Kwa wanaorudisha kadi za CHADEMA na kujiunga na CCM

The sage

Member
May 25, 2011
29
4
Hapa naomba tuwe wakweli. Kwa maneno yao wenyewe viongozi wa juu wa CCM wameshuhudia kuwa chama kimepoteza mvuto kwa watanzania na hasa kwa vijana. Wakati huohuo CHADEMA ni chama kilichojipatia umaarufu mkubwa na kukifunika CCM kwa kila namna, hasa kwa wakati huu.

Hivyo mtu anaporudisha kadi ya CHADEMA na kujiunga na CCM ni wazi kuwa ni kwa maslahi binafsi hasa kwa kujipatia fedha za kujikimu kutokana na hali ngumu ya maisha au kwa tamaa tu ya kujilimbikizia mali. Kwa mtu mzalendo kweli na anayejali maslahi ya Taifa hawezi kujiunga na chama cha magamba ambacho badala ya kurekebisha kasoro zake kinazunguka kuupotosha ukweli ambao wakombozi wa kweli wamejitahidi kuwafumbua macho watanzania.

Jamani watanzania tuamke, tuache kurubuniwa na visenti vichache huku tukiviweka hatarini haki na uhuru wetu kwa chama hiki kisicho na huruma kwa watanzania!
 
hakuna anayerudisha kadi, kama wanavyotafuta watu na kuwabeba katika mafuso, kujaza watoto ktk kumbi za kujadili katiba, ndivyo hivyo walivyotafuta watu kuwatafutia kadi za chadema na kuwapa za magamba, wanajidanganya wenyewe.
 
Kiukweli unaweza kukuta watu wamehamasishwa kwa kubebwa na malori,pengine kupewa chochote ili warejeshe kadi,kama shahada za kura zinanunuliwa itakuwa kadi ambayo ni rahisi kuipata?
 
Kwa hiyo kama hakuna anayerudisha kadi wasi wasi wenu wa nini? Si mrelax kidogo muone 50yrs of experience ina worth kitu gani.
 
Kuna cku nilipigiwa cm na watu fulani nisiowajua,wakaniambia wao ni wanafunzi wanataka kadi,nikawauliza ngapi,wakajibu kama 50,wako wanne kad 50,wapi na wapi,tena wanasema kwa 2000,nikakataa,wakapanda kwa 3000,bd nikagoma,mara mwenyekiti wangu akanipigia kuna watu wa Ccm,wanataka kadi zetu,usiuze leo,HIZO NDIZO MBINU ZA CCM
 
[QUOTENafikiri unahitaji kuvuliwa gamba mazee, mende mkubwa wewe, maskini wa mali na akili na mtu usiye hata na haya msalimie Malaria Sugu=Nduka;2046283]Kwa hiyo kama hakuna anayerudisha kadi wasi wasi wenu wa nini? Si mrelax kidogo muone 50yrs of experience ina worth kitu gani.[/QUOTE]
 
Hapa naomba tuwe wakweli. Kwa maneno yao wenyewe viongozi wa juu wa CCM wameshuhudia kuwa chama kimepoteza mvuto kwa watanzania na hasa kwa vijana. Wakati huohuo CHADEMA ni chama kilichojipatia umaarufu mkubwa na kukifunika CCM kwa kila namna, hasa kwa wakati huu.

Hivyo mtu anaporudisha kadi ya CHADEMA na kujiunga na CCM ni wazi kuwa ni kwa maslahi binafsi hasa kwa kujipatia fedha za kujikimu kutokana na hali ngumu ya maisha au kwa tamaa tu ya kujilimbikizia mali. Kwa mtu mzalendo kweli na anayejali maslahi ya Taifa hawezi kujiunga na chama cha magamba ambacho badala ya kurekebisha kasoro zake kinazunguka kuupotosha ukweli ambao wakombozi wa kweli wamejitahidi kuwafumbua macho watanzania.

Jamani watanzania tuamke, tuache kurubuniwa na visenti vichache huku tukiviweka hatarini haki na uhuru wetu kwa chama hiki kisicho na huruma kwa watanzania!

CHADEMA ni zaidi ya fusso na taarab, ni zaidi ya michakato ya uzamani na upya wa kamati, ni zaidi ya ahadi na matembezi ya kusikiliza kero, ni zaidi ya nyama choma na bia baridi, ni zaidi y halua na tende. CHADEMA imo mioyoni mwetu, na moyo ndio msingi wa uhai yaani LIFE. Kwa maneno mengine CHADEMA is life, na LIFE haiandikwi kwenye kipande cha karatasi! Nape can collect all sorts of papers in this planet lakini hawezi kukusanya kilicho mioyoni mwa watanzania wengi! Atakusanyaje life? hawezi!
 
Ni kweli kwamba kadi zinarudishwa ila SI KWELI kwamba walipewa na CHADEMA.
Wamepewa kadi kabla ya mkutano wazirudishe kwenye mkutano kwa aliyewapa.
Ni sawa na kujifariji kwa kuandika barua ya posa na kisha kujijibu mwenyewe kwamba umekubaliwa halafu unawaonesha watu barua yako ya kukubaliwa posa.
 
Kadi za Chadema zinanunuliwa na Magamba unaambiwa ukirudisha Kadi ya Chadema unapewa Khanga, Kofia na Pesa ya kula siku 1 au 2. Na walio wengi wanafuata pesa na khanga na wala Magamba wasikutishe ukiona Kadi subiria uchaguzi 2015 ndio utakapojua kuwa Magamba wanavyopigwa chini na kufilia mbali
 
Night blindness, kuchuma nyanya za kijani wakiona zimeiva kwamba ni nyekundu.
Kukicha wanagundua makosa waliyofanya usiku.
 
Back
Top Bottom