Kwa wasiomjua Magufuli, Je, anafaa kuwa Rais?

Status
Not open for further replies.
Mze kila mtu ana good na bad History hata magufuri ana mema mengi tu amefanyia taifa hili mfano ameweza kusimamia wizara mbalimbali kwa ufanisi mkubwa kulinganisha na wenzake waliopata kupita katika wizara hizo mfano ujenzi wa barabara aliweza kusimamia vizuri zaidi na hiyo ndiyo sifa tunayompamba nayo sana kwa kweli hata mimi ninampongeza lakini hata humo ukiangalia kwa ndani utagundua kuwa kuna vitu vingi alifanya ambavyo kimaadili vinamwangusha kuwa kiongozi bora na ukweli utabaki ndani ya samaki kumi walioza angalau yeye hajafikia hali mbaya anaweza kiliwa hata kwa ndimu
 
Umeongea maneno yenye hekima sana na lengo hapa siyo chuki ni vizuri watu kuwapatia taarifa wapime mzani wa mazuri na mabaya ya viongozi wet.

Kama mazuri yakizidi na watu wakaamua hakuna wasiwasi wowote lakini itakuwa mbaya kwa kuamua kuendelea kukaa kimya upenzi ushabiki hautusaidii chochote katika kujenga nchi hii hata kama mtu ni kipenzi wangu binafsi katika uongozi wa taifa lazima tumwambie kuna mhali umekosea mzee huenda alikuwa amjikwaa na akaamua kujirekebisha.
 
Acha majungu na porojo wewe. Sisi tunaangalia nini alichofanya kwa taifa na siyo nini alichofanya Biharamuro. Inawezekana wewe umetumwa na mafisadi kuanza kumchafulia Mhe. Magufuli. Waambie waliokutuma kwamba tumekung'amua.

Kwa taarifa yako, hakuna mwanadamu aliyemsafi. Kinachotazamwa hapa ni uthubutu wa kiongozi kuchukua maamuzi makubwa na magumu kwa maslahi ya umma. Kwa sifa hiyo, niambie ni nani anayeweza ndani ya baraza la mawaziri la sasa, kama siyo Mhe. Magufuli?? Ebu tuondolee porojo zako humu jamvini zisizo na mashiko.
 
Nafikiri alimaanisha TULAWAKA kwani ndio iko Biharamulo na niliwahi kusikia kuwa jamaa anataka mipaka ibanguliwe ili Tulawaka iwe Chato.
Na aliyoyaongea Burigi ni kilio cha siku nyingi cha wana Biharamulo.


Mzee nashukuru kwa ufafanuzi wako mzuri
 
Try to think before you make your conclusion.

Wewe ulijua baya gani la JK kabla hajaboronga akiwa raisi?? Si ndio nyie mllikuwa mnamsifia wakati wa kampeni 2005 kuwa eti rais kijana sijui mchapakazi sasa yako wako?? Mh! fatilia aliyoandika Burigi uone kama hayana ukweli. Mtu anatoa kiapo kuwa wana Biharamulo Magh. watakiona kwa sababu walimnyima kula na kweli anatimiza kiapo chake lakini mijitu inaona kwamba that's no concern! Hebu tujenge utamaduni wa kuchulia mambo serious before we conclude on such matters. (kifupi heshima yangu kwako inaanza kushuka)

Kuchukulia jambo seriously maana yake ni kuunga mkono hoja!! Wewe lazima utakuwa umetumwa! Kama sivyo, basi 'mtindio wa nanii..' lazima umeanza kukunyemelea.
 
Mkuu Buzwagi haipo Biharamuro, au mi nimepoteza kumbukumbu! lakini hapana nimefanya interview hapo mara mbili najua iko kahama. hayo mengine yawezekana yapo na siyo kwa Dr Magufuli ila ni mtindo wa CCM wengi niseme karibu 90% ya wabunge wanafanya hizo mbinu. Maoni yangu, CCM hawatakiwi Tanzania bara.
 
Wewe ndiyo mleta porojo hapo usizuie watu kupata taarifa acha watu wapate taarifa fanyia kazi habari hizo ndiyo useme maneno yako otherwise utakuwa hauna maana yeyote mimi sileti habari hizi kishabiki kama ulivyo nenda biharamulo kauliza haya fuatilia hayo halafu ndiyo uje unasema ni porojo mtu mwenye hekima hakurupuki asikiapo jambo hufanyia kazi jifunze hilo utaheshimika
 
Acha majungu na porojo wewe. Sisi tunaangalia nini alichofanya kwa taifa na siyo nini alichofanya Biharamuro. Inawezekana wewe umetumwa na mafisadi kuanza kumchafulia Mhe. Magufuli. Waambie waliokutuma kwamba tumekung'amua. Kwa taarifa yako, hakuna mwanadamu aliyemsafi. Kinachotazamwa hapa ni uthubutu wa kiongozi kuchukua maamuzi makubwa na magumu kwa maslahi ya umma. Kwa sifa hiyo, niambie ni nani anayeweza ndani ya baraza la mawaziri la sasa, kama siyo Mhe. Magufuli?? Ebu tuondolee porojo zako humu jamvini zisizo na mashiko.
Wewe ndiyo mleta porojo hapo usizuie watu kupata taarifa acha watu wapate taarifa fanyia kazi habari hizo ndiyo useme maneno yako otherwise utakuwa hauna maana yeyote mimi sileti habari hizi kishabiki kama ulivyo nenda biharamulo kauliza haya fuatilia hayo halafu ndiyo uje unasema ni porojo mtu mwenye hekima hakurupuki asikiapo jambo hufanyia kazi jifunze hilo utaheshimika
 
Kaka acha MAJUNGU mbona unakuwa kama mnafiki. Kwani wewe ndio msafi sana mpk uchambue viongozi kwa kukosoa mambo yasiyo ya msingi katika maendeleo?

Unapompima kiongozi muangalie kwa maendeleo aliyofanya. Magufuri is among the best minister wala hilo halina shaka, wewe kaa na majungu yako tu hayo na wala hayatakufikisha kokote. Jiheshimu mjomba!!
 
Rev. Masanilo nimekushusha thamani, we unaona Magufuli bora kweli? Ungechunguza kwanza madai haya kabla ya kuandika crap zako. JK mlisema walisema hivi hivi watu wakamng'ang'ania kiko wapi leo. Tuyapime haya kabla ya kuandika ujinga wetu tunaouona ni bora. Kwangu mimi sijaona mwema aliye CCM anayefaa kuwa rais wangu!
 
Mkuu Buzwagi haipo Biharamuro, au mi nimepoteza kumbukumbu! lakini hapana nimefanya interview hapo mara mbili najua iko kahama. hayo mengine yawezekana yapo na siyo kwa Dr Magufuli ila ni mtindo wa CCM wengi niseme karibu 90% ya wabunge wanafanya hizo mbinu. Maoni yangu, CCM hawatakiwi Tanzania bara.

Nafikiri alimaanisha TULAWAKA kwani ndio iko Biharamulo na niliwahi kusikia kuwa jamaa anataka mipaka ibanguliwe ili Tulawaka iwe Chato.
Na aliyoyaongea Burigi ni kilio cha siku nyingi cha wana Biharamulo.
 
Haya ni madai mazito sana.

Kama ni kweli jamaa amefikia hatua ya "Kukidnap" watu ili akae madarakani basi jamaa hafai.

Haijalishi amefanya nini kwa Taifa hili yeye akiwa kama kiongozi, kwani kitendo cha kufanya mbinu za kimafia na kuvunja sheria za nchi kwa ajili ya madaraka kwa kweli hakikubaliki.

hii inanikumbusha skendo ya "Richard Nixon" na issue ile ya Watergate. Watu makini hawawezi kufurahishwa na uongozi wa visasi na Uvunjaji wa sheria kwa ajili ya "Power at any cost".

Wana JF tuwe makini sana na Viongozi wa CCM na wale wa UPINZANI, inavyoonekana tumekata tamaa kabisa kiasi kwamba akitokea kiongozi mmoja akafanya kajambo fulani kazuri basi tunamkubali moja kwa moja, inabidi tuwachunguze watu hawa, tuweke rekodi zao wazi, tuwapime kwa nyendo zao hapo ndo tutakuja kujua kwamba fulani angalau anafaa.

Madai aliyoleta mwanzilishi wa mada ni madai mazito, na ushahidi ukipatikana muheshimiwa hana budi kufikishwa katika vyombo vya sheria.

JAMANI TUSIAMINI KIRAHISIRAHISI TUWAPIME HAWA, TUWACHUNGUZE KABLA HATUJAWAPA DHAMANA KUBWA ZA UONGOZI WETU.

Nakubaliana na wewe kabisa Gamba la Nyoka kwa wanaojua vizuri scndal ile ya "Watergate" na aliyoyafanya Nixon na kwa vipi wamerekani wakaamua kumpa alichostahili mpaka akajiuzulu basi tunapaswa nasi kuwa makini..siyo vizuri ku-crash kila mtu anachosema jamaa ametoa wito/rai kwa waandishi wa habari kwenda na kufanya uchunguzi wa kina kisha waujuze umma wa watanzania juu ya mambo hayo yanayoongelewa..tuwe na utamaduni wa kufuatilia mambo katika muda muafaka muafaka.
 
Sehemu ya habari kama hizi, hasa ile ya kulipiza kisasi kwa wana Biharamulo Magharibi na kuchepusha barabara, nilishazikia siku nyingi.

Nawasilina na walio Biharamulo wanipe ukweli wa masuala yote haya.

Kama walivyosema wengi, katika CCM angalau huyu ana unafuu kidogo; kama mchangiaji mmoja alivyosema, CCM ni samaki waliooza ila huyu kaoza lakini unaweza ukajitahidi kumla kwa kuwekamo ndimu.

Kwa urais hafai, labda kwa nafasi ya waziri mkuu - sehemu inayohitaji uchapakazi na ufuatiliaji wa mara kwa mara. Afterall, kwani lazima rais atoke ccm?
 
Bw Burigi msg sent. Wenye akili huchukuwa muda kutafakari na kupima kabla ya kuhitimisha. Wanao-conclude haraka haraka they are not open minded. Keep it up! Kama una taarifa za watarajiwa wengine tumegee.
 
Nakubaliana nawe. Tunaweza kujadili mazuri na mabaya ya potential candidates. Sina tatizo na hilo. Hisia zangu kwa kuangalia "timing" ya hii post, zinanirudisha kipindi cha 2000-05 ambapo ndani ya CCM walianza taratibu kwenye magazeti mbali mbali lakini hasa RAI (akina Salva on behalf of EL and RA) kupakazia tuhuma watu wote waliokuwa wanaonekana tishio la kuweza kushindana na waliyemtaka.

Nina hofu kuwa hiki ndicho kinachoendelea kwa sasa, kuwachafua mmoja mmoja, halafu baadaye wanakuja na ambaye ataonekana mbele ya jamii kuwa hana "uchafu" au ana afadhali kidogo. Lakini ukweli ni kuwa huyo watakayeleta jina lake anaweza kuwa mchafu zaidi, uchafu ambao unakuwa umefichwa makusudi.

Kama ni kujadili, ni vizuri kuwa objective, na kuwa impartial. Yaelezwe mazuri na mabaya ya hao watu.

mkuu mgodi ni tulawaka nimechanganya kidogo sorry kwa kukosea unajua migodi imekuwa mingi hadi unasahau kujua mwingine u wapi lakini habari ndiyo hiyo na kuhusu kuwa yeye ndiyo bora kuliko wana ccm waliobaki nakubaliana na wewe hilo sikatai kabisa lakini je hatutakiwi kujadili na mabaya yake mnataka tujadili mazuri tu

 
Haya sasa,...with 2015 around the corner, agents at work!
Kwangu mimi hii ni Vita ya panzi.
 
Ni muhimu kupata taarifa kama hizi kwa watu wanaofikiriwa kuwa viongozi wetu, na si vizuri kuwakatisha tamaa wanaotoa taarifa hizi na kuwapa watu fulani utakatifu wakati pengine hawana.

Nakumbuka mwaka 2005 watu walivyokuwa wamepagawa kwenye forum ya uchaguzi.com (kama JF ya leo), ulikuwa huwezi kusema neno lolote watu wakaelewa na ulikuwa unaitwa majina yote ya usaliti hapa duniani ukimkosoa mgombea wao kipenzi. Niliandika makala kuhusu sababu 15 kwa nini CCM wamteue SAL-ngumi, mateke na matusi niliyopata kutoka kwa wana uchaguzi.com siwezi kusahau, na leo ndiyo hao wanaoongoza kumpiga mawe aliyekuwa mgombea wao kipenzi.

Sasa tusirudie kosa tulilofanya mwaka 2005 kwa kuendekeza ushabiki wa kijinga na kudharau watu wanaotupatia taarifa za upande wa pili wa wale wanaotaka kuwa viongozi wetu. Huu sio muda wa ushabiki na ubazaza usio na mantiki.

Lazima kila kiongozi tumpime vya kutosha na lazima tugeuze kila jiwe.

Nakubaliana na wewe kwa asilia 100, Na hili tatizo linaendelea kukuwa kwa kasi hapa JF, hatupendi kuona mtu tunayempenda akaandikwa upande wa pili, tukiwa kama ni great thinkers tusiwe wepesi wa kuweka mikono ya baraka kichwani mwa mtu bila kuangalia pande zote tofauti na hapo tutapunguza credibility zetu na wakati mwingine tunajikuta tunakuwa dissaponted baada ya kujua kile tulichokuwa tunaamini ni tofauti
 
You might be 100% right or 100% wrong but that's not important issue right now. Nadhani ni vizuri kujikita kwenye matatizo ya nchi hii ambayo yameipeleka nchi yetu ICU badala ya kila wakati kuwaza madaraka na uchaguzi tu
 
NI kweli haya ni madai mazito lakini hauwezi kuyaamini na kuyafanya ndo hali halisi ya bwana Pombe eti kwa kuwa mtu mmoja kajisikia leo kuyatoa. Miaka zaidi ya 10 imepita toka alipotenda baadhi ya haya, ulikuwa wapi kuyasema?

Hata kama madai yako ni ya kweli, umejiangusha wewe mwenyewe maana hukuyatoa mapema. Matokeo yake madai yako yanazidiwa nguvu na utendaji wake na hivyo watu kumwona yeye anafaa zaidi kuliko madai yako.
Hajachelewa kuyaleta haya mabaya ya Dr Magufuli maana tayari tunaelekea kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2015
Ukiondoa wote CCM angalau Magufuli kidogo kwa hiyo lazima tumchunguze kama kweli atatufaa au hafai

Madai ni mazito tena sana japo jamaa anachapa kazi kwa hiyo tunawaomba waandishi wa habari na wanaohusika zaidi kuendelea kutafuta ukweli wa hili na kutuhabarisha zaidi ili tuamue wenyewe

Magufuli ni mchapakazi na hata Lowasa ni mchapakazi lakini tunaangalia mabaya yao wote ili kujiridhisha kabla ya kufanya maamuzi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom