Kwa wale wenye chinese phones.

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Simu hizi zinasumbua sana kuzi-configure automatically with internet from various service providers.Usihangaike sana,forexample mimi ninatumia TECNO HD 71 na ilizingua kuunga internet automatically.Nilichofanya ni kutuma maneno yafuatayo kwenda VODA,..WAP NOKIA 5000 KWENDA NAMBA 15300 na mambo yakajipa swafi.Pia nimewasaidia wengi kwa technique hii.Haijalishi ni voda,tigo.airtel etc,unachotakiwa ni kudanganya aina ya simu,andika common brands za simu kama za nokia,samsung,ericson etc na utafanikiwa.
 
angalizo:line utakayotumia kuunga internet iwe haijawahi kutumika kuunga internet hapo kabla,vinginevyo utajibiwa kwamba ulishapewa huduma hii hapo kabla.
 
Hiyo tunajua siku nyingi sana, leo wewe ndio umegundua? Ok kwa wasiojua najua watafaidika.
 
Hiyo tunajua siku nyingi sana, leo wewe ndio umegundua? Ok kwa wasiojua najua watafaidika.

kama unajua ni wewe, usiwe na uchoyo wa tekinolojia, kuna wengine ndio wamenunua simu sasa hivi, itawaidia, usiwe mtu wa kukatisha tamaa wenzio.
 
Hiyo tunajua siku nyingi sana, leo wewe ndio umegundua? Ok kwa wasiojua najua watafaidika.
Hongera mkuu,lakini mimi sijaigundua leo,nimeigundua kitambo sana,ila nimeona niiweke hapa kwa sababu nimesoma malalamiko mengi tu hapaj jf na cha ajabu wewe hukujitokeza kuwapa mbinu mbadala.
 
Sijui hii imekaaje. Tume ya mawasiliano Kenya imetangaza kuzifungia simu zote fake hivi karibuni kupitia service provider. Inakisiwa zaidi ya theluthi moja(33%) za simu KE ni fake. Subiri kishindo muda si mrefu.
 
Hapa Bongo itakuwa vilio kila mtaa, sijui kama mitandao ya simu itakubali kupoteza wateja. Mmnavyojua hapa Bongo **** mitandao ya simu yenye ushawishi kuliko mashirika ya kijamii
 
Back
Top Bottom