Kwa wasomaji wa Riwaya na hadithi, Someni hii!

Nimerejea baada ya kumaliza kuisoma. Kazi nzuri sana. Endelea kuandika mara kwa mara ili ukinoe kipaji chako. Kumbuka pia kusoma sana kazi za watu wengine ili hatimaye uwe mwandishi bora kabisa.
 
Habari, nimetunga riwaya ambayo nategemea nitapata maoni yenu kwani iko mbioni kuchapishwa. Na hapa nimeona niwawekeeni kitabu hicho na nitarudi kupata maoni yenu baada ya kukisoma. Nategemea sana maoni na ushauri wenu wana JF wote ambao ni wapenzi na washabiki wa Riwaya. KARIBUNI. View attachment 54349

Tayari nshasoma kitabu chote.
Pengine ulitaraji nifanye uchambuzi wa fani na maudhui yake hadi kufikia hatua ya kutoa 'hukumu' kwa kusema udhaifu wa mwandishi ni moja, mbili, tatu.. Lakini niseme kuwa hilo sitalifanya, na badala yake nakupa maoni ya jumla tu. Umeonesha umahiri katika kujenga taharuki na kumfanya msomaji avutike kuendelea kusoma; hilo ni jambo jema ambalo riwaya nzima imetawaliwa kwalo. Lakini nimepata mashaka kidogo juu ya umakini wa Bonge kukubali kudanganyika kwa urahisi vile kubadilishiwa begi na asigundue haraka. Kumbuka umesema kwamba begi hili limenunuliwa tu dukani na kupelekwa moja kwa moja bila kushughulika na kuliwianisha uzito, sura ya uchakavu... almradi kujenga mazingira ya kulifananisha na begi halisi. Hilo halionekani na linajenga mashaka kwenye uumbaji wa wahusika ambao wanapaswa kuonesha umahiri kuuvaa uhusika wao. Liko jambo moja la kukosekana muwala wa matukio fulani fulani. Mathalani riwaya haijabainisha kifo cha Chausiku au Merina kinavyohusiana na mlolongo wa matukio mengine. Labda iwe ni kwa lengo la kuacha mwaya wa kuendeleza riwaya siku za mbeleni, lakini 'mzigo' kutofunguliwa licha ya tangu mwanzo kuonesha kwamba ungefunguliwa hata kama hilo lingemaanisha kifo linaancha maswali mengi kuliko majibu. Msomaji pengine anaweza kutabiri (yaweza kuwa kwa makosa...!) kwamba ndani ya begi kulikuwemo ngozi ya binadamu, viungo vya albino hasa kutokana na mdokezo mahala fulani kwamba pana harusu ya uozo 'ilisikika' kutoka kwenye mzigo. Mhusika Bonge alipata kujitambulisha mahala fulani kuwa ni afisa wa Polisi. Pengine lilikuwa jambo lenye afya zaidi ikiwa ukweli juu ya hili ungabainishwa ili kwamba jamii ipate funzo. Kwamba pana watu matapeli hujisingizia kwamba wao ni watu fulani kumbe sio; au watu fulani tuliowapa dhamana fulani fulani kwenye jamii wanaonesha tabia iliyo ghalati kabisa na viapo vyao. Pengine nikushauri kwamba una nafasi kubwa ya kuireusha zaidi riwaya hii na kuifanya kuwa ndefu kwa kuziba mainya ile iliyomo kwenye msuko wa matukio. Ujue mathalani vifo vyote vilivyotokea hatujaona 'urefu' wa mkono wa dola na msomaji anaweza kuamini kwa makosa kwamba ni rahisi kumuua mtu na bado usitiwe hatiani kwa kuwa tu utatoroka kutoka Dar es Salaam kwenda Musoma.

Natua hapa kwa leo, naamini tutaendela kubadilishana tajriba.
 
Ndugu mmoja alisema 'Watanzania ni wavivu' nikamuuliza 'katika nini?' Kumbe nimegundua sehemu mojawapo ni katika kujisomea! Mbona comments nyingi kabla ya kusoma? Nani kapitia riwaya hiyo?
Nitarudi nikimaliza kusoma.

BUCHANA umetaja kwa usahihi kwamba Watanzania ni wavivu wa kusoma ingawa pana kosa moja dogo limekutoroka nasi tukaliona. Hili ni lile la kujitoa kwenye kundi la Watanzania wavivu japo tangu uahidi kurudi baada ya kusoma majuma kadhaa yamekwenda na wala hujaonekaana tena. Hao uliowalaumu wametoa 'comments' nyingi bila kuisoma riwaya kwanza, ndiyo watakuwa wa kwanza kukushangaa, bila shaka!!!
 
simulizi ni nzuri,inampa msomaji hamu ya kuendelea kusoma!
ni imani yangu kuwa unaelekea kuwa mtunzi mzuri zaidi cku za usoni..
mashaka yangu ni matukio tu ambapo moja ya tukio linalonitia shaka katika swala la umakini wa akina Martin na kundi lake..ukatili na sifa alizopewa Martin nilitegemea zingekwenda sawa na kampani aliyonayo na hili lisingepelekea kumwaga habari muhimu kwenye korido ambayo inafahamika wazi wazi kwamba chumba kimoja wapo Bwana Kajuna alikuemo, hivyo wasingepaswa kuongea siri kijingajinga tu na kirahisi kama ilivyokua..nafikiri zile habari zingemfikia Kajuna kwanamna nyengine, na sio kama vile kwani ilikua ni rahisi mno.

nionavyo mimi pia ingewekwa bayana kama kweli ulikua ni mtego Kajuna kukutana na Merina,Merina kusahau simu mpaka kufikia hatua ya kupigwa picha katika tukio la mauaji..japo Kajuna aliwaza kua huenda lilijua tego lakini mimi kama msomaji ningetegemea mwandishi angetoa maelezo hapo mbele namna chezo lilivyopangwa na lilipangwa vipi,je ilikua mtu yeyote angeweza kuwa Kajuna ilimradi tu alienda pale bar ya tabata ambapo Merina aliingia ama walimtaka Kajuna tu!
ni kazi nzuri ..big up jomba!
NIKIKUMBUKA MENGINE NITARUDI.
 
Back
Top Bottom