kwa walio na ndoa tu......!!!!!!!

achana na tabia za unafiki eti" darling,....sweet,......i miss u. Ndoa yangu ina miaka 9, kila mtu yupo bize kuleta fedha ndani. Nimefunga ndoa ya serikali tumetumia kama laki moja tu, Zaidi ya hapo ni kuingia katika madeni. Ndoa ni makubaliano ya mke na mume, ila jitahidi uoe mke sio mrembo, utajuta
 
dah hongera sana! unafikiri ubize wenu ndio uliowafikisha hapo? au mnachokileta ndio kimekuwa msingi wenu? au kuacha hayo maneno ya kinafiki ndio imekuwa kinga ya ndoa yenu? au kwa sababu ndoa yenu ya kiselikali..? je unazani mrembo sii mtu wa kujenga nae familia? nipe kimekusaidia nini mpaka hapo ulipo,???
 
Mdogo wangu kama ulivyoambiwa mwanzo ndoa hhuwa haina formular. mimi ndoa yangu ina miaka minne nilianza kwa kufuata formular kutokana na kwamba nilikuwa nasoma sana makala za shaluwa kwenye web ya shigongo. nikawa nafuatilizia kila kitu. tulikuwa tunagombana sana na ke wangu coz kila nilichokisoma nuilienda kukifanyiia kazi kwa mke wangu.
jambo la maana kwako jaribu kujiweka katika nafasi nyuma ya mkeo. yaani kila jambo mpe mkeo kipaumbele, msifie kila mara hata pale ambapo unajua hakufanya vizuri tafuta tu pointi moja umsifie ili ajiione anapendwa na anakubalika. jambo lingine ambalo ndilo la muhimu kuliko yoote jenga uhusiano na MUNGU wako kama wewe ni mkristo kama mimi jitahidi usali pamoja na mkeo, na kuwa mstari wa mbele kwenda kanisani, kama wewe ni mwislamu vilevile. mleteee zawadi mkeo kila mara mara 2 ama 3 kwa wiki hivi. sio lazima zawadi kubwa hata kama ni pipi, chokolate ama chochote ili mraddi tu ajue kuwa unapokuwa mbali na yeye huwa unamkumbuka. kama wewe ni mfanyakazi ukisafiri usirudi bila zawadi ya kueleweka kama nguo, kitambaa, viatu ,mkoba na chochote kile utakachoone. katika siku yako tenga muda wa kukaa na mkeo mkiwa wawili kabla ya kulala. na wanawake maranyingi wanapenda kufanya mapenzi mchana na asubuhi kuliko usiku maana usiku wanakuwa wamechoka kwa kazi nyingi za mchana kutwa na wanahitaji pumnziko so epuka kudai unyumba muda mfupi tu baada ya kwenda kulala. pia muone mkeo ndo mwanamke pekeee mzuri duniani tena msifie mara kwa mara kwa uzuri alionao na ukiwa unasema hayo mwangalie usoni usiseme ukiwa umeficha uso ataona unamdanganya. pia wakati wa mamboz wanaume wengi akimaliza tu anageukia upande wa pili, hiyo ni sumu ya penzi mwanamke anapenda kukumbatiwa mara mmalizapo mambo yenu kwani hujiihisi kuwa hana thamani tena baada ya kukupa uroda so kulifuta hilo just endelea kumkumbatia kwa dakika 15 hivi baada ya kuwa mmemaliza kupeana shughuli. nawatakia ndoa njema
 
habari za hapa wanajamii...?? nigependa nipate ushauri kwa walio ndani yandoa tu, maana mii natarajia kiungia ndani ya ndoa !.. hasa wale ambao ndoa zao zinaumri wa miaka 10 na zaidi. ni kitu gani kimewasaidia kudumisha ndoa zao...? na niyapi yakuzingatia ukiwa ndani ya ndoa..? nawakaribisheni sana...!!
INGIA TU BEST MENGINE YANAJIEST HUMO HUMO kuna vitu wenzio tunafanya ambavyo kabla ya kuoa au kuolewa tulikuwa tunabisha hatuwezi kufanya !so ndoa its an experience of its own,huwa ndoa hazifanani kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!kila mtu ana yake!ukiiga mi nnayofanya kwenye ndoa yangu kwako yanaweza yasifanye kazi.au yakafanya kazi so we nenda ukatengeneze taasisi yako wenyewe na mkeo,and utaona raha yake!ila policy ni moja ndoa inaweza kujengwa na vitu minor sana na ikavunjwa na vitu minor hivo hivo so TAKE CARE
ALL THE BEST BOTHER!
 
[QUOTE= asante sana na hongera kwa kuweza kuifikisha ndoa yako umri huo.! na huwa nadhamini sana ushari wenu, najisikia kuwa niko na mawazo yenu mda wote. asante na siku njema.
 
SHUKURA WANAJAMII WOTE KWA USHAURI WENU..! mawazo yenu mda wenu mlio tumia kunishauri ni muhim sana sina uwezo wa kuwalipa isipokuwa shukurani. wote mlio nishauri na kunitahazarisha. nawaahidi sitawaangusha nitachukuwa mema na mabaya yatabaki hapahapa. najivunia kuwa na nyinyi. maana hata mke mtarajiwa nae amepatika hapahapa. karibuni wote, nawatakia siku njema.
 
Kila mmoja awe tayari kuyavumilia mapungufu ya mwenzi wake... By the way mbona hujatuambia huyo bi dada ni nani nae tumpe hongera zake? Kila la heri mkuu..
 
mawasiliano, jambo la msingi sana, kama mekwaruzana au mwenzio amekukera au umemkera kwa namna yotote, hakikisha kabla hujatoka asubuh kwenda kwenye mihangaiko yako mmeongea na kufix tatizo hlo.

Sala muhim sana, siku majarib ni mengi kwenye ndoa zetu lazima kumtanguliza Mungu...........................

hongera na Mungu akutangulie, ndoa yako iwe na mafanikio
 
ndoa inajengwa na kumtegemea Mungu kwani ndiye aliyezianzisha, pia wanandoa wenyewe wanapaswa kuidumisha kwa kuoneshana upendo,support ya kihisia na kuheshimiana.nyote wawili mnapaswa kuwa na nia ya kudumisha ndoa yenu, maana ndoa inazaliwa inapaswa kukua.
 
Onja mpiko kwanza, anachotaka mwenzio mpe, alafu uwe unajituma sana mengine ni sacrifice, lowliness nk. Ushauri mwingi wamesha posti wanaJF wengine. Karibu kwenye kifungo
 
Kumbuka ukweli kwa mwanamke ni uongo na Uongo kwake ndo huamini kuwa ni kweli!
Karibu kwenye jahazi ambalo kila leo hukumbwa na misuko suko but safari inaendelea kwa mwendo wa kuvumiliana na kusameheana
 
Back
Top Bottom