Kwa wale wanaokwenda vyuo wazingatie haya

zema21

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
619
251
Vijana wengi wanapopata nafasi za kujiunga na vyuo huwa wanafurahi saana na kuona kuwa wamepiga hatua kubwa saana na pia huwa hawashauriki wakiamini wameshafika mahali ambapo wanaweza kujiamulia mambo na kufanya lolote wanalolitaka.....
Ukienda kutembelea vyuo mbalimbali utasikitika kuwaona baadhi ya mabinti wadogo wakitembea na nguo zinazoacha sehemu kubwa ya miili yao nje(nusu uchi). Pia wavulana/wanaume baadhi huishia kuingia kwenye ulevi na uvutaji wa bangi na mambo mengine machafu..
Pia utashuhudia wengi wao wanawekana kinyumba...

Ushauri wangu kwenu ni kwamba kabla hujafanya maamuzi jitafakari kwanza... fikiri kwa makini, wafikirie ndugu zako, wazazi, walezi, wadogo zako na wengineo.....kisha ndo ufanye maamuzi ya kujiingiza kwenye haya magenge kwani wengi wamejikuta wakiwa wanajutaa mno lakini inakuwa haina maana kwao kwani huwa inakuwa too late kwao.....kwa wale waliokuwepo UDOM 2011 college of education walishuhudia jamaa mmoja akijaribu kujiua kwa hali na mali katika jaribio la kujirusha ghorofani baada ya kujigundua kuwa ameambukizwa HIV na kwa makusudi na binti aliyekuwa mpenzi wake.. Pia yupo jamaa alimwagiwa maji moto usoni na msichana aliyekuwa mpenzi wake lakini kisa cha kumwagiwa maji msichana alikuwa hana mapenzi ya ukweli kwa kijana yule....Tafakari kila njia za mienendo yako ukiwa chuoni..uhakikishe kila unalolitenda halitakuwa na majuto yoyote kwako na jamii yako...kuwa mfano wa kuigwa na jamii badala ya kuwa reference ya maovu....
Kama unataka kuingia katika relation iwe ni mara yako ya kwanza au la kuwa makini saana mchunguze mno unayetaka kuingia naye katika mahusiano...Kumbuka kwenda kupima ukiwa na mwenzi wako......pia kumbua saana kuwa maisha hayajabadilika wala level yako ya undergraduate si ya kukufanya ujisahau ujione kama ndo umesha-win .....
Mtangulize MUNGU katika kila Jambo hudhuria msikitini, kama ni mkristo Fellowship/kanisani usikose....tenga muda wako kufanya mambo ya kijamii pia MWENYE MASIKIO NA ASIKIE
Naomba kuwasilisha
 
Mi nafundisha chuo kikuu wale wanaofika mwaka wa kwanza huwa nawapa onyo na maadili ya kuishi chuoni nillichojifunza makundi yanaawaribu sana,kuna vijana nimesoma nao seminary niliwaacha nyuma sana walivyofika huku useminari uliishia getini wakaona kama walikua mbali na dunia,wazazi wetu wanajinyima sana kutusomesha tena katika mazingira magumu sana ila mwisho wa siku tunawaumiza vibaya kwa matendo yetu,wazazi hawazai mtoto aje kuwa kahaba,teja au apate ukimwi akiwa masomoni,wanapoteza pesa nyingi na nguvu kutafuta ada na pesa za kujikimu kifamilia ili usome uje kuwa na maisha bora na wao wajivunie na kufurahia maendeleo yako ya kuwa na kazi nzuri,uoe au kuolewa katika staha hayo ndo matukio ambayo wazazi wetu wanapenda yatokee kwetu na si kusoma kwa taabu miaka mingi na kupata ukimwi ukiwa mwishoni mwa masomo yako maana mambo yote waliyokufanyia ni sawa na kutupa pesa mtoni au kwenye moto na hii hupelekea wazazi kukata tamaa ya kuwasomesha ndugu zako uliowaacha.
pse vijana wenzangu mlioko vyuoni sasa iwe bhaaaaaaaaaaaaaaaasii!bhaaaaaaaaaassi!
 
i'll be blunt here, nimesoma UDSM na naweza kusema kuna marafiki wa kila aina. walokole, walevi, vicheche, waliotulia kwenye masomo nk wote wapo; its up to you kuchagua. sipendi hii dhana ya kwamba chuo ni kama da.ng.uro au kila aendaye anatafuta mapenzi maana iko general mno na sio ya ukweli.
 
Kwakweli umewashauri vizuri. Mwenye macho ya kusoma na asome!
 
Nimeukubali ushauri wako na nitajitahidi kuutimiza coz mi mwenyewe niko mwaka wa kwanza udsm.Asante kwa ushauri.
 
@Blaine ni kweli kabisa kuwa "si kweli kwamba vyuo ni kama da.ng.uro au kila aendaye anatafuta mapenzi" lakini kuna mengi ya kuhuzunisha tumeyashuhudia. Wengi wanaharibikiwa na wanaharibu future zao kwa kutokujua au wengine huona ni mambo sahisi wanayoyafanya ila ninachotaka kuwakumbusha vijana ni kuwa makini katika mienendo yao na kujitenga na magroup yatakayowaharibia futures zao kuna mengi sana tumeyashuhudia so ni wajibu wetu kuwashauri hawa wadogo zetu/kaka/dada/ na ndugu zetu... Kumbuka wengi wao wana umri kati ya miaka 18-24 so kwakweli bado ni wadogo
 
Nimeukubali ushauri wako na nitajitahidi kuutimiza coz mi mwenyewe niko mwaka wa kwanza udsm.Asante kwa ushauri.

Kashindi all da best katika masomo yako,chuo ni sehemu ya kujifunza na sio sehemu ya kuonyesha ww ni nani,soma kwanza starehe zipo na zitakuwepo mtangulize mungu wako kwa kila jambo na utafanikiwa
 
mkubwa ulilolisema ni la kweli kabisa maana wengi wanafikili kuwa chuo ndo sehemu ya kufanya starehe zote za dunia kitu ambacho si cha kweli nina mfano mmoja, kuna dada nilikuwa naongea nae kuhusu suala zima la mapenzi lakini yeye alilolisema ni kwanba kwa saa hajiusishi na mambo hayo mpaka akifika chuo!! nilimshangaa kweri na kugundua kuwa wengi sana wana amini kuwa chuo ndo sehem ya kufanya mambo hayo.
 
Well done!
Nimependa ushauri wako mkuu, dhana ya fungulia mbwa inawaharibu sana vijana...
 
acheni kuwatisha bure, kuna madanguro kama Tandale uwanja wa fisi?

Huko mnawatahadharisha vipi wanafunzi wanaoishi huko??

Na wakienda makazini je? Hakuna wanaoliwa vyooni?

Asiyefunzwa na mamaye. . .
 
appreciated, lakini kama ulivyosema wengi wao wakifika level hiyo hawapendi kushauriwa........, so hata wakisoma hii post wengi wao watapuuza. Sikio la kufa......
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom