Kwa wanaotafuta wachumba wa kweli wa kuoana

Kimbweka uko juu ndugu yangu, ndio maana pale Buguruni unawakamatia vibaya sana wakikuona ulivyojipigilia.

Darasa Huru linaendelea kama anavyotuambia JOS MTAMBO & JLT.


Ukidili na Watoto wa Shule, Chipsi kuku Nyingi,
Ukiwapata hakuna kushangaa, Watakuita mdingi,
Usiogope Uniform, Begi zina nguo za home.
Pozi kimtoni, tabasamu akuone handsome,
Au shika sigara nuna, akuone Gangster,
Ukipendana na demu bomba anavuta, tembea na lighter.

Je umechagua kibonge? Kama wacheza sumo?
Hata kama we fidodido imo.
Pamba zimkatae? usisite kumsifu,
Mwambie akipungua atakua zinga la model.

Utakunywa nini? Sema shampeni, au sema red wine, sema original ya kutoka Paris.
Kunywa pombe, badili lugha, ongea ung'eng'e, kiengereza, kwasabu huwezi, maneno meza.

Kama demu wako mfupi, watoe kasoro warefu.
Msifie nywele, msifie mguu, penzi juu.
Kama ye sista duu, kua brother duu,
Ringa kidogo, toa manjonjo ya buble-gum

Hili ni darasa Huru,
Mambo si safi mpeto,
Shika lako,
Shika na la mwalimu,
Hujashikwa mikono,
Hujashikwa miguu,
Akili ni nywele,
Kila mtu anazo zake!!!
 
Mie nashukuru kwa Mayasa wangu hiyo Rasimu Mpya ya kutongozea haikunihusu kabisa, nilimwita enzi hizo Palm beach Hotel 1979 nikafunguka tena kwa umakini kama nasoma Hotuba maana nilikuwa kihisia zaid nashkuru Mtoto alinielewa, Rest in Piece My MAYASA. GOD created you for Me and I was Created for YOu:
 
Back
Top Bottom