Kwa wanaopenda ufugaji mkubwa

Discussion in 'Ujasiriamali' started by Malila, Aug 24, 2009.

 1. M

  Malila JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,044
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 38
  Kama kuna wanaopenda kufuga wanyama hasa Mbuzi ( wa maziwa,nyama),njooni tuunganishe nguvu tufanye mambo.Inawezekana kabisa tukafuga kwa mafanikio sana. Kila kitu kipo ndani ya uwezo wetu.

  I believe together we can go.
   
 2. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,526
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 38
  Mnaweza kuanza wawili au watatu hivi. Baadae mnaanza kuuza uzoefu wenu kwa wengine watakaokuwa tayari kuunda vikundi.
  Picking partners should not be taken lightly. It is a vital step for your mission to prosper.
   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,044
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 38
  Asante mkuu,usemacho ni sahihi kabisa. Uwingi si hoja,kikubwa tija ktk jambo lenyewe.
   
 4. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,526
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 38

  Yes, hata hivyo, ni muhimu kufikiri mapema au kuwa na wazo la namna ya ku-expand baadae. Tuseme kuaandaa semina kwa wengine baadae, ambapo ni fursa ya kujitangaza hali kadhalika kuuza sehemu ya ulichozalisha.
   
 5. m

  masapa Member

  #5
  Aug 25, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante Bw. Malila. Ni wazo zuri sana na niko tayari.
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,044
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 38
  Stay tuned,ukiweza ni-pm ili tuanze mawasiliano, nimejaribu ktk mradi fulani kwa kuwatafuta watu wenye intrest ile,mwanzo ilikuwa taabu kidogo kwa sababu ilibidi nitoboke kiasi. Lakini sasa nashindwa kuwatosheleza wahitaji wa ile project.

  Lazy dog kasema vema,on how to pick b/ness partiners. Mkuu njoo tujipe moyo tutashinda.
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,044
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 38
  Nursery ya kitu hiki niliijaribu mahali fulani,kwa hiyo wazo hili lilipata msukumo kutokea ktk nursery hiyo. Ndoto za kuanza na ku-expand zipo na kubwa tu.
   
 8. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 910
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 18
  malila, hii thread imenikumbusha ile safari ya Mkuranga!!
   
 9. Tiger

  Tiger JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2010
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,693
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 36
  Tuko pamoja wakuu.
  Tutawasiliana kwenye pm zaidi.
   
 10. Tiger

  Tiger JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2010
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,693
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 36
  Safari ya Mkuranga niliisikia kwa Malila.
  Poleni sana na zile mvua.
   
 11. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 12,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 38
  Mkuu Malila, hongera kwa kufuga. Mie nina mpango wa kwenda kufuga wilaya moja huko mkoani Tanga. karibu nawe
   
 12. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 38
  wazo zuri jamani na mm nipo tayari mtakapoanza
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,977
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Je mbuzi anaweza kufugwa na kustawi vizuri katika maeneo yapi?

  Je maeneo ya pwani yanafaa kwa ufugaji wa mbuzi?
   
 14. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,569
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mimi natafuta ranch kubwa hizo za selikali, nataka kufuga ng'ombe wa maziwa na nyama si chini ya mia tano kwa kuanzia. kama kuna mtu anayeweza kunisaidia namna ya kuzipata anipigie pande hapa. kwahabari ya pesa, si zaidi ya $1 million. asanteni.
   
 15. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heshima kwako mkuu, the idea is sweet but for me you have to be so elaborative on how to share your idea.
   
 16. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 48
  Unapita lini kanda ya kti Mkuu Malila? Nami nakumbushia issue ya Mkuranga
   
 17. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 910
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 18
  kanda ya kati unaendeleza kilimo gani
   
 18. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 48
  Nimeanza na mahindi; lakini pia nataraji kuanza ufugaji wa kuku wa kienyeji na nikijufunza zaidi hata hao mbuzi wa nyama
   
 19. Mrbwire

  Mrbwire JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2010
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF. hasa wajasiliamali walio katika sekta ya ufugaji. Ninaomba mchango wenu wa mawazo kuhusu ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.

  • Ni aina gani ya specie inafaa kwa mfugaji aliyeko maeneo ya joto kama Dar es salaam?
  • Kuna friends walinunua ng'ombe wa maziwa kutoka Iringa na Arusha; ng'ombe bora wenye uwezo wa kutoa lita 18 kwa mkamuo mmoja. Baada ya kuwafikisha DSM walidhoofika, wakashusha production na mwisho walikufa mmoja baada ya mwingine. Je, ni kosa kuwachukua ng'ombe eneo la baridi ukawapeleka sehemu yenye joto kama DSM?
  • Kwa mtu aliyeko DSM na maeneo ya jirani, ni wapi anaweza kupata specie bora za ng'ombe? Cost ya ng'ombe ni kiasi gani? Tupeane contacts na taratibu zinazofuatwa ili kupata ng'ombe hao
  • What are the "Dos" and "DONTs" kwa mfugaji wa ng'ombe wa maziwa? (Mfano when we talk about chakula chao, malazi na pia pakiwa na maradhi n.k)
  Mwisho napenda kutoa changamoto kwa wajasiria-mali kuitazama biashara hii kwa jicho la tofauti. Naanza kuhisi kuwa ni sawa na mtu anayemiliki kisima kidogo cha mafuta. Tena anachimba mwenyewe na bila ushuru mkubwa. KWA NINI NINASEMA HIVYO?... Ninasema hivyo kwa sababu lita ya maziwa kwa sasa inakwenda mpaka 1,200/=! Mtu aliye na ng'ombe watatu wenye kutoa lita nane kwa mkamuo ana uwezo wa kupata lita 48 kwa siku. Lita 48 ni sawa na shilingi 57,600/= kwa siku! Kumbuka huyu tunayemuongelea ni mfugaji mdogo kabisa mwenye ng'ombe watatu tu!

  Naomba kuwakilisha kwa kuwaomba wadau kuchangia mawazo juu ya project ya Ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.... Tafadhali nipewe mwanga zaidi kwenye hizo dondoo nne hapo juu.
   
 20. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani uende wizara ya kilimo na mifugo. Onana na wataalamu wa Ng'ombe wa wizara, nadhani watakupa information ambazo zitakusaidia sana. Naamini watakushauri mpaka maeneo ya kufugia hao ng'ombe wako.

  It's a good move though, according the calculation above.
  Make your move, isiishe kwenye maandishi tu.
   
 21. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #21
  May 20, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,339
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 38
  kama upo dar nenda pale mandela rd just after tazara area ,kuna wizara husika watakupa ushauri mzuri wa mbegu bora ya ng'ombe wa maziwa,na pia how to's za kufuga,ila fahamu kufugia cows in dar ni gharama sana na inachukua muda wako mkubwa,kwani majani ni ya kununua ,bora ufugie mkoa wa pwani,eg kibaha,chalinze ,or mkuranga, siyo mbali sana na dar and u can transport maziwa yako kila siku kuliko kufugia dar na kuwa na headache ya malisho ya hao wanyama
   
 22. t

  thesonofafrica Senior Member

  #22
  May 21, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  usisahau hawa wanyama wana gharama sana kuwatunza na kuwatibu.
  Hivyo,hesabu yako ya juu ni theoretical zadi.
  ni sawa na mtu anapokumbia kuwa ukiwa na daladala Dar kila siku utaletewa 40,000.
  ina mana kwa wiki 280,000.Kwa mwezi 1,120,000.Hiyo ni theory.
  Practically ukiingia unakuta sivyo.Mwenzako yalishanikuta kwenye biashara ya Tax cab.
  Hivyo,piga hesabu vizuri kabla ya kuamua kuwafuga hao wanyama,
  All the best.
  THE SON OF AFRICA
   
 23. PoliteMsemakweli

  PoliteMsemakweli Senior Member

  #23
  May 25, 2010
  Joined: Nov 21, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 6
  Ukitaka ushauri wa harakaharaka unonana na DK Michael yuko pale Ubungo opposite na TANESCO simu namba 0713344576.
   
 24. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #24
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 48
  Wadau wa jukwaa

  Hebu tushirikiane kuijenga hii ili ije kuwa muhtasari ufaao
   

  Attached Files:

 25. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #25
  Aug 22, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 517
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 18
  kaka maskini jeuri nakupongeza kwa mtazamo wako wa kiujasiliamali,,ni mzuri sana kuliko hata kuajiliwa,,kwa kuwa unataka kufuga kuku naomba unipe mawazo muhimu uliyoyapata kuhusu huu ufugaji,,,maana mimi pia nina mpango huo tangu siku nyingi na sasa nipo kenywe mchakato wa kukusanya mawazo kutoka kwa wadau mbalimbali..ninatanguliza shukurani zangu mkuu.
   
 26. kasopa

  kasopa JF-Expert Member

  #26
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Boss wazolako ni zuri linatakiwa kufanywa kazi lakini hapahujatoa maelezo ya kutosha kumvutia mtu tunapenda kujua mahesbu yaununuzi malsho na ukuaji mpka uanze uzalishaji kama ni maziwa ama nyama na pia hao mbuzi unapo wanunua wanakuaw tayari namimba mabakuna jama alichangia hoja katika ushauri flani alifafanua mpaka nikawa na hajayakuianya nanukuu,


  Mimi ni mfugaji, nitakushauri kufuga ngombe kwa mchakato ufuatao:

  Ujenzi wa banda = Ths 500,000/=
  Manunuzi ya Ngombe 5 x Tsh 900,000 = Tsh 4,500,000/=
  (Ngombe utawanunua wakiwa na mimba ya miezi 6)
  Kuwahudumia ng'ombe kwa miezi mitatu kabla ya production = Tsh 1,500,000/=
  (inahusisha mshahara kwa wafanyakazi wawil + chakula + madawa)

  Jumla = Tsh 6,500,000/=

  Baada ya Miezi 3;

  UZALISHAJI:

  Ngombe hawa watakuwa wakitoa maziwa si pungufu ya lita 5 kwa asubuhi na jioni kwa kila ng'ombe. Hivyo uzalishaji kwa siku utakuwa lita 10 kwa siku kwa ng'ombe.

  MAPATO

  Lita 10 x Ng'ombe 5 = lita 50 kwa siku x Tsh 1000 (bei ninayouza mimi hapa) = Tsh 50,000 kwa siku
  Mapato kwa mwezi = Tsh 50,000 x 30 = 1,500,000/=

  Gharama za uendeshaji kwa mwezi = Tsh 600,000/=

  Faida = Tsh 900,000/= kwa mwezi

  BAADA YA MIAKA 5:

  Kumbuka ng'ombe huzaa kila mwaka hivyo basi baada ya miaka mitano utakuwa na ng'ombe wasiopungua 25. Kipato chako kwa mwezi unaweza kufikia si pungufu Tsh 18,000,000 endapo utakuwa na ngombe jike 20 kati ya hao 25
  Asante kwa ushauri mkuu

  I believe together we can go.[/QUOTE]
   
 27. D

  Dafia Senior Member

  #27
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [/QUOTE]

  Hii nimeipenda sana hao ng'ombe wanapatikana wapi? tupe contact na sisi tuingie kwenye ufugaji.
  Maana hiyo faida kwa mwezi inazidi mshahara wangu.
   
 28. M

  Malila JF-Expert Member

  #28
  Sep 14, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,044
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 38
  Hii nimeipenda sana hao ng'ombe wanapatikana wapi? tupe contact na sisi tuingie kwenye ufugaji.
  Maana hiyo faida kwa mwezi inazidi mshahara wangu.[/QUOTE]

  Ng`ombe wazuri wa maziwa original (friesian) wapo kitulo Makete - Njombe,wanauzwa laki sita. Wamepandishwa tayari na ni shamba la serikali la mfano kwa sasa. Tatizo ni kuwasafirisha mpaka ulipo.
   
 29. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #29
  Sep 14, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,571
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 38
  Wakuu,

  My dream ilikuwa kufuga nguruwe, lakini tangu July 2008 nilianza na kuku wa mayai 500, nikaja 1000, then nikauza wale 500 wa mwanzo, so far business yangu imerudisha capital which was arround 9m. Tangu June 2010 nimeanza kupata Project Profit. Lakini Setup nzima including fixed assets eg Maji, mabanda, solar, nyumba za shamba boys ilikuwa 18m. Kwa hiyo bado 9m ku Break even.

  Kwa sasa ninao 1500, production kwa siku ni Trays 37 kwa siku ambapo sales @5,000 per Tray napata 175,000 Kwa Siku

  Chakula wanakula kilo 175 - mifuko 3.5 ya Kilo 50 @ 24,000 = 84,000

  Madawa , Manpower ni 250,000 kwa mwezi average.

  Profit = 175,000 - 84,000 = 91,000 Kwa Siku times 30 days you get = 2,730,000 Tshs - man power & Running cost = 2,480,000/= Kwa Mwezi. (Hii ni cash in hand per month)

  Expanstion by June 2011 ni 3 times of this production. and In June i will be selling those kuku mzee ones kwa 5,000/= each so nitapata 5m, which i can use this cash to re invest.

  Its a risk business but watch out.
   
 30. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #30
  Sep 14, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,571
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 38
  Mlila tatizo wana JF wengi hawako serious katika kilimo na ufugaji - May be hawako familiar
  sababu wamekulia mijini, sasa unapoongelea kufuga nguruwe, kilimo cha Mitiki, Kilimo cha Mpuga kwa umwagiliaji, ufugaji wa mbuzi wa maziwa & ngombe etc watu hawakuelewi kama inawezekana ukapata pesa hadi Tsh 20m kwa mwezi. Mtu yupo radhi avumile mshahara wa 2m kwa mwezi na gari moja na nyumba ya kupanga kijitonyama hadi anafikia umri wa kustaafu.

  Lakini hizi forum zitawaamsha wengi, hakuna haja ya kugombana na bosi wako akupe allowances, allawances zipo shambani. Anyway wachache watakaofuata maoni yako watafaidika sana.

  Kuna jamaa utawasikia - "Yaani mi Engineer, Mwansheria mzima nikafuge nguruwe / kuku !! nitake radhi", ha ha ha
   

Share This Page