Kwa wana JF wote, tuisaidie bodi ya mikopo kukusanya mikopo

greenstar

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
390
53
RAI yangu kwa Wana JF wote ambao tumenufaika na mikopo tujitokeze kwa wingi kulipa mikopo tuliyoipa vyuoni ili wadogo zetu waweze kusoma bila migomo isiyokuwa na maana.Nimefanya tafiti nyingi kutafuta sababu za migomo nikagundua BODI imeishiwa uwezo wakuwalipa wanafunzi mikopo kama walivyopangilia kutokana ufinyu wa bajeti kutoka serikalilni.

Kulipa mikopo itasaidia kujenga kizazi kipya cha wasomi ambao wataipenda nchi yetu na kuitumikia kwa dhati la sivyo tunaandaa tanabaka la wahuni na wezi kwa vile hawapata haki yao ya msingi kusoma na kujiimarisha kitaluma.Tanzania ya leo,si ya miaka mitano ijayo.Kutakuwa na wimbi kubwa la uharifu kutokana na ongezeko kubwa la vijana wasiokuwa na kazi wala makazi ya kudumu!

Mabadiliko hayo hayatokani na siasa uchwara bali ni hujuma ya Watanzania wenyewe kutolipa mikopo na ongezeko kubwa la wanaokwepa kulipa kodi hususani wafanyabishara wajanjawajanja......

Migomo haitaisha vyuoni hadi pale tutakapokuwa waelewa na watiifu katika kulipa mikopo na kodi zetu kwa wakati mwafaka ili kuwawezesha wanafunzu vyuoni wapate fedha kwa wakati....Pia maadili yafundishwe ngazi ya SEKONDARI kujenga utii katika kazi za serikali na sekta binafsi.

Mungu Ibariki Tanzania!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
mmmh, shida sio bajeti ni vipaumbele!
Tulipe tu lakini haimaanishi walewanaonyimwa mikopo (ambao hasa ndio uwezo wao ni mdogo kumudu gharama za vyuo) kuwa watapata! nionavyo mimi kwa 'trend' ilivyo sasa, zitatafunwa tu kama zileeeee... za Ep......, au watapewa watoto wa wazito!
Usiitupe p,se!
 
Oh ok

Sasa nadhani kuna watu tunaanza kujenga uzalendo humu kitu ambacho nimekipenda sana apart from criticizing on every situations facing government and it's institutions sasa hili ni jambo la kawaida Kabisa kwa kila Mtanzania awe na wajibu wa kujua jukumu na wajibu wake kitu ambacho sasa hivi hakipo badala yake sote tumekua victims of politics.

Nadhani hapa ni suala la bodi ya mikopo kuwa wabunifu wa kutumia system ambayo itaiwezesha kujua taarifa za wahitimu wote wa vyuo mahali walipo na employment status Yao Baada ya kumaliza chuo.

Pili lazima wa syncronize na makampuni yote ya Ndani ya Tz na iwe ni sharti kudeclare your credit status before employment na wawe na well centralized system Ambayo itawaalart kuwa ID number Fulani imeajiriwa sehemu X or Y na after a certain grace period wanaanza kukata refund .

Nadhani bila ya msaada wa system na database nzuri itaendelea kuwa Takrima na kuwa vituko tu na lawama....

Tatu with the invent of National ID nadhani this issue will be history Kama wakijipanga vizuri na national database ikiwa nzuri and CENTRALISED
 
Duu! Nikifikiria nilivyoteseka kupata huo mkopo, nimepigwa sana virungu, mabomu ya machozi kufuatilia huo mkopo!
 
Duu! Nikifikiria nilivyoteseka kupata huo mkopo, nimepigwa sana virungu, mabomu ya machozi kufuatilia huo mkopo!
Kama ni hivyo basi mlishamalizana, hawakudai na wewe huwadai si ndio!?
 
In the name of father son and holy spirit ctalipa hadi pesa walizokwapua warudishe those HESLB moles ndo ntarudisha........otherwise they wil hang me alive!
 
For you info, bodi yenyewe ndo wazembe, kwa nini hakuna mfumo mzuri wa kukusanya hiyo mikopo?
Yanaendesha bodi ki-kanjanja mno!
Afu, kwa nini nilipe mkopo wakati kina jitu patel wamechota maela na wameachiwa huru?
Dowans, IPTL, Aggreko, etc.
Bodi wakamwambie jk na riz1 watulipie madeni. Sisi hatulipi.
 
Back
Top Bottom