Kwa watanzania wote waoishi ughaibuni

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Mara nyingi nimemsikia Rais wetu JK akisisitiza na kuwataka Wa Tanzania wanaoishi Nje ya Nchi waje kuwekeza Nyumbani, na hata anaposafiri nje ya nchi huwa anawaambia Wa Tz walio nje ya nchi waje kuwekeza Nyumbani...Ninanukuu kauli yake:"Nakuombeni sana msisahau nyumbani, mje kuwekeza... na mkumbuke nyumbani ni nyumbani...."

Sasa Swali langu ni kuwa hivi hawa Wa TZ walio nje ya nchi wana fedha nyingi sana?

Na swali la Pili Kwa WA TZ mlio nje ya Nchi, mnauitikiaje wito wa Rais wetu kipenzi cha wengi.....
 
Jambo hilo ni la kutizamwa kwa tahadhari kubwa sana. Kama walimnyima Mengi hoteli ya Kilimanjaro kwa kukumbatia watu wenye asili ya weupe ndio unafikiri kweli wanamaanisha wanachosema?

Sasa hivi tunasikia watuhumiwa wawili wa ufisadi waligombania tenda ya zana za kilima na alielamba dume ni yule wa makampuni mengi zaidi yaliyokwapua pesa za EPA.

Mnafikiri watu kama kina Iddi Simba hawana uwezo wa ku-tender? Ni ka mchezo kale kale ka serikali cha ku-tith.
 
Kwani kuwekeza mpaka uwe na mamilioni ya pesa? Ukijenga nyumba yako mwenyewe ni kuwekeza. Ukiinunua shamba ni kuwekeza. ukianzisha biashara yako ni kuwekeza. Siyo kila kitu mpaka upate msaada wa serikali. Entrepreneurship ni kuwa na wazo, ukabuni mradi, ukatafuta mtaji wa kuupa mradi uhai na halafu ukautekeleza. Msitafute visingizio kama mnayo pesa njoo muwekeze kwa kadri ya uwezo na taaluma zenu.
 
"............mnauitikiaje wito wa Rais wetu kipenzi cha wengi....."

Hapa tu ndo ulipoharibu swali lako.!
 
TUANZE KUWEKEZA KWANZA SISI TULIOPO NDANI. kWANINI KUWAITA WA NJE WAKATI WA NDANI WENYEWE HATUWAPI FURSA IPASAVYO?
 
Aisee mlioko ughaibuni kazeni kamba hukuhuko mlipo..Hawa wanawadanganyeni tu, mkirudi ndio wa kwanza kuwakirihi na kukuekeeni viunzi, halafu wakishafanikiwa kuwaharibia wanawatangeni ETI MLIKUWA MNAJIFANYA WAJANJA MMEFULIA. Njooni bongo mkizeeka kuja kula pensheni. Mkijitusu kuja kichwakichwa huku kwenye vumbi na mafuriko yanayokuja at will, MMEUMIA.
 
Mara nyingi nimemsikia Rais wetu JK akisisitiza na kuwataka Wa Tanzania wanaoishi Nje ya Nchi waje kuwekeza Nyumbani, na hata anaposafiri nje ya nchi huwa anawaambia Wa Tz walio nje ya nchi waje kuwekeza Nyumbani...Ninanukuu kauli yake:"Nakuombeni sana msisahau nyumbani, mje kuwekeza... na mkumbuke nyumbani ni nyumbani...."

Sasa Swali langu ni kuwa hivi hawa Wa TZ walio nje ya nchi wana fedha nyingi sana?

Na swali la Pili Kwa WA TZ mlio nje ya Nchi, mnauitikiaje wito wa Rais wetu kipenzi cha wengi.....

Kumbe ni kipenzi cha wengi??
haya Watanzania mnakaribishwa kuwekeza
 
Aisee mlioko ughaibuni kazeni kamba hukuhuko mlipo..Hawa wanawadanganyeni tu, mkirudi ndio wa kwanza kuwakirihi na kukuekeeni viunzi, halafu wakishafanikiwa kuwaharibia wanawatangeni ETI MLIKUWA MNAJIFANYA WAJANJA MMEFULIA. Njooni bongo mkizeeka kuja kula pensheni. Mkijitusu kuja kichwakichwa huku kwenye vumbi na mafuriko yanayokuja at will, MMEUMIA.

Hongera kwa kusema kweli. Ni kweli nyumbani ni nyumbani na wengi wangependa kurudi lakini kwa sasa hakulipi kabisa kurudi nyumbani maana ni kujitafutia frustration tu za kimaisha. Na wwngi waliokuwa na nia ya kurudi machaele yamewacheza. Eti mchumia juani mje kulia kivulini!!!! Sasa sijui kama nchi yetu imefikia mahala inastahili kuitwa ni kivuli. Angalia ile mvua ya juzi dar mabwawa na tope kila mahali!!! kutokana na poor drainage system na wakuu wa nchi au wa mkoa kimya bila hata kutia neno. Bora muendelee kuchumia juani na kulia huko huko juani huku hakuna kivuli hata kidogo jua ni mtindo mmoja kuliko hata la huko.
 
Utashangaa mafuriko ndani ya City Centre of the most commercialized city of the beloved bongoland..Hapo ndo utakapogundua kuwa hakuna serikali..ni kikundi cha watu wachache wasio na chembe ya awareness wala kujali. Miaka ya majuzikati hapa wali-procure huduma za wachina wawajengee hayo machemba na mamitaro, but with TO ZERO RESULTS & EFFICIENCY..jamaa wamekamata fuba halafu haoo wanarudi kujenga majiji yao kaa Chongqing et al sisi wanatuachia kajiji ketu kasiko na shepu wala umbo. We are so pathetic.
 
Back
Top Bottom