fikirikwanza
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 7,452
- 3,065
- Thread starter
- #41
Je Mh. Halima Mdee na Uwaziri kivuli wa Ardhi, Nyumba na Makazi; Juu ya hili unasemaje kwa wananchi wa Tanzania???
Sijafanikiwa kusoma maelezo yote ya kwenye uzi wako na hiyo ni kutokana na malalamiko mengi yasiyo na tija na kubwa ni ujinga tu wa kutoelewa kuhusu viwango vya bei ya ardhi. Ni vyema siku nyingine ukawa unauliza kuliko kulalama.
kwa ufupi; ardhi ndio raslimali mama kati ya zote, na uthamani wa ardhi umetofautiana kutokana na eneo ilipo ardhi hiyo, na thamani yake pia uongezeka siku hadi siku, lakini pia hutokea mara nyingine kwa thamani ya ardhi kushuka (laws and policies, zoning ana planning regulations etc).
Kuhusu bei ya ardhi; bei ya ardhi kwa soko huria uamuliwa na nguvu ya mahitaji na utoaji (demand and supply factors), kwa soko huria kiwanja ambacho kimepimwa na kina hati (a plot), kwa mita za mraba sio chini ya Tshs 30,000. Sasa zidisha hicho kisa na ukubwa (kwa maana ya eneo) la kiwanja husika, hii ni kwa Dar es salaam na maeneo mengine ya nchi yenye hadhi ya miji na majiji. Kwa Masaki, Upanga and the like; kwa mita square moja hupati kiwanja chini ya Tshs. 1,500.000. Kwa hiyo soko huria ndivyo lilivyo.
Tuje kwa serikali; serikali ya Tanzania imekuwa ikiuza ardhi na kuitoza kodi ardhi kwa bei ya kutupa kabisa, mleta mada kama uamini, hilo eneo unalo lalamika, hemu jaribu kuuliza kwa soko huria kiwanja bei gani, kwenye eneo hilo hilo. Tuache milawama ya ajabu na muda mwingine tuisifu serikali hasa kwenye kuhakikisha raia wake wanapata makazi yao wenyewe.
Gvt plots are the cheapest though not affordable. Plot price is the summation of land acquits ion cost, survey costs, title deed preparation costs plus a premium of less than 15% call it a profit but in actual sence it serves as a revolving fund for future projects. If you are to pay a fair compensation, there is no way plots are going to be cheap because the two are dependent but very much opposing each other.
my opinion, we need to change our perspective, let the Nhc, NSsf, ppf etc construct as many houses as possible and float in the market for lease- purchase (call it mortgage), tuachane na ufahari wa kujenga nyumba wenyewe, hii biashara ndo kwanza inachangia ufisadi kwa kiwango kikubwa. Tax very very heavily private property developers, I'm telling you mwisho wa siku stress za nyumba zitapungua, wanaostahili (matajiri) kujenga nyumba watajenga wenyewe Si wengine tutaendelea
Inasikitisha sana kuona mtanzania hana fursa nzuri ya kujenga makazi bora kutokana na dhana mbaya ya serikali ya kuggeuza ardhi kuwa mtaji mkubwa wa mapato ya kuendesha nchi, yaani haki mojawapo ya makazi kati ya nne za maji, chakula, makazi, mavazi inagandamizwa kwa kasi kubwa.
Hebu tujiulize kwanini bei ya kiwanja iwe kubwa kuliko kipato cha mfanyakazi wa kima cha chini kwa mwaka mzima??? kweli sera za CCM zinaakili??? yuko wapi Filiku
njombe, yuko wapi Makamba January, yuko wapi Mama Anne Kilango, yuko wapi Sitta yuko wapi Mwakyembe, yuko wapi Waziri anayehusika na Makazi, Yuko wapi waziri wa Ardhi, Yuko wapi waziri wa maendeleo ya jamii, yuko wapi Waziri MKUU, yuko wapi RAIS???????
Zaidi yote yuko wapi Mbunge, ambaye tunamlalamikia kila siku kuhusu bei ghali ya viwanja, aliyeahidi kwenda kuongea matatizo yetu bungeni yuko wapi???
Je hata ardhi ambayo mungu katupatia bure nayo inashindikana kuigawa kwa watanzania ili wajenga makazi bora, inakuwa suala la tajiri hata na hili? kulala sehemu nzuri imekuwa luxury????
Ushauri wangu kila mtu apewe kiwanja kwa bei ya laki 1-5 tu, serikali ivunje mtandao wa ulanguzi wa viwanja; ardhi sio biashara, iweje mtu anachukua viwanja 50 ili auze kwa bei ghali, udhaifu wa serikali ukome sasa. Mbaya zaidi wakati wa magufuli alidai hata naibu wake RM alikwa na viwanja vingi vingi amejilimbikizia.
Unyonge wetu ututoke kwanza ndo tusitahili haki. TUUNGANE KUPAMBANIA HAKI YA MAKAZI BORA