KWA WANANDOA TU: Haki Za Mume Na Mke

Baba Mtu

JF-Expert Member
Aug 28, 2008
870
168
Je, wewe ni mwanamke na umeolewa???!!! Je, wewe ni mwanamume na umeo???!!! Kama jibu ni ndio, fungua hapa Haki Za Mume Na Mke | Alhidaaya.com ili usome na uelewe nini wajibu wako kwa mumeo/mkeo na ni nini haki yako kutoka kwa mumeo/mkeo. Ukishasoma unatakiwa umtekelezee mwenzio haki yake ili ndoa yenu idumu, na utakuwa na kila sababu ya kudai haki yako kutoka kwa mwenzio. Kazi kwenu nyie mlio katika ndoa.

MUHIMU: SOMA KWA MAZINGATIO ILI UELEWE, CHUKUA YANAYOKUFAA NA UYAACHE YASIYOKUFAA
 
baba mtu safi sana kwa juhudi zako za kujaribu kunusuru ndoa.safi mno!

Du i can not believe that the book condones whipping women, kumbe wanaume wengi waislamu wakiwachapa viboko wake zao wanaweza kusema ni sehemu ya maelekezo ya dini. Na serikali haitatakiwa kuingilia kati uhuru wa dini.
 
Du i can not believe that the book condones whipping women, kumbe wanaume wengi waislamu wakiwachapa viboko wake zao wanaweza kusema ni sehemu ya maelekezo ya dini. Na serikali haitatakiwa kuingilia kati uhuru wa dini.

Umeilewa visivyo hiyo haya, nakushauri mtafute mwanazuoni akufafanulie zaidi. Na sio peke yako bongolander walioielewa vibaya hiyo haya na nyingine kama hizo. Hebu soma tena:

Mume vile vile ni wajibu wake kumtia adabu mke anapohisi uasi wa mke wake kama alivyoamrisha Allaah سبحانه وتعالى katika kauli ifuatayo :

وَاللاَّتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلاَ تَبْغُواْ عَلَيْهِنَّ سَبِيلاً إِنَّ اللّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا

{Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu} (An-Nisaa 4:34)

Aya hii inataka maelezo kidogo kwani baadhi wa wanaume wameifahamu sivyo Allaah سبحانه وتعالى Aliposema "muhame katika malazi na wapigeni"

Ibn Abbas na wengineo wamesema kuwa Aya imemaanisha kupiga mpigo usio mkali (yaani mpigo hafifu) Al-Hassan Al- Basri kasema kuwa ina maana mpigo usio wa nguvu.

Maulamaa wameelezea maana hasa ya kauli hii kwamba inamaanisha:
a) Kwanza mume amnasihi mkewe bila ya kumshutumu au kumuonea au kumtia aibu kwa watu. Atakapomtii hapo basi yawe yamekwisha. (sio unakurupuka na kuanza kumpiga mkeo bila kumsihi kwanza).

b) Atakapoendelea kutokumtii mume wake basi awe mbali nae kitandani, yaani asiwe analala nae kwa muda hivi wala asiseme nae mpaka mke ahisi vibaya ajue kuwa kweli mumewe kakasirika nae, Pindi mke akikubali makosa yake basi yawe vile vile yamekwisha warudie hali yao kama kawaida . (kabla hujampiga mkeo baada ya kumuonya kwa makosa alokufanyia, inatakiwa wewe mumemtu umpe azabu ya kumtenga wakati wa kulala tu, yaani hufanyi nae tendo la ndoa. Mambo mengine yanaendelea kama kawaida)

c) Kisha tena ikiwa bado mke hana utiifu, hapa sasa mume anaweza kumpiga mkewe.
(katika uislam kumpiga mkeo ni hatua ya mwisho kuichukua baada ya kumuonya kwa maneno/mdomo na kisha kumnyima unyumba kwa siku kazaa).
Lakini sio kumpiga kwa nguvu kama walivyofahamu waume wengine bali kama alivyotuelezea Mtume صلى الله عليه وسلم katika hadithi ifuatayo:

في صحيح مسلم عن جابر عن النبي صلى الله عليه وسلم : أنه قال في حجة الوداع :

واتقوا الله في النساء فإنهن عندكم عوان ولكم عليهن ألا يوطئنفرشكم أحدا تكرهونه

فإن فعلن ذلك فاضربوهن ضربا غير مبرح ولهن عليكم رزقهن وكسوتهن بالمعروف

Imepokelewa na Muslim kutoka kwa Jabir kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema katika Hijja ya kuaga {Mcheni Allaah kwa wanawake kwani wao ni wasaidizi wenu. Mnayo haki juu yao kuwa wasimuruhusu mtu msiyempenda kukanyaga zulia lenu. (kuingia katika nyumba yao) Lakini wakifanya hivyo, mnaruhusiwa kuwatia adabu ndogo. Wao wana haki kwenu kwamba muwatimizie matumizi yao na nguo kwa njia ya kuridhisha
Haya inayofuata baada ya hiyo ya 34 inasema:

""Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari. Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri (An-Nisaa 4:35-36)

Uislam unamthamini sana mwanamke tofauti na wengi wanafikiria. Je, unajua kuwa kwa mfano wewe bongolander umemfumania mkeo akizini na mwanamume mwengine, huna haki kumpiga wala kumtolea siri kwa watu wengine???? Sharia Law inakuhitaji ulete mashaidi wanne walioshuhudia mkeo akiziniwa na huyo mwanamume utakayemtaja. Ukiona hamuelewani na mkeo ni bora ukampa talaka kuliko kuanza kumtolea kashfa kuwa yee ni mzinifu, iwapo utamfumania na ukakosa mashaidi wanne walioshuhudia kitendo hicho.

Ndugu bongolander usiwe na shaka na quran, ni kitabu kisicho na shaka ndani yake, vitu vinavyohitajika na binadamu vinapatikana humo.

Ewe bongolander nakuomba fungua tena hapa http://www.alhidaaya.com/sw/node/246
usome unayopasa kumtendea mkeo kama umekwishaoa

MUHIMU: SOMA KWA MAZINGATIO ILI UELEWE, CHUKUA YANAYOKUFAA NA UYAACHE YASIYOKUFAA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom