Kwa wataalam wa hisabati tu

hoyce

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,117
297
Nimesikia hapa JF hakuna wataalamu wa hisabati, kama wapo kwa hili watachanganyana vichwa, watueleze kwanini inakuwa hivi:

Zidisha 259 x umri wako ( tuite A ) x 39 = ( A A A )

Jibu utakalopata ni namba tatu zinazofanana, kila moja ikitaja umri wako bila kukosea.

Haya leta mameno ila msiniulize source
 
Nimesikia hapa JF hakuna wataalamu wa hisabati, kama wapo kwa hili watachanganyana vichwa, watueleze kwanini inakuwa hivi:

Zidisha 259 x umri wako ( tuite A ) = ( A A A )

kwa mtu mwenye miaka 21 inakuwaje
katika hali ya kawaida 259*21=5439

tuifanye miaka 21 ni A
nauliza je jibu litakuwa 212121 (AAA) au 21*21*21 =9261
lipi ni jibu la kutegemea kati ya hayo hapo juu naomba kusaidiwa ili nasi tujifunze hesabu.
 
Huyu bwana kakosea maelezo kidogo tu,ni kwamba jibu linalopatikana,kwa mfano 259*21=5439,then 5+4+3+9=21,sio kila namba inataja umri wako,ni lazima ujumlishe namba moja moja kati ya zile zinazounda jibu lako!
 
Ahsante kwa kumsaidia kufafanua. Manake dah!
 
Huyu bwana kakosea maelezo kidogo tu,ni kwamba jibu linalopatikana,kwa mfano 259*21=5439,then 5+4+3+9=21,sio kila namba inataja umri wako,ni lazima ujumlishe namba moja moja kati ya zile zinazounda jibu lako!

Chukulia mimi nina mwaka mmoja yaani 1. Sasa 259*1=259. Je ni sawa na 2+5+9=? Mbona haileti maana bado?
 
atakuwa kakurupuka na kanamba kake kamoja kalikokubali halafu anageneralize! maths is not about mkurupuko.

mfano miaka 28; 28x259 = 7252
sasa 7+2+5+2=16
 
kwa kawaida hisabu(Numerology) zimegawika mafungu aina tatu.
1-Abracadabra
2-Chaldean
3-.........
Hiyo ulio tumia ni ipi usaidiwe...!
 
Nimesikia hapa JF hakuna wataalamu wa hisabati, kama wapo kwa hili watachanganyana vichwa, watueleze kwanini inakuwa hivi:

Zidisha 259 x umri wako ( tuite A ) = ( A A A )

Jibu utakalopata ni namba tatu zinazofanana, kila moja ikitaja umri wako bila kukosea.

Haya leta mameno ila msiniulize source

HUYU SIKUMUELEWA VIZURI LABDA AFAFANUE TENA

ILA HUYU WA CHINI NDO KAINGIA CHAKA KABISA

Huyu bwana kakosea maelezo kidogo tu,ni kwamba jibu linalopatikana,kwa mfano 259*21=5439,then 5+4+3+9=21,sio kila namba inataja umri wako,ni lazima ujumlishe namba moja moja kati ya zile zinazounda jibu lako!
 
HUYU SIKUMUELEWA VIZURI LABDA AFAFANUE TENA

ILA HUYU WA CHINI NDO KAINGIA CHAKA KABISA

Huyu bwana kakosea maelezo kidogo tu,ni kwamba jibu linalopatikana,kwa mfano 259*21=5439,then 5+4+3+9=21,sio kila namba inataja umri wako,ni lazima ujumlishe namba moja moja kati ya zile zinazounda jibu lako!

mkuu tunahitaji kuelimishwa hasa kwa wale wenye miaka ifuatayo
1
2
3
4
5
6
7
8
10
100
na umri wa babu wa singida mwenye umri wa miaka 134 kwasababu ni sehem ya jamii yetu tungependa nae hiyo kanuni imhusu.
 
Nafikiri mtoa mada alimaanisha (259) x (umri wako) x (39) = (umri wako) (umri wako) (umri wako)

Hii ni kwasababu (259) x (39) = 10101
Sasa ukijumlisha zao la mamoja, mamia na makumi elfu na umri unapata hizo namba zinazo fanana

1 x (umri wako) + 100 x (umri wako) + 10000 x (umri wako) = (umri wako) (umri wako) (umri wako)
 
kwa mtu mwenye miaka 21 inakuwaje
katika hali ya kawaida 259*21=5439

tuifanye miaka 21 ni A
nauliza je jibu litakuwa 212121 (AAA) au 21*21*21 =9261
lipi ni jibu la kutegemea kati ya hayo hapo juu naomba kusaidiwa ili nasi tujifunze hesabu.
ni 212121
 
SAMAHANI SANA: kwenye post niliacha namba moja.

Usahihi: zidisha 259 x umri wako x 39

.
 
Nafikiri mtoa mada alimaanisha (259) x (umri wako) x (39) = (umri wako) (umri wako) (umri wako)

Hii ni kwasababu (259) x (39) = 10101
Sasa ukijumlisha zao la mamoja, mamia na makumi elfu na umri unapata hizo namba zinazo fanana

1 x (umri wako) + 100 x (umri wako) + 10000 x (umri wako) = (umri wako) (umri wako) (umri wako)

Sahihi kabisa mtu wangu, nilikosea
 
Back
Top Bottom