The Dude
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 1,029
- 453
.....umenikumbusha forest dahhhh!! Natamani maisha ya yale yarudi.
Halafu kwene fellowship mlikua mnajileta kwa wingi ikifanyika kwetu,unakumbuka aza jangwa ya tycs na ukwata?
.....umenikumbusha forest dahhhh!! Natamani maisha ya yale yarudi.
........Yeah, mie nilkuwa azajangwa ya ukwata. Umenikumbusha mbali sanaaaaaa!!Halafu kwene fellowship mlikua mnajileta kwa wingi ikifanyika kwetu,unakumbuka aza jangwa ya tycs na ukwata?
....sijui ulikuwa mwaka gani azania, miaka niliyokuwa mie jangwani vidume vya azania vilikuwa vinajigonga sana kwa wasichana wa jangwani......hadi kula chipsi walikuwa wanakuja kula jangwani kwa Z ilimradi wapate kampani ya wasichana.
Azania wachumba.
Wagumu walikua TA (Tambaza), ASS (Azania Soma Sana) walikuwa mabishoo.
daaah Azaboy, mie namkumbuka yule jamaa aliyekua anauza karanga kwa kupima na kisoda! Sijui alikua anatuwekea nini kwenye karanga zake...ni lazima kila day ujisikie kuzionja tuuuu
mwl kwayu, na yule wa siasa
Huo ni wivu na roho mbaya,unajifanya hujui kuwa Azania sekondari ilikuwa special school kwa wavulana katika mkoa wa Dar.Ngoja nikukumbushe na kama unabisha kamuulize Kapuya au Mungai mawaziriwetu wa elimu enzi hizo.kwa wasichana walikuwa majirani zetu wa Jangwani.Ili uende Azaboys ulitakiwa kupata maksi 120/150.Sasa nakutajia special nyingine Tanzania kwa enzi hizo.kwa wavulana,Ilboru,Mzumbe,Kibaha,Mkwawa,Tanga technical na Tabora boys.Kwa wasichana,Msalato na Tabora girls.Hizo shule nilizotaja ilikuwa huchaguliwi mpaka upate maksi 140/150 au zaidi.Je una hoja?
Unamzungumzia mr yengela?Yule alikuwa tungi ol the time..afu akija na demu sie tunapanda ghorofani kuchungulia akipiga game daah!!
....sijui ulikuwa mwaka gani azania, miaka niliyokuwa mie jangwani vidume vya azania vilikuwa vinajigonga sana kwa wasichana wa jangwani......hadi kula chipsi walikuwa wanakuja kula jangwani kwa Z ilimradi wapate kampani ya wasichana.
Nimeshangazwa sana na comment yako uliyoandika,nani hajui heshima na historia ya Azania sekondari?Hebu tuambie shule uliosoma wewe inaitwaje?Ha! unasema Azania ....?watakucheka watu.
wachumba na mashemeji nawamisije!
wachumba na mashemeji nawamisije!
halafu walikuwa hawapiti geti lao. Lazima waingilie geti la jangwani washangae visketi ndio waende kwao. Lol. Bora sahivi wamewekewa ukuta wa kuwatenganisha na jangwani.
Siamini kama ulisoma jangwani husninyo daaaaah!!Ukute nlishawahi kudate naww..
sio kweli hata kidogo Azania hatukuwa mabishoo na kama tungekuwa mabishoo tusingeletewa Discipline master mkali mpaka akawa maarufu Dar es salaam yote namaanisha Mchwampaka.Walichotuzidi Tambaza ni kwamba walikuwa wanaweza kuanzisha vurugu sehemu yoyote na hadi kusabasha kumuua mtu. Unakumbuka walivyomuua yule kondakta wa daladala mwaka 1994.Huo ndio ulikuwa mwisho wa o'level Tambaza,tukabaki vidume sisi tu Azaboys.Walizidisha sana ndumu wale.
Get your story straight ile vagi ilikuwa 1993, hakukuwa na Tambaza Boys 1994. Mchwampaka alikuwa maarufu kwasababu ya ukali na sura yake...(unakumbuka neno u...wa paka?). Sababu kubwa ya kusamaratishwa kwa TA boys ilitokana na kuvunjwa kwa ukuta wa Muhimbili primary ambao ulijengwa ili kutenganisha shule hizo mbili kwa kisingizio cha kulinda watoto wa primary.
Wanafunzi wa TA walikasirika kwasababu walikuwa wanaenda muhimbili primary kucheza basketball (kwasababu kiwanja cha Tambaza kilikuwa cha udongo) ndipo walipoamua kuuvunja. Vigogo waliokuwa na watoto wao pale wakaamua kuifunga shule yetu mwezi July 1993 shule ilipofunguliwa (Oct 1993) walimu wote wa Tambaza wakawa wamehamishwa na baadae (1994) wakawasambaratisha wanafunzi nchi nzima.
All in all Tambaza ilikuwa ni shule nzuri yenye vifa vya maabara kuliko shule yoyote Tanzania na ilikuwa na walimu wazuri wanaofundisha tofauti na Azania ambapo walimu walikuwa hawafundishi kabisa yaani wanafunzi wanaakaa siku nzima bila hata ya mwalimu mmoja kuingia darasani. Miaka ya themanini wanafunzi wa mzizima na Shaban Robert walikuwa wanakuja kufanya practical za London GCE Tambaza kwasababu kulikuwa na vifaa vya uhakika.