Kwa wanaopenda makalio makubwa - tahadharini na waganga feki

bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
7,326
6,718
Haya mambo hayoooooo!

Mwanamama mmoja nchini Marekani aliyetaka kuutengeneza mwili wake uwe wakuvutia zaidi amejikuta matatani, baada ya kudungwa sindano za saruji na gundi ili kuongeza ukubwa wa makalio yake.

Mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina kutokana na sababu za kisheria, alikuwa akitaka kufanya kazi katika klabu ya usiku, na hivyo alitafuta daktari anayeweza kumbadilisha, lakini kwa bei nafuu.

Polisi wamesema mwanamke huyo alikutana na mwanamke mwingine aliyejifanya ni daktari, na kuanza kujaza mwili wake kwa saruji, gundi ya kuzibia matairi na mafuta. Msichana huyo alilipa dola mia saba ili kupatiwa hips na makalio ya kuvutia.

Hata hivyo sindano za mchanganyiko wa saruji, na mafuta na gundi zilimsababishia maumivu makali na akalazimika kwenda hospitali. Kila alipokwenda hospitali kutokana na maumivu alikuwa akiona aibu kusema hasa chanzo cha maumivu yake.

Hata hivyo mama wa msichana huyo alimbana mwanaye hadi akasema kilichomsibu. Polisi walimkamata daktari huyo feki na kumshtaki kwa kosa la kufanya udaktari bila leseni na pia kusababisha maumivu.

Mamlaka za huko zinasema huenda kuna wasichana wengine wengi wamekumbwa na jambo hilo lakini wanaona aibu kujitokeza.


Source: BBC Swahili (Kisa na Mkasa)
 
....Ukitaka uzuri (kama hukuzaliwa nao) shurti udhurike
 
Back
Top Bottom