Kwaheri mtandao jk karibu mtandao rjk

Mizizi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,275
391
Katika hali isiyofurahisha, baada ya malalamiko kadhaa juu ya kuwepo kwa kupeana madaraka mbalimbali katika ofisi za umma kwa kujuana na kwa kujali uswahiba katika serikali ya JK, baada ya mambo kudorora, kilio hicho kilionekana kusikika na ule mtandao kuonekana kusambaratika, Mtoto wa mheshmiwa huyo RJK amethibitika kuanzisha mtandao mpya ndani ya jumuiya ya vijana ya CCM (uvccm). Habari zilizokuwa za wazi kabisa, Ridhwan amefanikiwa kushawishi na kufanikisha kupanga safu za watendaji, ambao ni makatibu wa uvccm wa mikoa na wilaya kote nchini. Habari zaidi zinaeleza kuwa, lengo kuu la kufanya hayo ni kumuandalia rafiki yake beno malisa kuchukua nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo kitaifa. shutuma zaidi kutoka kwa baadhi ya wanajuiya na viongozi wa chini wanasema kwamba, Ridhwan na Benno walifanikisha kutoa mkopo wa zaidi ya shilingi millioni mbili kwa kila katibu wa mkoa wa jumuiya hiyo ili kupata uungwaji mkono zaidi. lakini baada ya chama hicho kupeleka nafasi ya uenyekiti kupelekwa zanzibar, kasi hiyo ya mtandao ilipungua nguvu.
Zaidi inasemekana kwamba, Ridhwan alishiriki katika kujenga mtandao huo ambao unaonyesha haukuwa na nia ya kujenga jumuiya hiyo. kwani makatibu wengi waliopewa nafasi hizo hawana sifa wala ari ya kiutendaji na hivyo kutoleta mabadiliko yoyote katika jumuiya na chama cha mapinduzi.
Inasemekana na yeye ridhwan ni mgombea katika jumiya hiyo.
 
Ridhwan na Benno walifanikisha kutoa mkopo wa zaidi ya shilingi millioni mbili kwa kila katibu wa mkoa wa jumuiya hiyo ili kupata uungwaji mkono zaidi. lakini baada ya chama hicho kupeleka nafasi ya uenyekiti kupelekwa zanzibar, kasi hiyo ya mtandao ilipungua nguvu.
Zaidi inasemekana kwamba, Ridhwan alishiriki katika kujenga mtandao huo ambao unaonyesha haukuwa na nia ya kujenga jumuiya hiyo. kwani makatibu wengi waliopewa nafasi hizo hawana sifa wala ari ya kiutendaji na hivyo kutoleta mabadiliko yoyote katika jumuiya na chama cha mapinduzi.
Inasemekana na yeye ridhwan ni mgombea katika jumiya hiyo.

Kumbe huyu kijana ujanja wake woote ni kwenye siasa za makundi? Hakuna la zaidi analoweza kuisaidia nchi hii kama kijana wa kitanzania bila kuwagawa na kuwatawala vijana wenzake? Job true true
 
Habari hizi hazina msingi na pia hazivutii.Ni habari za kupandikiza chuki na fitina ndani ya CCM na UVCCM.Laiti zingekuwa ni habari za uhakika ningepata raha kwa sababu zinaivunja vunja CCM lakini nahisi hazina ukweli.
 
Alnadaby,
Nadhani si jambo jema kulipuuzia jambo hili bila kuomba ufafanuzi zaidi, Nadhani unajua kama ridhwani ni mtoto wa Mkuu wa nchi, kwa hiyo ushawishi wake mbele ya vijana wenzake ni mkubwa zaidi. Unadhani ni busara kwake yeye kutoa ufadhiri kwa kijana mmoja katika harakati za kisiasa na kumuunga mkono asilimia kwa mia na kuwaacha wengine? pia katika mkakati huo, ridhwan alikuwa anaandaliwa kuteuliwa kuwa katibu muhamasishaji wa UVCCM taifa.
 
Basi lete data za uhakika tukuelewe.Yeye kama mwanasiasa ana mtu anayemuunga mkono,sasa hawezi kumfanyia kampeni kila mtu!Na hili la kugawa fedha unahitaji ushahidi wa kutosha kuthibitisha hilo.
 
Kwa habari nilizonazo, anagombea uwakilishi wa UVCCM katika baraza kuu la Taifa kutoka kwao pwani. pia anaandaliwa kuteuliwa kuwa katibu muhamasishaji wa umoja huo kitaifa
 
Babu yake Yusuf Kikwete amebwagwa kwenye uchaguzi wa wazazi pwani, sintashangaa Ridhwani na vijisenti vyake toka EPA na yeye akabwagwa huko vijana!!
 
Babu yake Yusuf Kikwete amebwagwa kwenye uchaguzi wa wazazi pwani, sintashangaa Ridhwani na vijisenti vyake toka EPA na yeye akabwagwa huko vijana!!

Hao vijana wana "nguvu" si wakupuuza....remember kilichotokea kule Kizota,Dodoma mwaka Jana 2007?Benno Malisa hakutarajiwa.....ilikuwa...hao ndio RJK na Benno very close friends from UDSM.............

By the way...
kuhusu hayo ya kugawa 2m,japo inawezekana kwa hawa jamaa, ushahidi wa kutosha unahitajika

//Baba Jei
 
Back
Top Bottom