Kwa wana JF wote

Audax

JF-Expert Member
Mar 4, 2009
442
12
Napenda Kuchukua fursa hii kuwatakia wote sikukuu njema ya Noel na mwaka mpya 2011.

Nachukua fursa hii pia kuomba msamaha kwa wale wote ambao niliwakosea katika mwaka huu kwa njia moja au nyingine wote tusameheane.

Nawashukuru kwa jitihada zenu za kuelimisha jamii kupitia website hii. Hii ni pamoja na kufichua maovu na kuwa wawazi-hakiki hatua hii inastaili pongezi nyingi. Nawapongezeni kwa dhati kwa hatua hii muhimu tuliyofikia hasa katika suala zima la kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu, wizi wa mali ya ummma , kuelimishana kwa mambo ya maisha na mengine mengi.

Kwa wale mliojiunga hivi karibuni, karibuni saana.Kumbuka michango yenu inasomwa sehemu mbali mbali duniani, hivyo hamna budi kuchangia kwa mtazamo wa kujenga.

Katika kila mwaka kuna malengo tunajiwekea, Kwa upande wangu nashukuru mungu nimefanikiwa na kwa yote niliyojiwekea. Lakini hata kama hukufanikiwa au hukuyatimiza, ucfe moyo maana tunajifunza kutokana na makosa. Kumbuka wakati ni mali, ukiamua unaweza.Jipange upya ili mwaka ukianza tuanze na utekelezaji.

Tusisahau ya kuwa maendeleo yapo mikononi mwetu, hii ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii na kutimiza wajibu wako popote ulipo.

Ni hayo tu. Mungu awajalie afya njema na msheherekee kwa amani.
 
well noticed mkuu..... thnx a lot
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom