Kwa wanawake tu!

Najua siku za karibuni mada ya wasaidizi wa nyumbani zimekua nyingi,lakini swali hili litaweza kujaribu kuona namna wanandoa wanavyotazamaHebu fikiri umeolewa,wewe ni muajiriwa pamoja na mumeo nae ni mwajiriwa halafu mumeo anakuuliza tutafute msaidizi hapa nyumbani,nawe ukakubali halafu akakuuliza tutafute wa jinsia gani?Utachagua wa jinsia ipi na kwanini?
Nitachagua wa kike lakini awe Polygon kama ni pentagon nitamfikiria
lakini Circle NO! No! No! No!
 
Nitachagua wa kike lakini awe Polygon kama ni pentagon nitamfikiria
lakini Circle NO! No! No! No!
Ha ha haaa samahani nilifungua bila kusoma heading kumbe
haturuhusiwi, tungekuwa tunaruhusiwa ningesema mimi napenda msichana wa kazi awe yule
ambaye katolewa hatua za awali kwenye miss TZ.
 
Majukumu mengi ya nyumbani anayawezea mwanamke so nitachagua wa kike!! Ila kabla sijamjibu, ningemrudishia kwanza naye hilo swali maanake haya mambo ya jinsia nayo sometimes yanakujaga na intra-personal conflict/interests!
 
Ha ha haaa samahani nilifungua bila kusoma heading kumbe
haturuhusiwi, tungekuwa tunaruhusiwa ningesema mimi napenda msichana wa kazi awe yule
ambaye katolewa hatua za awali kwenye miss TZ.

mmmh!! Huyo sister do mi sitamuweza. Kazoea pizza za uncle Lundenga leo hii nije kumwambia anipikie ugali wa mhogo ataweza?? Chai ya watoto asubuhi mpaka a apply make-up saba saba ndo iandaliwe saa ngapi? Kwenda sokoni kwenyewe, mwendo wa Happiness magese.......NO a.k.a HAPANA!!
 
Haya mambo ya house-girl kwa kweli mi siwezi kuchangia sana maana PERSONAL OPINION ni kwamba ni utumwa fulani, na we can live without.
nikirudi kujibu swali la thread, house-girl ni mfanya kazi kama wewe na mume wako, anakuja hapo kufanya kazi za ndani, apokee mshahara wake na aendelee kimaisha.
Sasa kama mtaanza kuangalia wazuri na wabaya, wanawake na wanaume, basi hata offisini wakatazeni waume zenu kufanya kazi katika ofisi ya wanawake wazuri. house-girl wowote ukimlipa the minimum wage (ambayo inalingana kweli na kazi anazo zifanya ndani) atakua msafi na mwenye kuvutia (they are younger than you, kwa kawaida) na kama mume wako haaminiki kwa housegirl na huko nje haaminiki pia.
Alternative ni kama alivo sema Lizzy kutafuta wa kuja day time, au twice/trice a week.
 
RusianRoulete,hujasema sababu ya kuchagua wa kike!
 
Wifi kwa maisha ya jijini,nyumba mnaiacha alfajiri mnaiona saa moja usuki,hgal ni sawa na mlinzi wa mchana. Wakasti mwingine mna safari za kikazi watakuja kuwahamisha bila hiari mkirudi mwajikuta wageni. Kama una mwenza ambae humuamini hata kuishi nae na hgal,sidhani kama ni sawa kuwa na mwenza huyo kwa kweli

Kama mtu anaishi na mumewe kama partner hana haja ya Mfanyakazi pale tu mkioana... Maana mpo wachache (yaani wawili) ni rahisi saana kumangae... Chakula ni cha the whole week kinanunuliwa weekend, usafi kama kufua & kunyosha, mazingira ndani na nje ni siku moja ya weekend, Kupika ukijimanange kikubwa uwe na Microwave yasaidia saana.

Kimbembe kinakuja kama mnaishi na familia zaidi... yaani iwe mtoto/watoto wa ndugu... Mfanya kazi ni inevitable... Tena wa kike...
 
King'asti,kwanini uishi na mtu usiemuamini?
 
nitachagua jinsia ya kike kwa sababu sitokuwa na wasiwasi na mume wangu
 
Ningechagua wa kike,manake anamudu shughuli nyingi nazohitaji msaada nazo kutokana na kazi nyingi!!
 
Back
Top Bottom