Kwa wazazi: soma hapa tafadhali

Kusema ukweli ile habari ilinivunja moyo halafu binti mwenyewe alivyokuwa anafanana na mamake!! Mh hata sijui tufanyeje hapo usikute alionywa kidogo tu akaona anaonewa. Nadhani kwa staili hii itabidi tuwe tunawaonya watoto wetu kwa kuwalia timing kama tunavyofanyaga kwa spouses wetu!! unasubiria kwenye good mood ndo unaanza lakini mwanangu, siku ile kusema ukweli sikufurahia...........

Sure MJ haya mambo yanatisha

Hiyo signature yako nimeipenda .all the best
......Frankly Speaking If this is a dream, I just Wanna keep on dreaming...I Do Love You...S.M.L 2011
 
Kwanza nikushukuru Kwapwani na wale wote waliochangia mada hii, Nimepata faraja moja kubwa sana kuwa wapo watu ambao wanatafakari namna bora ya makuzi ya watoto, tuendelee na kazi hii ngumu na wala tusichoke wala kukata tamaa. ila napenda kuongezea kuwa katika malezi haya na hasa katika kujenga mahusiano kati ya mzazi na mtoto ni wajibu au ni vyema na inapendeza sana kushirikishana wazazi wote wawili yaani baba na mama, maana naamini tumekulia katika tamaduni tofauti na mapokeo ya maisha pia ni tofauti itakuwa ni jambo la busara mkikaa kama wazazi na kuweka mikakati ya pamoja ya namna bora ya kulea watoto hasa ukiangalia changamoto za maisha. kuna njia nyingi za kufundishana siku hizi vipeperushi vimejaa vya namna ya kufungua amongezi, usiseme umechelewa hata sisi na uzee huu naamini tunatamani wazazi wetu wawe karibu zaidi na sisi waoneshe kutupenda, kutusikiliza na kutuamini kile tunachowaambia. unaweza pi search parental child communication kwa maelezo zaidi.

Mungu Awajae zekhi na baraka tele wazazi wote na wape subira na uvumilivu katika malezi.
 
Swali la 2 ni: How to balance! kuwa mzazi/rafiki/mshauri kwa watoto wetu? hii siku nyingine wapendwa.
Nakubali kukosolewa ili nijifunze zaidi
Mix with yours

Mzazi mwenzangu - Kapwani nimesoma uzi wako na kuuelewa vizuri. Analopanga Mungu uwezi kuzuia, ila kwa kujaribu - napenda kujibu sali lako la pili la namna ya kubalance. Mara nyingi wazazi hatuna ratiba na watoto wetu katika maisha tunayoishi. Malezi tumewaachia watu ambao - they are after money - Mtoto anaamka asubuhi anaenda shule, akitoka shule - anaondoka tena kwenda tuition, akitoka tuition ndo muda wa kucheza kidogo, ratiba ya siku imeisha anakula chakula cha usiku na kulala au labda kama muda unaruhusu wengi utawakuta wakiwa kwenye runinga - kinachooneshwa kwenye TV zetu majibu tunayo - ni michezo ya runinga isiyokuwa edited kwa ajiri ya watoto.
Wazazi tujenge mazingira ya timetable - baadhi ya siku tukae na watoto tuwafundishe wenyewe. Siku nyingine kuhojiana nao maswali mbalimbali, siku nyingine kutoka nao out (sio kwenda kanisani) . Tukijenga ukaribu wa namna hiyo kwa watoto - watoto watakuwa huru kutoa mawazo yao kwetu sisi wazazi.
Mimi nililelewa na mama - baba alikuwa mbali na nyumbani kikazi - lakini nilikuwa na ukaribu na mama yangu - hadi sasa ambapo niko mbali na mama nina mawasiliano ya karibu sana na mama zaidi ya baba. Upendo wa utotoni unadumu sana kwenye ubongo wa mtoto.
Wa kuongeza aongeze na wa kunisahihisha simkatazi.
 
kutokana na maelezo ya mama na dada wa binti aliejinyonga pamoja na majirani, kunauwezekano kuwa binti alikuwa na ujauzito, alijaribu kutoa ikashindikana akaamua kujiua, siku moja kabla ya kujiua alikuwa amejifungia ndani muda mrefu, dada yake alikuja jioni na kumgongea mlango lakini alichukua muda mrefu kufungua, haijulikani nini alikuwa akifanya, inaonyesha ndo siku aliyojaribu kutoa mimba, usiku wake mama yake alimuona katika hali ya utulivu sana hakuwa akiongea na mtu, akamuuliza lakini mtoto akasema kuwa hakuna shida, siku ya kijiua alikwenda bafuni kuoga kama vile anajiaanda kutoka kwenda kwenye shunghuli zake.
swala linaloshangaza nikuwa alikutwa na kamba ya kujinyongea shingoni lakini hakuwa amejitundika popote kama ilivyo kawaida ya watu wanaokutwa wamejinyonga, maiti ilikutwa nyuma ya mlango ikiwa imezua mlango kwa ndani, kutoka damu sehemu za siri, majimaji.
Kuna maswali mengi ambayo familia na majirani wakiulizwa unaweza kupata majibu sahihi katika hili

Huu ni mtazamo wangu, polisi nao watakuwa na yao.
 
Asante kwa taarifa hii, sikuwa na taarifa hii kwa urefu.....ila nili doubt kuwa alipata tatizo linalohusu relationship ya mapenzi au mimba....at her age, swala la mimba lilikuwa na kila sababu ya kuchanganya sana maskini.....kumbuka pia alikuwa anashinda somewhere mchana kutwa anajifunza kushona...huwezi kujua huko alikuwa anafanya nini!!! imeniuma sana kama mama, maana nami nina kabinti ka miaka 5....imenisikitisha sana

mix with yours
 
Kwanza nikushukuru Kwapwani na wale wote waliochangia mada hii, Nimepata faraja moja kubwa sana kuwa wapo watu ambao wanatafakari namna bora ya makuzi ya watoto, tuendelee na kazi hii ngumu na wala tusichoke wala kukata tamaa. ila napenda kuongezea kuwa katika malezi haya na hasa katika kujenga mahusiano kati ya mzazi na mtoto ni wajibu au ni vyema na inapendeza sana kushirikishana wazazi wote wawili yaani baba na mama, maana naamini tumekulia katika tamaduni tofauti na mapokeo ya maisha pia ni tofauti itakuwa ni jambo la busara mkikaa kama wazazi na kuweka mikakati ya pamoja ya namna bora ya kulea watoto hasa ukiangalia changamoto za maisha. kuna njia nyingi za kufundishana siku hizi vipeperushi vimejaa vya namna ya kufungua amongezi, usiseme umechelewa hata sisi na uzee huu naamini tunatamani wazazi wetu wawe karibu zaidi na sisi waoneshe kutupenda, kutusikiliza na kutuamini kile tunachowaambia. unaweza pi search parental child communication kwa maelezo zaidi.

Mungu Awajae zekhi na baraka tele wazazi wote na wape subira na uvumilivu katika malezi.

Wakati nakua sikujua kama kulea ni very challenging.....nina mtoto 1 tu lakini duhhh sijui nikiwa na katimu kadogo nita manage vipi na kazi za kuajiriwa na kaburu hizi...muda na mtoto + nyumbani ni wa kusaka sana..kuna wakati natamani ningekuwa mama wa nyumbani....yaani acha tu

mix with yours
 
Kwa kweli ni muhimu sana wazazi wa sasa kuwa karibu na watoto wetu kwani hatari ambazo zinawazunguka watoti wetu ni nyingi,hasa kwa wenye watoto wa kike hatari pale nyumbani ,hatari barabarani na hata huko shuleni.Ni muhimu kuwa karibu na watoto wetu ili waweze kutuuliza na sisi ndio tuwe watu wa kuwapa majibu ya maswali mengi waliyonayo kuliko wapate majibu hayo kutoka kwa watu wengine ambao wanaweza kumpotosha.

Ni kweli kama utasoma paper za Leshabari wa Muhimbili utaona kuwa peers ndio watoa taarifa namba wani......it is very shame kuona hadi sasa kuna wazazi wanawasukumia mashangazi au wa bibi au rafiki zao kuongea na watoto wao namna ya kujisitiri ukiwa kwenye siku zako....sasa shughuli inakuja pale ambapo huyo shangazi ni shankupe....anamfundisha hata asiyostahili kujua katika stage hiyo...

mix with yours
 
Asante sana Kapwani..
Kwa hii Post yako nakumbuka machungu yaliyonipata nikiwa na umri mdogo sana13-15 lakini kwa sababu wazazi wetu enzi zile hawakutuweka karibu sana ..walijenga mazingira ya sisi kuwaogopa hata ukiwa na jambo kumuanza unaona issue sana unajihoji mara mia
Sitasahau ...sitasahau
Kabinti kangu sasa kanasoma baby class najitahidi kuwa karibu nae nimwelewe hatua kwa hatua katika ukuaji wake hata sasa akitoka shule ananipa vituko na viugomvi vyao vya kitoto nafarijika.Pale napoona kakosea namwambia tu hapa sio hivi mwanangu ...
Nitajitahidi kuwa karibu nae siku zote za maisha yangu.

Inasikitisha

Pole kwa yaliyokupata dear...nami nakumbuka siku moja nilichezea majani ya magimbi baadae nikajishika sehemu*****kwa bahati mbaya nadhani nilikuwa na miaka 9 ivi, basi nikajisikia kuwashwa sana na maumivu ....nikaamua kumweleza mama kuwa najisikia hali hii mahali hapa....looh aliniuliza tu swali moja...je umeshaanza kucheza na wavulana.....maskini sikuwa hata na idea hiyo nikajibu kwa hofu hapana....jamani mama akakaa kimya, hakunikagua wala kufanya lolote ( kumbuka sikuwa nimwemwambia habari ya najani yale).....next day akasema bado unaumia nikajibu no nae akala kona..... basi sikukata tamaa nikatamani sana kujua why nilipatwa nahali ile....baadae wenzangu wakaniambia kuwa ni utomvu wa majani ya magimbi na kuniasa nisishike tena

mix with yours
 
Mie niko karibu sanasana kwa kweli, kitu chochote lazima aniambie yaaani, na ninamweleza wazi mambo ya dunia yalivyo, tangu hivi na umri mdogo, kwa hiyo hata akikua nitaendelea hivihvi, sasa mie nina ndugu zangu ni wakali hatar, utakuta watoto wao wanakuwa karibu na mie na kunieleza mambo mengi kuliko hao wandugu, na mie natumia nafasi hiyohiyo kuwapa mafunzo ya dunia inavoenda na kuwa kama mwongozo bila kuwasemea au kuwakaripia

Kwa huyo mtoto itakuwa tu mambo ya wanaume tu, mtoto akiingia uteenager usipokuwa na busara unaweza ua, sababu wanakuwa wanafikiri wanajua kuliko wewe, yaani wanaweza mwona mzazi kama mshamba fulani hv, inabidi uwe na zaidi ya busara kuweza kuwa handle hawa watoto

Dear hii itakusaidia sana ....just play ua pati yaliyo beyond tumwachie MUNGU. Usiahahu pia kumu orient na mambo ya MUNGU...kwa wakristo sunday school na Bible discussion nyumbani ni nzuri ....kwa ndugu zangu waislamu mtanisaidia nyie mnafanyaje zaidi ya ile training ya chuo

mix with yours
 
Ahsante sana mpendwa kwa hilo, huu ni ukweli usipingika,mimi niliona taarifa hiyo ilisikitisha sana, ila kinachonishangaza sana ni kuona damu, hivi kweli mtu akijinyonga anatoka damu au kuna kitu kimejificha hapo!!!!!
...Tuko pamoja nami pia hiyo ilinishangaza kidogo. Niliwahi kushuhudia bwana mmoja amejinyinga miaka ya 80 lakini sikuona akitokwa na damu kwa hiyo hata kwa yule binti kuona ametoka damu ilinishangaza at least kwa mkojo inaeleweka maana kule ku-suffocate lazima matundu yaweza kutoa kutoa some discharge!!!..I thought some fishy thing was behind the whole story!!!...
 
Pole kwa yaliyokupata dear...nami nakumbuka siku moja nilichezea majani ya magimbi baadae nikajishika sehemu*****kwa bahati mbaya nadhani nilikuwa na miaka 9 ivi, basi nikajisikia kuwashwa sana na maumivu ....nikaamua kumweleza mama kuwa najisikia hali hii mahali hapa....looh aliniuliza tu swali moja...je umeshaanza kucheza na wavulana.....maskini sikuwa hata na idea hiyo nikajibu kwa hofu hapana....jamani mama akakaa kimya, hakunikagua wala kufanya lolote ( kumbuka sikuwa nimwemwambia habari ya najani yale).....next day akasema bado unaumia nikajibu no nae akala kona..... basi sikukata tamaa nikatamani sana kujua why nilipatwa nahali ile....baadae wenzangu wakaniambia kuwa ni utomvu wa majani ya magimbi na kuniasa nisishike tena

mix with yours
....Kapwani unachosema nakiona mara kwa mara kwa my wife wangu.Tuna mabinti wawili 1st born ni 9 years na 2nd born ni 6 yrs. Huyu mdogo yeye akiwashwa kidogo mbio kwa mama yake kumuonyesha tena anavua na chupi kabisa. Nilichogundua kwa mke wanguni hofu kubwa inayomkumba kwa hiyo humpekenyua sana na maswali mengi. Kwa kweli nami pia nashawishika kuwa amakini na mienendo ya watoto wetu lakini tusikimbilie sana kutumia mabavu katika kutafuta ufumbuzi ni hatari.
 
Back
Top Bottom