Kajuni
JF-Expert Member
- May 27, 2009
- 486
- 186
Mimi ninae rafiki yangu mzungu (mjerumani) anishi Berlin. Rafiki yangu huyu ameolewa na jamaa kutoka magharibi mwa Uganda (Mbarara). Kwa bahati huyu rafiki yangu wa kizungu alipata mimba na kujifugua mtoto wa kiume (Fini Mugisha).
Siku moja tukiwa home kwao akaja kaka wa huyu mzungu pamoja na mkewe kumpa hongera ya kujifungua. Basi kilichonishangaza ni pale yule mwanamke wa kizungu wa huyo jamaa alipo mwambia mmewe kwamba ana mwonea wivu wifi yake kwa kuzaa na mwafrika kwani nae pia ilikuwa ni ndoto yake na alitamani siku za nyuma kama angepata bahati hiyo..... Je tulio kwenye ndoa hii ina leta picha gani? tunaweza kuvumilia pale wenzetu watakapo tueleza ndoto zao za nyuma?