Kwa yeyote mwenye shida ya sheria za kazi

Nimefanya kazi kwa mwaka mzima naingia saa1 asubuh natoka saa 12 au saa2 usiku silipwi Overtime sheria inasemaje?
Yeyote anaefanya kazi zaidi ya Masaa nane (tisa ikiwa ni pamoja na mda wa mapumziko) Masaa yote baada ya hapo yatakuwa ni Masaa ya ziada na yatalipiwa kama Masaa ya ziada
 
Ndio maana nikasema ni sehemu ya mkataba kwa sababu appointment ni uteuzi anaeteuwa ndio anasaini kudhibitisha uteuzi ambao ufwata misingi ya mkataba mkuu
 
Naomba ufafanuzi katika ELRA 2004 kifungu cha 40 (1) &(2) kuhusu unfair termination. Compensation inayozungumziwa kifungu cha (2) ni miezi 12 tu au pamoja na mshahara yako tangia unafukuzwa hadi hukumu? Manake wanasema is not substitute to any other amounts! Hizo other amount ni pamoja na mshahara au yenyewe haihusiani?
 
chumvichumvi,
Nisaidie hili, Mtumishi mmoja wa idara ya Elimu , "alitoroka" kituo cha Kazi kwa kupata barua FEKI ya Uhamisho toka Kituo /Shule mmoja mjini Mwanza na kwenda Kufundisha Shule fulani moani Morogoro , Ulipokuja uhakiki wa watumishi ilibidi arudi Mwanza ambako alipewa charge sheet na TSD kwa kuwa amesimamisha na atapokea Nusu Mshahara , akapewa siku14 kuwa amejitetea kwa nini asifukuzwe kazi.

Likajazuka la uhakiki wa watumishi , akapelekwa TAKUKURU ambako aliamriwa kurejesha pesa alizopokea akiwa nje ya kituo chake cha Kazi ambako anahesabiwa "MTORO" , akiwa anafanya hivyo , ile nusu Mshahara pamoja na Account yake ya Bank ZIKAFUNGWA hivyo pesa ya nusu mshahara ikio bank Marejesho ya pesa alizotakiwa kurejesha alisha maliza kurejesha Mpaka leo hajapata majibu ya TSD na Pia mkurugenzi wa Mji haja mpatia barua kutamka kuwa amefukuzwa kazi hivyo yupo ana "hang" bila kujua hatima yake , akienda kwa HR aanambiwa hilo ni agizo toka ngazi za juu.

IPI FATE YA MWALIMU HUYU KIUTUMISHI
Asante
 
Mimi niliajiriwa kwa sifa ya Diploma kwa kuwa nafasi ya kazi ilitaka mtu mwenye sifa iyo japo mimi nilikuwa tayari nina sifa ya juu zaidi ya Diploma sasa ni vipi naweza kufanya ili nianze kutumia cheti changu cha juu ili nilipwe mshahara mpya? Pia ni muda gani MTU anaweza pandishwa cheo kwa mtumishi Wa serikali?
 
Kuna ndugu yangu mwalimu amepandishwa cheo mara moja lakini mshahara wamemdabo mara mbili yaani kwa cheo hasichostahili, aliandika barua arudishwe kwenye daraja lake ni miezi mitano imepita hawajafanya marekebisho. Je endapo watamrudisha daraja lake na kumkata fedha atapataje msaada kisheria wakati makosa si yake?
 
Wanajamvini wenzangu kwa yeyote mwenye shida na masuala ya sheria za kazi awe huru kuniuliza.

Karibuni!
Ndugu habari! Naomba msaada je hatua gani mwajiri anapaswa kuchukua juu ya mtumishi ambaye anatuhuma za kumuibia mwajiri kwa kugushi nyaraka za malipo? Aidha kesi bado kufunguliwa Ila iko police? Je akisitishiwa ajira ni wrong termination? Please help me with this.
 
Asante kwa uzi huu. Kuna askari waliachishwa kazi miaka 3 iliyopita na walikua na kesi ya jinai na sasa wameshinda. Je wanawezaje kufungua shauri dhidi ya IGP kuomba ashinikizwe wardi kazini?
 
Mwajiri wao anapaswa kuitisha kikao cha kamati ya nidhamu kilichowatoa kazini kufanya marejeo ya adhabu waliyoitoa dhidi yao kufuatia hukumu iliyotoka na kuwarudisha kazini na kuwalipa haki zao. Asipofanya hivyo basi wana haki ya kwenda mahakamani
 
Ndugu habari! Naomba msaada je hatua gani mwajiri anapaswa kuchukua juu ya mtumishi ambaye anatuhuma za kumuibia mwajiri kwa kugushi nyaraka za malipo? Aidha kesi bado kufunguliwa Ila iko police? Je akisitishiwa ajira ni wrong termination? Please help me with this.
Unfair termination ina ingredient mbili
Je sababu ya kukuachisha kazi ni reasonable?
Je wakati wanakuachisha kazi walifuata procedure?

Kwa hoja uliyoleta sababu ya ku terminate ajira yake mwajiri ana sababu ya msingi kufanya hivyo kwani wizi ni mojawapo ya serious misconduct inayokubalika kisheria. Kwa mantiki hiyo hoja ya kwanza inamruhusu kufanya maamuzi hayo aliyochukua.

Hoja ya pili, je kabla ya kumfukuza kazi mtuhumiwa aliitwa kwenye ksmati ya maadili na kupewa nafasi ya kujitetea juu ya tuhuma hizo? Kama hilo halikufanyika pamoja na kwamba alikuwa na sababu ya msingi 'serious misconduct' maamzi yoyote yalichukuliwa dhidi ya mtuhumiwa ni batili hivyo ni unfair termination

Lakini kama alipewa nafasi akajitetea 'principle of natural justice' ilichukua mkondo wake basi termination is fair.
Na inatakiwa na sheria apewe barua ya kumu terminate

KAMA TERMINATION ILIKUWA UNFAIR ANATAKIWA KISHERIA NDANI YA SIKU 30 KUPELEKA MGOGORO CMA HATA KAMA AMESHITAKIWA NA KESI YAKE MAHAKAMANI BADO INAENDELEA
 
Richard Chomile,
Waliitwa kwenye kamati ya maadili wakaambiwa haki ya kuleta mashahidi, wakili na wakaulizwa kama wapo comfortable wakajibu ndiyo, kikao cha maadili kikafanyika, wakajitetea kwa kukana tuhuma, vielelezo vya mwajiri vikaonyesha wana hatia, wakatafutwa wakafate majibu ya kikao cha nidhamu hawakutokea, wakaandikiwa termination letter. wameenda cma kushtaki kwa unfair termination.
 
Naomba ufafanuzi katika ELRA 2004 kifungu cha 40 (1) &(2) kuhusu unfair termination. Compensation inayozungumziwa kifungu cha (2) ni miezi 12 tu au pamoja na mshahara yako tangia unafukuzwa hadi hukumu? Manake wanasema is not substitute to any other amounts! Hizo other amount ni pamoja na mshahara au yenyewe haihusiani?
Miezi 12 na mbili na kuendelea hiyo ni compensation mara nyingi unakuta muajiriwa anamdai muajiriwa wake pesa zingine mfano mishahara ya miezi iliyopita na kadhalika ambayo kwa ujumla wake huwa Arrears na ndipo neno not substitute linatumika meaning compensation haizuii mtu kulipwa arrears zake
 
Asante kwa uzi huu. Kuna askari waliachishwa kazi miaka 3 iliyopita na walikua na kesi ya jinai na sasa wameshinda.Je wanawezaje kufungua shauri dhidi ya IGP kuomba ashinikizwe wardi kazini?
Ndio wanaweza kufungua shauri na sababu ya wao kuchelewa kufungua shauri la kazi iwe ni hiyo jesi ya jinai ila anatakiwa kufunguliwa mashtaka sio IGP bali jeshi la polisi
 
Naomba kujua hili kisheria because nimeachishwa kazi sasa nahitaji kudai fidia zangu kupitia mahakama. Nilipoenda kwenye chama cha wafanyakazi ili kuanza process za kufungua mashtaka nilihitaji kudai muda wangu wa ziada sababu tangu nianze kazi huwa nafanya masaa 48 kwa week badala ya 45.

Sasa katibu wa chama ananipa tarifa kwamba overtime huwa inaisha ndani ya siku 60. Kisheria nahitaji kujua hilo? Pia kupatiwa usafiri, mimi binafsi nilikuwa natumia usafiri kwa gharama zangu ila sikuwahi kuhoji, je nina haki ya kudai fidia ya gharama zangu za usiku? Naomba kufahamu hilo!

Shukrani mkuu
 
Watakuja Wahusika
 
Attachments

  • 1476170155639.jpg
    1476170155639.jpg
    39.8 KB · Views: 129
Naomba kujua hili kisheria because nimeachishwa kazi sasa nahitaji kudai fidia zangu kupitia mahakama. Nilipoenda kwenye chama cha wafanyakazi ili kuanza process za kufungua mashtaka nilihitaji kudai muda wangu wa ziada sababu tangu nianze kazi huwa nafanya masaa 48 kwa week badala ya 45.

Sasa katibu wa chama ananipa tarifa kwamba overtime huwa inaisha ndani ya siku 60. Kisheria nahitaji kujua hilo? Pia kupatiwa usafiri, mimi binafsi nilikuwa natumia usafiri kwa gharama zangu ila sikuwahi kuhoji, je nina haki ya kudai fidia ya gharama zangu za usiku? Naomba kufahamu hilo!

Shukrani mkuu
Pole sana kwa hayo yaliyokukuta ni kweli issue yeyote inayohusiana na mshahara mda wake wa madai ni siku 60 ila panapo sababu ya msingi mdai anaweza kuomba tume kufanya madai nje ya muda
 
Kuna mwenyewe swali juu ya masuala ya kazi
Ukiwa na tuhuma fulani kazini, na ukasimamishwa kazi kupisha uchunguzi, je uchunguzi huo unachukua muda gani kisheria? Na je muda huo ukipata bila tume ya uchunguzi kufanya chochote wala kutoa maamuzi yoyote nini kifanyike au sheria inasemaje kuhusu hilo?
 
Back
Top Bottom