Mlenge
R I P
- Oct 31, 2006
- 2,125
- 2,291
Habari wandugu,
Katika kutoa huduma kwa jamii, napenda kuwashauri watu wanaotaka kujiendeleza kielimu, maarifa na kiteknolojia. Wapo watu wanaopenda kujiendeleza kwenye nyanja hizo, na hukosa watu wa kuwauliza. Au pengine wangependa kupata mawazo mbadala.
Kama unataka kujiendeleza kielimu, na ungependa kufahamu zaidi na kupata ushauri kuendana na ulipo na unakotaka kufika, tutumie uzi huu kuweka bayana uyatakayo. Iwapo hungependa uyatumayo yaonekane kwenye hadhara, basi jiunge kwenye tovuti ifutayo kwa ajili ya faragha zaidi: https://trello.com/invite/b/sT4WMZ3C/c3e273f5230374e65b1212217a165614/shule
Wapo wengine wanaopenda kusoma nje ya Tanzania, au ndani ya Tanzania, lakini kwa malengo mahsusi. Wengine wanasoma wapate cheti tu, wengine kwa sababu fulanifulani hawakupata fursa ya kusoma, sasa wanataka kujiendeleza, wote hawa wana nafasi yao ya kupata ushauri.
Sikai sana mitandao ya kijamii, lakini nitajitahidi kumjibu kila mmoja, hata kama si papo hapo.
Kuhusu mimi, nimejaliwa kupata fursa ya kusoma zamani na miaka ya karibuni. Kadhalika nimepata uzoefu wa kozi fupi na ndefu, ndani na nje ya Tanzania.
Karibuni!