kwa wamiliki wa maduka ya rejareja

Kuku wa Kabanga

JF-Expert Member
Oct 28, 2009
807
366
habari wakuu
mimi ni mgeni kwenye hih biashara,nataka kujua wazoefu wanahandle vipi wateja wanaopenda kukopa,hasa maeneo ya uswazi.
 
mikopo ni jambo la kawaida kwenye biashara kama yako! Ila ninachojua kila mkopo lazima ujulikane utalipwa lini?
 
Kabla ya kumkopesha mteja ni muhimu ujue kwanza chanzo chake cha mapato. Kwa walioajiriwa mara kwa mara wanalipa mwisho wa mwezi. Kwa wengine, ongea nao ujue watalipaje.

Anza kukopesha kidogo kidogo huku ukipima uaminifu wa mteja, wasumbufu unaanza kuachana nao na waaminifu unawatia moyo kukopa ili waendelee kuwa wateja wako. Hapo ni muhimu uwe na register nzuri ya wakopaji wako.

Kwa maduka ya uswazi mikopo haiepukiki, la sivyo utakosa wateja wengi.
 
mkopo lazima ukopeshe lakini kuna wateja anaanza kukopa kidogo kidogo mwisho anakuja kukopa deni kubwa anaanza kukusumbua.mimi mtu nikisha gundua ni mtata namtgesea akope deni lisilozidi elfu moja na simdai na huo ndo ukuta kwake.
 
weee ukikopesha lazima ulipwe pesa na sio mapenzi.maana mtu ukimkopesha anataka akulipe mapenzi ndo hapo mwisho wa kukufilisha.
Sikiliza kazi yangu ya dukani by Dogo mfaume...
 
Achana na biashara ya kukopesha rafiki yangu,,hakika utarudi nyuma,nimeshaexperience hiyo kitu wakati naimport laptops last 2 years kuna watu mpaka sasa hawajanilipa na wamesahau kuwa nawadai,that was a mistake i learned xo kama mtaji wako ni wa kuungaunga ucikopeshe,ni bora one bird on hand than a thousand birds on a tree.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom