Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

ok thanks hivo anatakiwa awe na ratiba yenye uwiano mzuri na anyonye kwa kiasi au kwa siku mara ngapi?
Chakula chochote kwa mtoto mdogo ni kati ya mara tano na sita kwa siku, hivyo gawa masaa ya kula
 
Kuhusu Kumuogesha mtoto :Ni muhimu kumwogesha kila siku uogeshaji unategemea umri na wakati ,kwa mtoto mchanga siku tatu hadi tano za mwanzo..... jitahidi mfunike vizuri kwenye taulo kavu uwe na vitambaa vidogo dogo ambavyo utavitumia kumfuta tandika taulo safi miguuni pako na hakikisha chumba kiwe na joto la kutosha funga madirisha na milango,uwe umetayarisha maji vuguvugu tumia utaratibu wa kumfuta kwa kitambaa laini usoni huku ukijitahidi kusupport kichwa chake mkaushe,mfute kichwani mkaushe awe mkavu ,mfunue taulo mfute pia kwa maji vuguvuvu ukiwa makini sehemu zilizo na mikunjo mkaushe mfunike malizia miguuni na pia mkaushe vizuri na kumfunika.Ni vizuri ukatumia sabuni zisizo kali na umpake mafuta ya nazi uliyoyaandaa nyumbani maji ya kuoga mtoto jitahidi uchemshe kama ya kunywa mapema na uache yapoe au uwe na yaliyochemshwa na kupoa kwa ajili ya kuzimulia,kiwiko cha mkono kitumike kupima uvuguvugu wa maji mtoto anapoongezeka uzito unaweza ukaandaa mahali maalumu mezani mahali ambapo vifaa vya mtoto vya kuogea vitatunzwa kumbuka kumsafisha pua na masikio kwa kutumia pamba maalumu a pia kumvalisha nguo kavu na zilizonyooshwa kuuwa vijidudu.
pamba maalum ni cotton pads ama zipi mkuu?
 
Umegusia engo moja muhimu sana lakini kuna wazazi huzaa watoto wasio na tatizo kabisa lakini mzazi akaja kumsababishia mtoto ulemavu au tatizo lingine lolote
Kwa mfano haishauriwi kabisa kumzaba mtoto vibao vya masikioni unaweza kumletea ulemavu wa kutosikia au kumlaza mtoto upande mmoja muda wote huleta tatizo la chogo au kichwa bapa au kilichobonyea upande
du hivi mtoto mchanga hulazwa kifudifudi ama chali ili alale vizuri/
 
Hili jambo nimekuwa najaribu kusema lakini wazazi wetu yani wakwe na mama zetu huchangia sana kuumiza watoto ktk eneo hili kwa kisingizio mtoto anahitaji joto mtoto huwa hasikii joto wanashindwa kuelewa dar ni tofauti pengine na mkoani ulipozaliwa wewe au bibi huyo alipokuzia watoto wake wengine unaenda clinic daktari anakushangaa jinsi ulivyomjaza mtoto nguo nyingi kabaki macho tu.wazazi tuwe makini hawa ni wakubwa zetu ila panapobidi kuwaelewesha tufanye hivyo vinginevyo ni sisi ndio tunakuja kupata shida na watoto wetu badae.

Umenikumbusha mama yangu. Alikua ananiambia nimjaze mtoto manguo mengi sasa unakuta mtoto anasweat mwili mzima mpaka akapata vipele mwilini sasa na manguo tunayomjaza akianza kusweat vile vipele vinamuwasha analia basi naanza kubishana na mama kumpunguza mtoto nguo ni ataongea hapo namwambia muache tu akipata pneumonia ntaenda nae hospital tumfunue. Basi mpaka sasa hiv namvalisha mtoto nguo kawaida ila anaona ndo mtoto ataumwa.

Sababu mimi alinilelea kilimanjaro kwenye baridi basi anataka na mwanangu ninaemlelea Dar nimvike manguo mengi pia.
 
mmmmm lkn mara madactari wanasem mtoto apewe suna mapema sasa da kaka mshana tufanyeje kinamama sisi ?
Wanachohofia ni maambukizi hasa UTI
59778ed0923f466e6c1498e13b0c8ffc.jpg
ac4fc503577d2d2f3256dba74f8e3811.jpg
 
Umenikumbusha mama yangu. Alikua ananiambia nimjaze mtoto manguo mengi sasa unakuta mtoto anasweat mwili mzima mpaka akapata vipele mwilini sasa na manguo tunayomjaza akianza kusweat vile vipele vinamuwasha analia basi naanza kubishana na mama kumpunguza mtoto nguo ni ataongea hapo namwambia muache tu akipata pneumonia ntaenda nae hospital tumfunue. Basi mpaka sasa hiv namvalisha mtoto nguo kawaida ila anaona ndo mtoto ataumwa. Sababu mimi alinilelea kilimanjaro kwenye baridi basi anataka na mwanangu ninaemlelea Dar nimvike manguo mengi pia.
Ila kumbuka hizi ni sehemu mbili tofauti zenye hali ya hewa tofauti hivyo zingatia sana ishu ya vyakula na mavazi
 
wakuu wa humu ndani naomba msaada.naina mtoto wa mwaka na miezi mitano,ila ana kilo nyingi sana kilo 17.je ni sahihi na kama si sahihi nimfanyeje apungue.ankula vyakula vya kawaida tu na kunyonya kwa sana.kliniki mama yake anampeleka ila wanamwambia atapungua akikua. kwa mwenye taaluma anisaidie
 
Dada angu alikuwa na mtoto kama huyo 2005, akashauriwa ampunguzie vyakula na ziwa.
Akapungua
 
Nadhani ushauri wa kliniki ni sahihi ila mwepushie vyakula vya mafuta kwa wingi pia mtafutie michezo itakayomfanya awe na movements
 
Dada angu alikuwa na mtoto kama huyo 2005, akashauriwa ampunguzie vyakula na ziwa.
Akapungua
nashukuru.ila huyu mtoto wangu ni mkorofi anaponyimwa ziwa na mama yake hulia sana na kwa sasa humpiga hata mama ake wakati anapodai kula au kunyonya
Nadhani ushauri wa kliniki ni sahihi ila mwepushie vyakula vya mafuta kwa wingi pia mtafutie michezo itakayomfanya awe na movements
asante ndugu ndugu mshana jr' ,mara nyingi hula ugali maharage na mboga za majani.
aaq.jpg
 
Habari mihangaiko humu, naomba kueleweshwa na tiba yake kuhusu mtoto mchanga sababu ya kucheua maziwa huku mengine yakitokea puani.
 
Wengi wetu humu tunalea ama watoto wetu ama watoto wa ndugu jamaa na marafiki.

Tumekuwa na mada maalum nyingi za mambo tofauti kama urembo magari simu n.k. lakini hatujawahi kuwa na mada hii maalum ya watoto.

Kumlea mtoto tangu kutungwa kwa mimba mpaka kuzaliwa na hatimaye kulelewa mpaka kuvuka kile kipindi cha hatari si jambo dogo.

Changamoto ni nyingi hasa na zingine hatujui jinsi ya kuzitatua lakini tukiwa na hii mada hapa jukwaani tutashirikishana na kujuzana mengi kwa haraka na uhakika zaidi.

Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji daktari au ufumbuzi wake ni kama huduma ya kwanza kabla hujapata usaidizi mwingine. HII NI TOFAUTI NA JF DOCTOR.

Kwa mfano, ufanyeje;

-Mtoto anapolialia
-Mtoto anapopata gesi tumboni
-Mtoto anapopaliwa kila akila chochote
-Mtoto anaposhtuka shtuka usiku na kulia sana nk k

Hatari zimnyemeleazo mtoto;
-Umeme
-Maji
-Moto
-Mwanga wa Tv
-Simu, mawimbi yake
-Vyombo na vitu mbalimbali
-Madawa na vipodozi nk nk

Hii ni mada pana yenye mambo mengi mno.

Kwa mfano kitunguu saumu ni tiba kwa mtoto anayelia na kushtuka usiku, Kijiko cha asali ni tiba kwa mtoto anayekohoa mfululizo (ukiacha kifua na mafua), Vitu kama mahirizi ya kiunoni na mkononi havimsaidii mtoto, Muda mwingi kumvalisha mtoto nguo nyingi humsababishia nimonia n.k.

Mambo ni mengi...

IKIWAPENDEZA ITAKUWA NI MADA MAALUMU YA WATOTO..

Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha..!
Hujafafanuwa vizuri bado Kitungu saumu anapewamtoto wa umri gani? na je Asali anapewa mtoto wa umri gani?sio kila mtoto anapewa kitunguu saumu au Asali? utakuja kuwadhuru watoto wa watu Mkuu@Mshana jr samahani kama nime kukwaza.
 
nashukuru.ila huyu mtoto wangu ni mkorofi anaponyimwa ziwa na mama yake hulia sana na kwa sasa humpiga hata mama ake wakati anapodai kula au kunyonya

asante ndugu ndugu mshana jr' ,mara nyingi hula ugali maharage na mboga za majani.View attachment 459816
Mmh mbadilishie diet na jitahidi kumfanya active...aisee ni bonge la kidume HONGERA
 
Hujafafanuwa vizuri bado Kitungu saumu anapewamtoto wa umri gani? na je Asali anapewa mtoto wa umri gani?sio kila mtoto anapewa kitunguu saumu au Asali? utakuja kuwadhuru watoto wa watu Mkuu@Mshana jr samahani kama nime kukwaza.
Sijaspecify umri ni kweli kabisa ila hii mada ni ya kushare uzoefu kwahiyo naomba tushirikiane
 
Hujafafanuwa vizuri bado Kitungu saumu anapewamtoto wa umri gani? na je Asali anapewa mtoto wa umri gani?sio kila mtoto anapewa kitunguu saumu au Asali? utakuja kuwadhuru watoto wa watu Mkuu@Mshana jr samahani kama nime kukwaza.
Ni kweli kabisa kaka ila sidhani kama kuna mzazi/mlezi anaweza kumpatia tu mtoto kabla ya kuuliza vema na kupata ufafanuzi kama nilivyofanya kwa wengine wengi
Naamini hujanikwaza kwakuwa lengo letu sote ni moja KUJENGA
 
147 Reactions
Reply
Back
Top Bottom