Kwa watu wa mkoa wa Mara

Tunabaguliwa natunabaguana jaribu kuangalia mabango ambayo yapo kwenye mpaka wa Mara/mwanza sasa Simiyu BANGO la Kutokea Mara kuingia Mwanza linasomeka hivi; KARIBU MKOA WA MWANZA na kisha angalia bango la kutokea mwanza kuingia Mara linasomeka hivi ; SASA UNAINGIA MKOA WA MARA as if kuna tahadhari unatakiwa kuwa nayo unapokuwa mara huu ni ubaguzi mkubwa sana tunaofanyiwa wana mara wote uwe mwana siasa ama not unabaguliwa hivyo
 
Na Mie nipo mbele yenu kwa 100%. Imagine mji kama bunda next to national park haina hata hotel za maana. Watalii wanarudi arusha wote. Kwetu karukukere ndo kama zizi la ng'ombe
 
Ni matumaini yangu kuwa mpo salama,kwa upande wangu namshukuru Mungu.
Kwanza kabisa ni-declare interest kwamba mimi ni wa mkoa wa Mara,wilaya ya Serengeti,tarafa ya Ngoreme,kata ya Kenyamonta.

Nina machache leo ya kuzungumza na wana-Mara wenzangu kuhusu mkoa wetu.

Mkoa wa mara ulikuwa na kasifa hivi hasa kalikoletwa na mwl nyerere,kwamba baba wa taifa kutoka mara.Zaidi ya hapo tunabaki na sifa za kijinga tu ambazo kimsingi haziujengi mkoa wetu bali kuudidimiza na sisi tunabaki kuchekelea tu huku nyumba inaungua.

Mji mkuu wa mkoa wa Mara ni Musoma mjini,mtakubaliana nami kuwa mji ule umekuwa kama mtoto aliyesumbuliwa na kwashiakoo kwa muda mrefu,yaani umedumaa,hauna mabadiliko chanya tangu nianze kuwa na ufahamu,bali unakuwa kwa kwenda nyuma.

Wilaya ya Serengeti na Taarime zimekuwa zikisifika kwa fujo na watu wake eti kuitwa majasiri,hizo ni sifa za kijinga na wanaotuita hivyo wanafanya makusudi kutudumaza kimaendeleo.

Wilaya ya Serengeti,Musoma vijijini,na Bunda zinaelekea kugeuka jangwa.Wachoma mikaa wamefyeka kupita kiasi,huku watendaji wa serikali wakiwepo tu.Hawana uchungu maana wengi wao ni wa kupita tu,sisi wakudumu ndo tumeamua kujitengenezea jangwa.

Ujasiri wetu uko wapi kama si ujinga,tuna sehemu kubwa ya ziwa victoria,samaki wanavuliwa,minofu inatolewa,kisha watu wetu wanakula mifupa(mapanki),huo ndio ujasiri.

Mbuga ya Serengeti kwa asilimia kubwa ipo mkoani Mara,lakini kupata nyama kama kitoweo kwa siku hizi kupitia mbuga ni dhambi ambayo adhabu yake ni kupigwa risasi hadi kufa
.Kama mtakumbuka zamani kulikuwa na kipindi fulani kwa mwaka wanaruhusu wananchi kuwinda kwa ajiri ya kitoweo.Hakukua na tatizo,wala hatujawahi kusikia wanyama wamepungua,ilikuwa ecosystem ya kawaida kwani sisi ni sehemu ya mbuga.Mfumo umefutwa,mbuga sasa iko na VIP,ukitaka kutangulia mbele ya haki katiza mbugani.Tumebaki kuangalia tu,wamefika mahali twiga wanabebwa na kupelekwa nje,eti mkoa wa Mara ni majasiri,sifa za kijinga.

Madini ya dhahabu yapo kwa wingi mkoani Mara,kuna Nyamongo,Buhemba,Park Nyigoti,Majimoto japo kwa uchache.Tunafaidije kama si kusaidia mkoa wa Mara kuwa na takwimu ya juu kwa virusi vya ukimwi na ukimwi(7.8%)
Eti mkoa wa Mara ni majasiri,sifa za kijinga.

Mkoa umekosa chuo cha maana cha utalii na Hotel management,vipo vya hovyo tu.Vyuo vya maana vipo Arusha na hivyo waajiriwa wengi wa hotel za mbugani wanatoka Arusha,Mara tunabaki kulalamika tu.Eti sisi ni majasiri,sifa za kijinga hizi.

Rais analazimisha kupitisha barabara ya lami mbugani kwa maslahi yake binafsi
(Kwa sababu ana hotel mbugani),watu wa mkoa wa mara tumenyamaza tu,wakati tunafahamu madhara yake.Eti majasiri,ujinga huu.

Mbuga ipo kwetu,ukipita barabara ya mbugani unalazimika kulipa ada ya kupita mbugani,kama vile wewe ni mtalii.Huu ni uhuni tunafanyiwa,udau wetu juu ya hii mbuga upo wapi.Kwanini ulazimishwe kukatwa pesa hiyo wakati hukuwa na mpango wa utalii.Eti Mara majasiri.

Tukiendelea kubweteka na sifa hizi za kijinga kuna wakati utafika Mara itatambulishwa kama sehemu ya Arusha,"AMINI NAWAAMBIENI"

Waliotufikisha hapa wanajulikana,imefika wakati Mkoa wa Mara kuanzisha muungano wa vijana wa MKOA.Vijana wa Mara wakiwa na sauti moja,wanaweza kupanga vipaumbele vya mkoa,na mwanasiasa yeyote atakaetaka ridhaa yetu aonyeshe nia ya dhati kabisa ya kushughulikia vipaumbele hivyo.Vijana tunaweza kufanya hivyo,lakini pia umefika wakati wa sisi vijana kuufanyia kitu mkoa wetu pamoja na taifa kwa ujumla.

Nilikuwa naongea na mmoja wa wabunge wa mkoa wa Mara eti anasema mkoa umedhorota kwa sababu vijana wake wengi ni walevi,so what?ana maanisha hakuna mabadiliko?kwanini aliomba uongozi.

Naomba tupeane maoni juu ya mkoa wetu,tukosoane kwa kujenga na ikiwezekana tuje na harakati mpya za kuujenga mkoa wetu.

Mods kama kuna madainayoendana na hii ilishatolewa naomba msii-combine,nataka kupata maoni ya wadau
.

Hapo kwenye red, inanishangaza sana kwani yule mzungu "PAUL" akija na timu yake wanaua wanyama ovyo mamia kwa mamia, wanaondoka na ngozi na vichwa tu. Sisi wakazi wa hapo tukigusa hata sungura unapigwa risasi. Jamaa hawa wana hela sana hata mkuu wa nchi analijua hili. Hoteli yao ndiyo imeshika namba moja kwa ubora duniani.

hapo kwenye nyeusi, ile hoteli ni kweli ni ya mkuu wa kaya inaitwa BILILA
 
Akohi nimekupata vema,ni kweli nina draft ya katiba hapa,nita-share na kila anaetaka.Kuendelea kuzungumza huku tumejificha nyuma ya keybord ni dalili za kushindwa hata kuliko wazazi wetu.Namba zako nimeziona,nitakutafuta baadae kidogo.Nafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu ili katiba ipate usajiri,nitaitangaza ili kuungwa mkono,na hapo tutafahamiana sana tu.Mara ni yetu, tuna rasilimali za kutosha,tunahitaji kuijenga.

0687315600, mkuu tutafutane tuijenge Mara yetu
 
Ni matumaini yangu kuwa mpo salama,kwa upande wangu namshukuru Mungu.
Kwanza kabisa ni-declare interest kwamba mimi ni wa mkoa wa Mara,wilaya ya Serengeti,tarafa ya Ngoreme,kata ya Kenyamonta.

Nina machache leo ya kuzungumza na wana-Mara wenzangu kuhusu mkoa wetu.

Mkoa wa mara ulikuwa na kasifa hivi hasa kalikoletwa na mwl nyerere,kwamba baba wa taifa kutoka mara.Zaidi ya hapo tunabaki na sifa za kijinga tu ambazo kimsingi haziujengi mkoa wetu bali kuudidimiza na sisi tunabaki kuchekelea tu huku nyumba inaungua.

Mji mkuu wa mkoa wa Mara ni Musoma mjini,mtakubaliana nami kuwa mji ule umekuwa kama mtoto aliyesumbuliwa na kwashiakoo kwa muda mrefu,yaani umedumaa,hauna mabadiliko chanya tangu nianze kuwa na ufahamu,bali unakuwa kwa kwenda nyuma.

Wilaya ya Serengeti na Taarime zimekuwa zikisifika kwa fujo na watu wake eti kuitwa majasiri,hizo ni sifa za kijinga na wanaotuita hivyo wanafanya makusudi kutudumaza kimaendeleo.

Wilaya ya Serengeti,Musoma vijijini,na Bunda zinaelekea kugeuka jangwa.Wachoma mikaa wamefyeka kupita kiasi,huku watendaji wa serikali wakiwepo tu.Hawana uchungu maana wengi wao ni wa kupita tu,sisi wakudumu ndo tumeamua kujitengenezea jangwa.

Ujasiri wetu uko wapi kama si ujinga,tuna sehemu kubwa ya ziwa victoria,samaki wanavuliwa,minofu inatolewa,kisha watu wetu wanakula mifupa(mapanki),huo ndio ujasiri.

Mbuga ya Serengeti kwa asilimia kubwa ipo mkoani Mara,lakini kupata nyama kama kitoweo kwa siku hizi kupitia mbuga ni dhambi ambayo adhabu yake ni kupigwa risasi hadi kufa.Kama mtakumbuka zamani kulikuwa na kipindi fulani kwa mwaka wanaruhusu wananchi kuwinda kwa ajiri ya kitoweo.Hakukua na tatizo,wala hatujawahi kusikia wanyama wamepungua,ilikuwa ecosystem ya kawaida kwani sisi ni sehemu ya mbuga.Mfumo umefutwa,mbuga sasa iko na VIP,ukitaka kutangulia mbele ya haki katiza mbugani.Tumebaki kuangalia tu,wamefika mahali twiga wanabebwa na kupelekwa nje,eti mkoa wa Mara ni majasiri,sifa za kijinga.

Madini ya dhahabu yapo kwa wingi mkoani Mara,kuna Nyamongo,Buhemba,Park Nyigoti,Majimoto japo kwa uchache.Tunafaidije kama si kusaidia mkoa wa Mara kuwa na takwimu ya juu kwa virusi vya ukimwi na ukimwi(7.8%)
Eti mkoa wa Mara ni majasiri,sifa za kijinga.

Mkoa umekosa chuo cha maana cha utalii na Hotel management,vipo vya hovyo tu.Vyuo vya maana vipo Arusha na hivyo waajiriwa wengi wa hotel za mbugani wanatoka Arusha,Mara tunabaki kulalamika tu.Eti sisi ni majasiri,sifa za kijinga hizi.

Rais analazimisha kupitisha barabara ya lami mbugani kwa maslahi yake binafsi(Kwa sababu ana hotel mbugani),watu wa mkoa wa mara tumenyamaza tu,wakati tunafahamu madhara yake.Eti majasiri,ujinga huu.

Mbuga ipo kwetu,ukipita barabara ya mbugani unalazimika kulipa ada ya kupita mbugani,kama vile wewe ni mtalii.Huu ni uhuni tunafanyiwa,udau wetu juu ya hii mbuga upo wapi.Kwanini ulazimishwe kukatwa pesa hiyo wakati hukuwa na mpango wa utalii.Eti Mara majasiri.

Tukiendelea kubweteka na sifa hizi za kijinga kuna wakati utafika Mara itatambulishwa kama sehemu ya Arusha,"AMINI NAWAAMBIENI"

Waliotufikisha hapa wanajulikana,imefika wakati Mkoa wa Mara kuanzisha muungano wa vijana wa MKOA.Vijana wa Mara wakiwa na sauti moja,wanaweza kupanga vipaumbele vya mkoa,na mwanasiasa yeyote atakaetaka ridhaa yetu aonyeshe nia ya dhati kabisa ya kushughulikia vipaumbele hivyo.Vijana tunaweza kufanya hivyo,lakini pia umefika wakati wa sisi vijana kuufanyia kitu mkoa wetu pamoja na taifa kwa ujumla.

Nilikuwa naongea na mmoja wa wabunge wa mkoa wa Mara eti anasema mkoa umedhorota kwa sababu vijana wake wengi ni walevi,so what?ana maanisha hakuna mabadiliko?kwanini aliomba uongozi.

Naomba tupeane maoni juu ya mkoa wetu,tukosoane kwa kujenga na ikiwezekana tuje na harakati mpya za kuujenga mkoa wetu.

Mods kama kuna madainayoendana na hii ilishatolewa naomba msii-combine,nataka kupata maoni ya wadau
.

Pole ndugu yangu Saganka haya mambo yatawezekana tu kwa kuunda serikali za majimbo mie nikiteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara nitakuwa na uchungu gani na huo mkoa iwapo kwetu ni Dodoma? Pili iwapo nitakuwa nimetoka Dodoma ambapko hakuna miti kwa wingi kama Mara nikifika Mara sintakuwa na uwezo wa kujua kama Mara ilikuwa na misitu mingi kabla sijawa mkuu wa mkoa wa mara mie nitaona tayari ina misitu kwa kulinganisha na nilikotoka yaani Dodoma kumbe ni tofauti iwapo Mwita Maranya au Chacha Wankuru Mwita angekuwa ni gavana wa Mara maana yeye anajua historia ya Mara atalingamisha Mara ya sasa na ya miaka ya 80 na kujua kwa sasa Jangwa linanyemelea Mara kwa kifupi anapakulingalisha na alipokuwa anakua lakini mie niliyetoka Dodoma sina pa kulinganisha, sina uchungu na Mara na pia naweza uza ardhi kwa wageni na kutajirika haraka kwa kujenga kwetu wala msijue maana hakuna ajuaye nitokako tofauti na Mwita Maranya au Chacha Wankuru Mwita akitajirika ghafla mtahoji maana mnajua historia yake na wazazi wake na alipokulia.
 
Viongozi wanaotoka ni wabinafsi hivyo wanajijali wao na kuwaacha wana Mara hohehahe. But tutalalamika mpaka lini we need to woke up and move. Ni leo sio keshona tuachane na siasa
 
Ndugu yangu hawa vijana wa mkoa huu na VIMORO HASA WALIOKO PEMBENI MWA HIFADHI NI VIGUMU SANA KUSAHAU HICHO " IBING'ARA, ANYAMA ORI " Ha ha ha ha ha ha very great power is needed to change them ila tutie nguvu ili tuwatoe kwenye fikra hzo maana ni watanzania wenzetu.

Mm nimekulia huko na kusoma primary na o level huko yaan tulifaulu wengi tu wakati wa kuhitimu elimu ya msingi ila tuliojiunga sec ni kiduchu na hasa wa kutoka mikoa mingine,wengi wao walisema kusomesha mtoto 4 yrs n kupoteza muda wa uzalishaji mali na watoto wao nao walikuwa wanashabikia tu wanashabikia hilo hadi namaliza chuo kikuu pale mliman kulikuwa na vijana kama 4 niliowafahamu kutoka serengeti hii ni aibu AMKEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEENI SASA TUTAWAUNGA MKONO SISI WAKUJA HUKO.
 
Mgawanyiko upo hata ndani ya vijana wenyewe; pale chuo kikuu cha mlimani (UDSM) nakumbuka kulikua na vyama vitatu vya mkoa wa Mara: kimoja kinajumuisha makabila yote yanahusiana na jamii ya wakurya, kingine makabila yanayohusiana na jamii ya wajita, na kingine kabila la wajaluo! Ukiangalia hata chaguzi zote Musoma mjini nasikia kampeni huwa zinaendana na makundi hayo matatu ya kikabila.
Ingawa ni kweli kuna umuhimu wa kuangalia maendeleo ya mkoa na kuachana na mambo ya migawanyiko iliyoko isiyokua na maana yoyote.
 
Nilikuwa Mugumu, sasa hivi watu wa mikoa mingine ndio wanakuja kuwekeza ili kutumia opportunities zilizopo na wenyeji wamekalia kubaguana, majungu na fitina miongoni mwao.
 
Mgawanyiko upo hata ndani ya vijana wenyewe; pale chuo kikuu cha mlimani (UDSM) nakumbuka kulikua na vyama vitatu vya mkoa wa Mara: kimoja kinajumuisha makabila yote yanahusiana na jamii ya wakurya, kingine makabila yanayohusiana na jamii ya wajita, na kingine kabila la wajaluo! Ukiangalia hata chaguzi zote Musoma mjini nasikia kampeni huwa zinaendana na makundi hayo matatu ya kikabila.
Ingawa ni kweli kuna umuhimu wa kuangalia maendeleo ya mkoa na kuachana na mambo ya migawanyiko iliyoko isiyokua na maana yoyote.

Sio wajita tu,hata ukifika serengeti utakuta kura zinapigwa kiukabila.Kuna haya makabila yanayojiona giants(Wakurya na Wangoreme),wanawaacha waikoma,wanata na waisenye kuwa watu wa kuunga mkono tu upande mojawapo.Tuondoke katika fikra hizo,maana tumekuwa tukikosa viongozi wa maana kwa ushabiki tu.Kuna bwana mmoja ni Mwisenye,anaitwa Daniel Mhochi,ni mtu wa maono kweli,lakini amesaka ubunge tangu mwaka 90 hadi 2010 hakupata kutokana na yeye kutoka katika kabila lenye watu wachache.Hayo ndo baadhi ya mambo ya kuondokana nayo.Najua itachukua muda,lakini tunaweza.
 
Mimi pia mjita, jamaa amekariri sifa za kijinga mara nyingi hadi post limepoteza ladha, halafu hana solution hata moja yeye ni wa kulalama tu, wacha niende jukwaa la mahusiano........

Nakutakia kila la heri katika jukwaa la mahusiano.Lakini ingekuwa vema kama ungepata muda wa kusoma na kuelewa.Lakini pia kujua tatizo ni hatua nzuri sana.Zaidi ya yote nimesema kuwa tayari nina draft ya katiba ya Muungano wa Vijana,ni hatua nzuri kwangu mimi.Hata hivyo kukosoa ni sehemu ya maendeleo.
 
Ndugu yangu hawa vijana wa mkoa huu na VIMORO HASA WALIOKO PEMBENI MWA HIFADHI NI VIGUMU SANA KUSAHAU HICHO " IBING'ARA, ANYAMA ORI " Ha ha ha ha ha ha very great power is needed to change them ila tutie nguvu ili tuwatoe kwenye fikra hzo maana ni watanzania wenzetu.

Mm nimekulia huko na kusoma primary na o level huko yaan tulifaulu wengi tu wakati wa kuhitimu elimu ya msingi ila tuliojiunga sec ni kiduchu na hasa wa kutoka mikoa mingine,wengi wao walisema kusomesha mtoto 4 yrs n kupoteza muda wa uzalishaji mali na watoto wao nao walikuwa wanashabikia tu wanashabikia hilo hadi namaliza chuo kikuu pale mliman kulikuwa na vijana kama 4 niliowafahamu kutoka serengeti hii ni aibu AMKEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEENI SASA TUTAWAUNGA MKONO SISI WAKUJA HUKO.

Kwahiyo wewe unafurahia wazungu kuja kuwinda wanyama wetu kwa raha mustarehe lakini sisi wenyeji ambao tumekulia mazingira hayo miaka na miaka tunanyanyaswa tusiguse nyama pori kabisa.

Siku za nyuma kulikuwa na msimu wa uwindaji, mara moja kwa mwaka, ambapo uliwekwa utaratibu wa kutoa vibali vya uwindaji kwa wananchi. Hapo ndipo wananchi wanaoishi kuizunguka mbuga ya serengeti walipata nafasi ya kuuziwa nyama pori kutoka kwa wawindaji walioruhusiwa kufanya biashara ya uwindaji wa nyama pori. Kwa sisi tuliozaliwa na kukulia Serengeti huwezi kututenga kitu kinachoitwa nyama pori, iwe mbichi ama iliyokaushwa. Hilo halikuhitaji kuwa na degree kulitambua, ni common sense tu.

Kwamba hushangai wamasai kuachwa kuendelea kuishi ndani ya ngorongoro lakini unashangaa wakurya na waikoma kula kimoro/king'ara? Kuna vitu vingine unapovifanya ambavyo vina athari ya moja kwa moja na maisha ya watu lazima uwape kitu mbadala, si suala la kukurupuka tu na kuweka sheria ambazo zinawakandamiza natives na kuwanufaisha wageni, na hili ni tatizo la watanzania kuwapapatikia sana wageni kuliko watanzania wenzao.

Wakati mwingine mnapojaribu kutoa maoni yenu muwe na adabu, sio mnaropoka tu kama zimewafyatuka. Afterall hapa ni mjadala wa wanamara kwa ajili ya kutafuta namna ya kujikwamua na madhila tuliyonayo, sasa nyie mliopata nafasi ya kujikwamua kupitia rasilimali zetu mnatakiwa muonyeshe heshima na si madharau kwani kwa kufanya hivyo hatutahitaji tena ushauri wako katika hili, nenda tu ukajenge/ukaendeleze huko kwenu utuache na Mugumu yetu, sisi wenyewe tutaweza kuifikisha mahali tunapotaka.
 
Tata mwitongo sijajua una umri gani,lakini kama mnaweza naomba tuanzishe "MUUNGANO WA VIJANA WA MARA"Usiokuwa na itikadi yoyote kisiasa(maana siasa zimetufikisha tulipo),utakuwa na nguvu,ili vijana watumie fursa za kiuchumi zilizopo kimkoa,kitaifa na hata kimataifa kujijenga kiuchumi,kimaamuzi na kuiokoa mara yetu.Nabhamwe tole bhamura.Kwa kuanza tu nimeandaa katiba ya muungano huo,imebaki kufany reg.na kuiweka hadharani tayari kwa kuomba kuungwa mkono na vijana wa Mkoa wa Mara.
safi sana mkuu, inapendeza kuongea kwa vitendo, tunasubiri mwaliko wako ili tuweze kuchangia japo mawazo ni kweli kile ki-mkoa kimekaa vibaya kidogo na ni jukumu letu kuweka mambo sawa, wana siasa wamekuwepo siku zote na kamwe hawana nia ya kufanya chochote pale zaidi ya kuomba kura kila baada ya muda
 
Kwahiyo wewe unafurahia wazungu kuja kuwinda wanyama wetu kwa raha mustarehe lakini sisi wenyeji ambao tumekulia mazingira hayo miaka na miaka tunanyanyaswa tusiguse nyama pori kabisa.

Siku za nyuma kulikuwa na msimu wa uwindaji, mara moja kwa mwaka, ambapo uliwekwa utaratibu wa kutoa vibali vya uwindaji kwa wananchi. Hapo ndipo wananchi wanaoishi kuizunguka mbuga ya serengeti walipata nafasi ya kuuziwa nyama pori kutoka kwa wawindaji walioruhusiwa kufanya biashara ya uwindaji wa nyama pori.

Kwamba hushangai wamasai kuachwa kuendelea kuishi ndani ya ngorongoro lakini unashangaa wakurya na waikoma kula kimro/king'ara? Kuna vitu vingine unapovifanya ambavyo vina athari ya moja kwa moja na maisha ya watu lazima uwape kitu mbadala, si suala la kukurupuka tu na kuweka sheria ambazo zinawakandamiza natives na kuwanufaisha wageni, na hili ni tatizo la watanzania kuwapapatikia sana wageni kuliko wasawahili wenzao.

Wakati mwingine mnapojaribu kutoa maoni yenu muwe na adabu, sio mnaropoka tu kama zimewafyatuka. Afterall hapa ni mjadala wa wanamara kwa ajili ya kutafuta namna ya kujikwamua na madhila tuliyonayo, sasa nyie mliopata nafasi ya kujikwamua kupitia rasilimali zenu mnatakiwa muonyeshe heshima na si madharau kwani kwa kufanya hivyo hatutahitaji tena ushauri wako katika hili, nenda tu ukajenge/ukaendeleze kwenu utuache na Mugumu yetu sisi wenyewe tutaweza kuifikisha mahali tunapotaka.
Mara itajengwa na wana-Mara wenyewe,achana na wadandiaji.Namba zangu za simu ni 0782 577 006,tutafutane ndugu tuzungumzie harakati zetu.
 
Back
Top Bottom