili swali na bado mpaka leo sijapata jibu kichwani mwangu labda mnisaidie ili niweze kukituliza kichwa changu kutoka katika kulifikilia hili kila wakati

Kila nisikiapo tangazo lolote lile katika vyombo vyetu vya habari basi mwishowe utasikia kibwagizo kikisema KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI

Je inamaana bila HISANI yao hayo matangazo ama hiyo misaada isingekuwepo? na inakuwaje wamarekani watoe hisani Tanzania wakati kila nikisikiliza habari za USA Watu wake hususani vijana wanalalamika kuwa hakuna kazi na bado wanamahitaji mengi sana ambayo ilitakiwa hisani hiyo Tuipatao Tanzania wangepatia vija wa kimarekani wasiokuwa na kazi wala mwelekeo

Kwa mfano tukikataa Hisani yao wamerikani watatufanya nini? kwani ni lazima kila kitu kiwe ni kwa hisani ya watu wa marekani? ama ndio UKOLONI MAMBOLEO ulivyo.

Wanajamvi ama viongozi wetu wanaogopa kukataa Hisani hizo kwani yaweza tokea ya Libya,maana hakuna ubishi kuwa USA kwa kofia ya NATO ndio waliofadhili kilichotokea Libya

TUTAFIKA KWELI KWA HISANI HIZI ZA WATU WA MAREKANI?
 
Nimekuwa nikitafakari mara kwa mara, asilimia kubwa ya matangazo yanayototela yanamalizikia "KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI", mfano kufunika neti, ulevi ni noma n.k. Ina maana sisi Watz hatujiwezi kwa kiasi hicho kwamba kila kitu kifanyike kwa hisani ya watu hao. Au sisi wenyewe ndio tunaendekeza hali hiyo?
 
mwisho wake itakuwa hadi kuvaa "Mdangi" ni kwa hisani ya watu wa Marekani
 
inawezekana hata wewe umeandika topic hii kwa hisani ya watu wa marekani
 
................ mara JF, "inaletwa kwenu kwa hisani ya .................... :A S embarassed:"
 
Nimekuwa nikitafakari mara kwa mara, asilimia kubwa ya matangazo yanayototela yanamalizikia "KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI", mfano kufunika neti, ulevi ni noma n.k. Ina maana sisi Watz hatujiwezi kwa kiasi hicho kwamba kila kitu kifanyike kwa hisani ya watu hao. Au sisi wenyewe ndio tunaendekeza hali hiyo?
Sentensi yako ya mwisho ndio jibu sahihi!
 
Ahsanteni.sana kwa kunichekesha jioni yangu inaenda shwaaari. Asante hii imewajia kwa hisani ya watu wa marekani.
 
USAID from american people, kama unakula hela ya mlipa kodi wa marekani ni lazima itambulike.
Asiliyake ni pakistan by then watu wanagawa misaada halafu wanajifagilia kwamba wametoa wao kuweka mambo sawa ndio ikaonekana haja ya kutaja cent imetoka wapi hata kama ni thumni.
Magaidi, mafisadi, wauza unga, pombe na magumashi ni mwiko kugusa cent ya mlipakodi wa usa.
 
itafika mahali NIMEOA MKE HUYU KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI!!

Kama unafanya kazi kwenye mashirika ambayo yako direct financed na USA kama NGO's nyingi za sekta ya afya na umeoa baada ya kuanza kazi hapo unapaswa kabisa kusema hiyo ndoa ni kwa hisani ya watu wa Marekani.

Na ni uungwana tu kama ambavyo ukitoa habari hapa JF unaeleza source LOL.
 
Yote yenye kibwagizo hicho ni mambo ya kipuuzi puuzi tu, huwezi kukuta Darasa au Daraja limejengwa kwa hisani ya watu wa Marekani au vitabu shuleni kwa hisani ya watu wa marekani. Wao wanaishia katika kunawa mikono, ulevi noma, tuvunje ukimya tunapotaka kubanguana na upuuzi mwingine wa aina hiyo. Ukifuatilia msaada wenyewe wanatoa vidola vyao milioni 1 na wanatumia 60% kwa mijizi kutoka kwao kuja ku-spy rasilimali zetu kwa kisingizio yanakuja kufanya monitoring ya misaada inayotoa... minyang'au kweli kweli mimarekani na inatumia ujinga wa wachache miongoni mwetu kutudhalilisha.
 
kuna tangazo moja la mke na mume
wanaambiwa wavunje ukimya wazungumze pamoja, halafu linamalizia
kwa HISANI YA WATU WA MAREKANI.
hadi wapenzi kuzungumza ni kwa hisani ya wamarekani.
 
kuna tangazo moja la mke na mume
wanaambiwa wavunje ukimya wazungumze pamoja, halafu linamalizia
kwa HISANI YA WATU WA MAREKANI.
hadi wapenzi kuzungumza ni kwa hisani ya wamarekani.
Bora kutawaliwa kijeshi kuliko kutawaliwa kiakili.
 
Rais wenu yuko madarakani kwa hisani ya watu wa marekani.
Ubongo wake unafanya kazi kwa hisani ya watu wa marekani.
Maamuzi yake anayafanya kwa hisani ya watu wa marekani.


Miaka michache ijayo itakua hata kwenda haja ni kwa hisani ya watu wa marekani.



Sichangii mada...
 
Rais wenu yuko madarakani kwa hisani ya watu wa marekani.
Ubongo wake unafanya kazi kwa hisani ya watu wa marekani.
Maamuzi yake anayafanya kwa hisani ya watu wa marekani.


Miaka michache ijayo itakua hata kwenda haja ni kwa hisani ya watu wa marekani.



Sichangii mada...

Inasikitisha, sijui kwa hili tunawaandaaje watoto wetu (taifa la kesho).
 
Ndugu zetu kumekuwa na kampeni ya hawa watu weupe hususani wamarekani wakitaka kuongeza virutubisho kwenye lishe ya mtoto swali linakuja tumeshindwa kabisa kuwapa vyakula vyetu asilia mungu alivyotujaalia mpaka mmarekani aje aongeze virutubisho vyake vya maabara kutukuzia watoto? Jamani hii misaada mingine tuiangalie kwa jicho la tatu sio kila kitu tunachopewa ni salama kwetu hilo ni angalizo tu sijui wenzangu mnaonaje.
 
Kwa muda sasa kumekua na huu utamaduni wa kila tukisaidiwa ni lazima tumtaje kwa nguvu zote yule alietusaidia..
Je haya pia ni miongoni mwa masharti ya msaada huo? na wakati mwingine huwa sio msaada bali ametupa chake na sisi tumempa chetu lakini bado tuendelee kumtaja na kumtangaza kwa nini kwani yeye pia hututangaza huko kwao au ndio African style??
Mfano shule ya msingi imepata choo l
azima utasikia "kwa hisani ya watu wa marekani
kijiji kimewekewa bomba la maji
lazima utasikia "kwa hisani ya watu wa marekani.
Vyandarua
lazima utasikia "kwa hisani ya watu wa marekani
Dawa za minyoo
lazima utasikia "kwa hisani ya watu wa marekani.
yaani kila kitu
lazima utasikia "kwa hisani ya watu wa marekani

Sijasikia tu hawa watangaza nia kama nao sio kwa hisani ya watu wa marekani....

Je hii "kwa hisani ya ........... inasaidia nini?
je tusipoisema tutapatwa na nini?
kwani nikikupa msaada bila ya wewe kunitangaza kwa watu kuna tatizo gani?

nawasilisha.
 
Back
Top Bottom