Kwa wasiomjua Magufuli, Je, anafaa kuwa Rais?

Status
Not open for further replies.
HAHahahahhahahahah Umeamua kupoteza muda mrefu kuweka crap! Magufuli ndiye Mwana CCM aliyebaki wengine ni magogo!

...sishangai conclusion yako, hasa ukizingatia ma-role model wako ni watekaji, wauaji, wanavisasi na wakamia madaraka km Hitler, Bush, Musolin na majenerali punguani! Do many wrongs make one right? Na Lowassa tumkubali basi, km ni uchapa kaz, au?
 
Kaka acha MAJUNGU mbona unakuwa kama mnafiki. Kwani wewe ndio msafi sana mpk uchambue viongozi kwa kukosoa mambo yasiyo ya msingi katika maendeleo?

Unapompima kiongozi muangalie kwa maendeleo aliyofanya. Magufuri is among the best minister wala hilo halina shaka, wewe kaa na majungu yako tu hayo na wala hayatakufikisha kokote. Jiheshimu mjomba!!

Duh, maneno yako makali, unaukaribu na muheshmiwa nini, mbona hutaki aguswe. Au wewe CCM? Au ww CHADEMA B? Au ww mmoja wa wahandis wanaojenga kale kagorofa pale obay? Maana jamaa katoa yake, aliyotafiti. Umpinge kwa tafiti basi ili tuhitimishe nani katafiti kutumia njia feki. Otherwise unakua na ww mbayuwayu km yeye tukitafit tukamkuta mwongo.
 
Hahahaaaaaaaa! Hivi kwani Taifa halijengwi na maeneo madogo madogo kama Biharamuro na mengineyo? Hivi kama hakuna hizi COMPONENT ndogo ndogo zinazoungana kutengeneza eneo kubwa likaitwa inter alia Taifa?Huyu Magufuli ndiye aliyewatishia wananchi wa kata ya Mganza kwamba wasipomchagua Diwani wa CC_ UMEME uliogharimu pesa nyingi kufika katika Kata hiyo hautawashwa. Lakini wananchi kwa jeuri walijibu "WAMEZOEA KUISHI BILA UMEME" hivyo hawawezi kuingiliwa katika uhuru wao wa kuchagua diwani wanaye mtaka kwa vitisho vya kutowashiwa UMEME. Hawa ndiyo viongozi wetu. Hypocrites and they are Chopping KILITANIA SMALL.
 
Asante sana mtoa mada kwa kumuweka wazi fisadi huyo magufuli mbele ya macho ya watu, mi hua nasema kila kila siku hakuna msafi hata mmoja ndani ya ccm, ila kuna mafisadi na wanafiki, wanafalsafa wanasema kua ndege wenye mabawa yanayofanana mara zote huruka pamoja, sasa iweje magufuli awe msafi kiasi hicho wakati yupo na akina rostam? Unafiki umemjaa kwa kutoa data za uongo ili apate umaarufu na kujisafishia njia, niliwahi kumsikia siku moja akitoa maelezo kuhusu idadi ya bata, kuku na mbuzi woote hadi samaki waliopo majini

mungu awalaani mafisadi woote
 
watu bana, mnarukia post tu! Hoja ni anafaa kuwa rais au lah? Ati ndo pekee kabak, so what? Inanikumbusha mfano wa jamaa angu-ati ukiwa na njaa sana SANA, na ukakuta pilau mezani, lkn katkat kuna kakinyesi, utakula pemben pemben upunguze njaa au utaacha njaa iendlee kukusigina?

...kama swala ni kutafuta aliebak CCM mchapakaz na mleta vijimaendeleo, hata EL anafaa zaidi mbona?
 
Kwani huyo Magufuli (sio Magufuri) amesema anautaka Urais? Tuanzie hapa ndio tuone hoja ya mtoa hoja kama inahitaji kujadiliwa...otherwise tusubiri
 
Thou jamaa ni mtu wa visasi lakini juhud zake zinaonekana,siamini kama kuna mtu mwenye visasi kama JK, nenda majimbo yanayoongozwa na wapinzani uone anavyowafanyia hila yeye na chama chake.
 
HAHahahahhahahahah Umeamua kupoteza muda mrefu kuweka crap! Magufuli ndiye Mwana CCM aliyebaki wengine ni magogo!

Try to think before you make your conclusion.

Wewe ulijua baya gani la JK kabla hajaboronga akiwa raisi?? Si ndio nyie mllikuwa mnamsifia wakati wa kampeni 2005 kuwa eti rais kijana sijui mchapakazi sasa yako wako?? Mh! fatilia aliyoandika Burigi uone kama hayana ukweli. Mtu anatoa kiapo kuwa wana Biharamulo Magh. watakiona kwa sababu walimnyima kula na kweli anatimiza kiapo chake lakini mijitu inaona kwamba that's no concern! Hebu tujenge utamaduni wa kuchulia mambo serious before we conclude on such matters. (kifupi heshima yangu kwako inaanza kushuka)
 
waliobakia ndani ya ccm are much worse than magufuli.
Kwa kila baya unalomwona nalo, wengine wanayo mara kumi zaidi.

Halafu mgodi uliopo biharamulo nafikiri unaitwa tulawaka, sidhani kama ni buzwagi....

mkuu mgodi ni tulawaka nimechanganya kidogo sorry kwa kukosea unajua migodi imekuwa mingi hadi unasahau kujua mwingine u wapi lakini habari ndiyo hiyo na kuhusu kuwa yeye ndiyo bora kuliko wana ccm waliobaki nakubaliana na wewe hilo sikatai kabisa lakini je hatutakiwi kujadili na mabaya yake mnataka tujadili mazuri tu
 
Kwani huyo Magufuli (sio Magufuri) amesema anautaka Urais? Tuanzie hapa ndio tuone hoja ya mtoa hoja kama inahitaji kujadiliwa...otherwise tusubiri

Mkuu sio mpaka aseme........
Binafsi siamini kama Magufuli ni mchapa kazu mzuri kiasi hicho...ila ni mzuri sana kuhahakisha ana 'coverage' nzuri ya media....ni EL type! Kifupi nadhani ni 'rafiki' wa media kuliko 'uchapakazi'.
 
Nimekuwa ni msomaji zaidi kuliko mchangiaji kwa muda mrefu lakini nimekuwa nikishangaa sana watu wanapokuwa wanaongea vitu wasivyovielewa ama kwa ushabiki au kwa kutokuelewa, mfano watu wameandika sana kuhusu uwezo wa Dr John Pombe magufuri kuwa anafaa kuwa rais wa jamhuri ya muungano watanzania kwa kutumia vigezo dhaifu sana kuwa kila anapopewa wizara hufanya vizuri nafikiri hicho si kigezo tosha kabisa cha mtu kuwa rais

Kwa wasio mjua Mh. magufuri nilitaka leo wamfahamu kwa ufupi tu kidogo ili na wao wapime kama kweli anafaa kuwa kiongozi wa nchi ktk nafasi kubwa km ya urais.

Magufuri ni mtu mwenye visasi sana na yu tayari kuumiza uma wa watu katika kulipa visasi kwa wasio mjua mh. magufuri alipata kugombea ubunge jimbo la biharamulo mara mbili bila kupita mara zote aliangushwa na kina marehemu phares Kabuye kwa kura nyingi sana ,aliweza kupata ubunge pale tu wilaya ya biharamulo ilipogawanywa majibo mawili yaani Biharamulo Magharibi na Biharamulo mashariki Hivyo akafanikiwa kuin gia bungeni kwa rushwa kubwa sana na kuwa mbunge wa Biharamulo mashariki wakati upande wa Biharamulo magharibi akiwa Mh. Choya.

Baada ya kupata ubunge Aliapa kiapo kama atahakikisha Biharamulo mashariki inakufa, kipindi hicho Magufuri alipata unaibu waziri hivyo alitumia nafasi hiyo kuivuruga Halmashauri ya Biharamulo na na kwa influence miradi yote mikubwa ya wilaya ikawa inaenda jimboni kwake moja kwa moja bila hata kupitia Halmashauri watu wote walitishwa makao makuu ya wilaya na hakuna aliyeweza kusema lolote kama manakumbuka vizuri alifikia kugombana na mbunge mwenzake wa mashariki aliyefikia kusema kama magufuri anatumia uwaziri wake kumhujumu jimboni mwake (kitendo kilicahomluudihi sana magufuri na kuhakikisha nakufanikisha Mh.Choya anadondoka ktk ubunge wa Biharamulo Magharibi. Alifikia kuwa analeta wageni wakitaifa direct jimboni kwake hata bila kupitia makao makuu ya wilaya lakini nia ikiwa ni kiapo alichokiweka kuwa lazima ataiua biharamulo Magharibi kwa kumnyima ubunge mara mbili hapa nataka kuwaonyesha kiongozi huyu mcheshi mchapa kazi lakini mwenye visasi vyenye kuleta maafa kwa wazee wanawake na watoto.

Je mtu huyu anaweza kuwa kiongozi wa umma?

Mwaka uliofuatia mheshimwa Magufuli alipita bila kupingwa baada mgombea mwingine aliyekuwa tishio kwake (jina nalihifadhi) kufanyiwa mizengwe wakati wa kurudisha form mpokea form alijificha na alijitokeza wakati mda wa kurudisha form umekwisha akaonekana mrudisha form amerudisha form too late lakini Mh. Magufuli alikuwa ameisha watisha viongozi wa chama na serikali wilayani biharamulo atakaepokea form za Bwana huyo basi yeye ni naibu waziri atahakikisha hana kazi watu wakatii na wakafanya dhuruma ya kumpitisha magufuri bila kupingwa.Je mtu huyu anaweza kuwa kiongozi wa umma?

Mwaka 2005 kijana mdogo anaitwa nahifadhi jina lake kupitia chama cha CUF ambaye alikuwa katibu wa wilaya wa CUF wilayani biharamulo alichukuwa form kugombea jimbo la biharamulo mashariki kwa magufuri huku akiwa na suport kubwa sana ya vijana na alikuwa anaenda kumwamgusha mh. Magufuli katika kinyanganyiro hicho, alichofanya Mh. Magufuli alimteka kijana huyo na kumpakia kwenye gari hadi mwanza kutoka mji mdogo wa Buseresere walimpelekea mke wa huyo bwana pesa wakampatia simu aongee na mme wake wakimshawishi waende hadi Mwanza wampatie pesa aondoe jina kwani pesa kidogo ya matumizi wameishamwachia mke wake yule bwana. Alipofika mwanza akapandishiwa dau hadi milioni 60 akubali kutorudisha form za ubunge ikiwa hapo imebaki siku 4 kabla form kurudishwa kijana akakabidhi form zake kwa Magufuli wakaenda nae hadi bank kijana kabaki kwenye bench mh. waziri akaingia ndani akatoka akamwambia account yake pale haina pesa waongozane hadi Dar es salaam. Wakapanda ndege hadi Dar kijana akafikishiwa kwenye 3 star hotel kwa bili ya mheshimiwa siku tatu bila kuonanana Mh. Magufuli.

Siku ya nne kijana anaona kwenye TV Magufuli amepita bila kupingwa akashtuka kaulizia hadi ofisini kwa waziri kafika akakaribishwa Mh. kama hamjui akamuuliza shida yako nini akasema nipe pesa zangu mh. akamwambia unakuja kuniomba rushwa nikuachie ubunge wewe kijana huna adabu kabisa. Mkifuatilia CUF, hiki kisa wanakijua vizuri kwani walipelekewa taarifa kama kuna mgombea wao ameenda kuuza ubunge kwa Magufuli ikabidi Green GUARD ya CUF iende kum-arrest na kumpeleka Buguruni makao makuu na kurudi Biharamulo kwa aibu kubwa lakini baadae alimtafutia kazi kwenye mgodi huko Tulawaka anafanya kazi kumziba mdomo kwa sababu kijana alikuwa ameapa kumfanyizia.

Huyu ndiye Magufuli, je anaweza kuwa kiongozi wa nchi katika uhuni wa namna hii?

Sinema ya Magufuli haiishi hapo; kile kiapo chake cha kulipa kisasi Biharamulo Magharibi kiliendelea alipolazimisha kupindisha barabara ya lami kuingia Chato toka Mwanza kwenda Bukoba kupitia Biharamulo makao makuu ya wilaya akaipindidhia Chato nyumbani kwake na kuua makao makuu ya wilaya ya Biharamulo. Huyu ndiye kiongozi anayeweza kuongoza watu?

Mh. Magufuli alipigana na kulobby kwa nguvu zote kuhakikisha Chato inakuwa wilaya ili Biharamulo Magharibi wasifaidi mapato ya ziwa ambalo yanapatikana upande wa Chato na Nyamirembe na ndiyo kilichokuwa chanzo kikuu cha mapato cha wilaya ya Biharamulo lengo ikiwa ni katika kuendelea kulipa visasi kwa nini upande wa magharibi walikuwa hawampi kura kwa mihura takribani miwili alifaulu na Chato ikawa wilaya mpya toka Biharamulo.

Alipojikuta amesahau kuwa mgodi wa Tulawaka upo Biharamulo na haupo Chato alianza kuharasi uongozi wa wilaya ya Biharamulo kuwa ule mrahaba wa mwisho wa mwaka unaotolewa na migodi kwenye halmashauri za wilaya migodi ilipo alitaka Biharamulo igawane nusu kwa nusu mrahaba wake na wilaya ya Chato. Huyu ndiye Mh. Magufuli, je rais anaweza kuwa na tabia hizi chafuchafu namna hii?

Iliposhindikana akiwa waziri wa ardhi Mh. magufuri kwa makusudi kabisa alibadilisha mawe ya mpaka kwa amri kama waziri wa ardhi kuiingiza Tulawaka ndani ya wilaya ya chato hivyo siku si nyingi chato itadai Tulawaka ipo kwao na watapola haki ya wana biharamulo swala hili lipo wazi kabisa halmashauri ya wilaya kupitia baraza la madiwani limelalamika sana kuhusu ushenzi huu wa magufuri huyu ndiyo mtu anaweza kuwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania?

Mwaka jana katika mpaka mwingine wa biharamulo na chato kijiji cha biharamulo kinachopakana na chato huko kata ya Runazi wanakijiji waligundua kuna dhahabu na kuna wachimbaji wadowadogo Mh. magufuri yupo analazimisha kubadili mipaka ili hiki kijiji kihamie wilayani chato na kumekuwa na mgogoro wa kiutawala unochochewa na yeye Huyu ndiyo Mh. Magufuli anaepigiwa debe humu ndani kama anaweza kuwa rais rais huangaliwa pande zote mafanikio na madhaifu kwangu mimi madhaifu ya magufuri ni mengi kuliko mafanikio mtakumbuka kilio cha nyumba za serikali lakini huyu jamaa mkumbuke ni bingwa wa kusimamia wakandarasi na kutaka viwango kktk ujenzi lakini yote tisa kumi mh. anajenga ghotofa pale kwake anapoishi Osterbay yeye nendeni mkaone maajabu ya mussa wajenzi mafundi mchundo hata ramani hazijapitishwa sababu wachoraji ni watu wa mitaani na mafundi ni ni vibaruwa mchundo huyu ndiyo Mh. Magufuli.

Lakini skendo kubwa ya huyu bwana ambayo waandishi wangefuatilia kumjua vizuri ni jinsi alivyochezea mipaka ya wilaya ya Biharamulo kubadilisha DN za vijiji na kusogezwa mawe yalioizinishwa na serikali bila hata serikali kujua kuzipeleka Chato hii ni hujuma kubwa na anastahili kujiuzulu waandishi nendeni mkawahoji wananchi na viongozi wa wilaya biharamulo mjue huyu mtu kitu alichofanya mtu namna hii hawezi kuwa kiongozi kabisa

Huko jimboni kwake wafanyakzi wa serikali wote walio against naye amewaumiza sana wengine hata kufunga vibiashara vyao vidogovidogo ili tu wakubaliane naye kifupi hajawahi kupita bila kupngwa ila amekuwa akipita kwa hila kubwa.

Naomba kuwakilisha ili tumpime kwa pamoja. Je, tabia hizi zinaweza kumpa urais kweli?

TUMPIME KWA PAMOJA HAYO NI MAONI YANGU TU


Kwakuwa ni mgomvi wa mipaka,siku akiwa rais,nadhani atakuwa mzuri kuilinda nchi yetu.Mipaka ya nch yetu itajikuta Entebe,Uganda,na Kisumu Kenya.
 
Sasa ni dhahiri vuguvugu la uchaguzi wa 2015 pazia linaanza kufunguliwa iweje useme eti huyu hafai kuwa rais wakati mtu mwenyewe wala hajaonyesha nia yakufanya hivyo hivi mh Magufuri ni mzito wa kufikiri na kusema mpaka wewe ndio unafikiri nakusema kwa niaba yake kweli umeonyesha udhaifu mkubwa wakuanza kampeni chafu za urais dhidi ya mtu ambaye hajatangaza kuitaji hata urais wenyewe inakubidi ufahamu watu wengine ni wachapakazi by nature wala si kwa ajili ya vyeo Pamoja na hayo nadhani watanzania tumeelevuka vyakutosha kuweza kujua yupi anafaa kuwa kiongozi hata kama siasa za majitaka zitafanywa dhidi yake Lakini kwa vyovyote vile itakvyokuwa hatutarajii kuongozwa na malaika wala shetani pamoja na sifa lukuki anazotakiwa awenazo sidhani kama atakosa mapungufu kama mimi na wewe
 
Rev. Masanilo nimekushusha thamani, we unaona Magufuli bora kweli? Ungechunguza kwanza madai haya kabla ya kuandika crap zako. JK mlisema walisema hivi hivi watu wakamng'ang'ania kiko wapi leo. Tuyapime haya kabla ya kuandika ujinga wetu tunaouona ni bora. Kwangu mimi sijaona mwema aliye CCM anayefaa kuwa rais wangu!

Usiwe unafata upepo tu! Usitake aminisha umma kuwa CCM wote hawafai! Kuna wachache walau wanaweza ! Magufuli ni mmoja wapo
 
Sisi tunamfahamu Magufulu kama kiongozi mchapa kazi asiyependa kuchanganya maneno, kwake ndiyo ni ndiyo hapana ni hapana, BASI.
Acha tabia za kidhabidhabina.
Peleka mbali majungu ya kike na wivu wa kike kama alivyosema Mzee Mkapa.Tunashida, ombwe la uongozi, tupe kiongozi anaefaa taja jina lake hapa tulijadili.ACHA KUTUMIWA NA MAFISADI.
 
Kwa maana hiyo magufuli Hana zuri hata moja ? Kikwete basi atawale milele tujue Tanzania tuna utawala wa kifalme
 
Magufuli ndiye kiongozi aliyebaki CCM.Acha kupiga majungu mkuu!
Na kwahayo ya magufuli ni tone katika ndoo ya maji!ukilinganisha na wabunge wa ccm wanayofanya,pili buzwagi ilipo mbona kijiografia iko kushoto na biharamulo na chato?yeye Magufuli huwezi ukamlinganisha na JK katika administration mimi naona ccm wana jembe!!hayo uliyoyasema ukiambiwa wengine walivyofanya kupata ubunge unaewza kusema bora yeye kapita kihalali ila hayo nimapungufu madogo ambayo hayawezi kutumika kama kigezo cha kuhukumu!!!
 
Kama kilichosemwa ni kweli basi akipata nafasi ya juu ya uongozi huyu ataua mara moja demokrasia. Hakuna mtu atakayekuwa na uwezo wa kukosoa serikali hata kama uozo gani utafanyika.
Ushauri wangu ni kwamba hakuna chema kinachoweza kutoka CCM nukta.
 
inaonekana kuwa wewe hapo umeona kitu fulani.
Nakubaliana nawe. Tunaweza kujadili mazuri na mabaya ya potential candidates. Sina tatizo na hilo. Hisia zangu kwa kuangalia "timing" ya hii post, zinanirudisha kipindi cha 2000-05 ambapo ndani ya CCM walianza taratibu kwenye magazeti mbali mbali lakini hasa RAI (akina Salva on behalf of EL and RA) kupakazia tuhuma watu wote waliokuwa wanaonekana tishio la kuweza kushindana na waliyemtaka.

Nina hofu kuwa hiki ndicho kinachoendelea kwa sasa, kuwachafua mmoja mmoja, halafu baadaye wanakuja na ambaye ataonekana mbele ya jamii kuwa hana "uchafu" au ana afadhali kidogo. Lakini ukweli ni kuwa huyo watakayeleta jina lake anaweza kuwa mchafu zaidi, uchafu ambao unakuwa umefichwa makusudi.

Kama ni kujadili, ni vizuri kuwa objective, na kuwa impartial. Yaelezwe mazuri na mabaya ya hao watu.



 
Ni muhimu kupata taarifa kama hizi kwa watu wanaofikiriwa kuwa viongozi wetu, na si vizuri kuwakatisha tamaa wanaotoa taarifa hizi na kuwapa watu fulani utakatifu wakati pengine hawana.

Nakumbuka mwaka 2005 watu walivyokuwa wamepagawa kwenye forum ya uchaguzi.com (kama JF ya leo), ulikuwa huwezi kusema neno lolote watu wakaelewa na ulikuwa unaitwa majina yote ya usaliti hapa duniani ukimkosoa mgombea wao kipenzi. Niliandika makala kuhusu sababu 15 kwa nini CCM wamteue SAL-ngumi, mateke na matusi niliyopata kutoka kwa wana uchaguzi.com siwezi kusahau, na leo ndiyo hao wanaoongoza kumpiga mawe aliyekuwa mgombea wao kipenzi.

Sasa tusirudie kosa tulilofanya mwaka 2005 kwa kuendekeza ushabiki wa kijinga na kudharau watu wanaotupatia taarifa za upande wa pili wa wale wanaotaka kuwa viongozi wetu. Huu sio muda wa ushabiki na ubazaza usio na mantiki.

Lazima kila kiongozi tumpime vya kutosha na lazima tugeuze kila jiwe.

Wengi, tunaongozwa na hisia katika kufanya maamuzi; Ushauri, Kama unaona jambo limevuta hisia zako kupita mpaka lipotezee harafu arudi badae kutoa mawazo yako. Magufuli namkubali ila nilikuwa sijui madudu haya (hasa kama yana ukweli itakuwa haijaka poa)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom