Kwa wale mliosoma kwa mkopo wa Bodi ya Mikopo ya elimu ya Juu Tanzania, Angalieni Tangazo hili

Watanzania mnanishangaza sana, Yaani kupenda vitu vya bure tuuuu.
Sasa msipolipa mnategemea wadogo zenu watasomaje?
Sawa hata kama kuna issues za ufisadi huko kwenye bodi, je unapataje nguvu za kukemea huo ufisadi wakati na wewe mwenyewe ni fisadi( kwa kutokulipa mkopo kwa makusudi).

Na kuna watu hapo juu naona wanahusisha makato ya PAYE na ulipaji wa mikopo. Jamani ivi ni vitu viwili tofauti! kwani wakati unaomba mkopo si uliingia mkataba na ukahaidi kulipa? sasa mambo ya PAYE hapo yanaingiaje?
Ebu acheni izo, rudisheni hela za watu.

Kwa taarifa yenu hata nchi tajiri duniani hawatoi elimu ya juu bure!

Na ninaenda kukagua hayo majina nikikuta ndugu yangu yeyote ambaye hajalipa......... watanitambua.
Waeelezee waelewe hawa, walikopa wenyewe kwa mikono yao leo wanaona matanga kulipa?
 
Bajeti ya posho kwa wabunge inatosha kusomesha watanzania.
Misamaha holela ya kodi kwa makampuni ya madini inatosha kuwasomesha watanzania wote bila kuwakopesha.

Pesa zenu kwani unadhani nasi wazazi wetu walikuwa hawalipi kodi?

Btw, pamoja na kwenda disco lakini shahada tunazo!!
Ndugu Mwita, hapa naona unachanganya vitu viwili tofauti, Mkopo watu walikopa na masharti ya mkopo walisoma sasa hii ishu ya wabunge sijui nini, ni ishu ya kuijadili kipekee ila hapa tujadiili watu kulipa madeni yao ili wadogo zetu wasome!
kama ni ufisadi tu deal na hao mafisadi
 
Watanzania mnanishangaza sana, Yaani kupenda vitu vya bure tuuuu.
Sasa msipolipa mnategemea wadogo zenu watasomaje?
Sawa hata kama kuna issues za ufisadi huko kwenye bodi, je unapataje nguvu za kukemea huo ufisadi wakati na wewe mwenyewe ni fisadi( kwa kutokulipa mkopo kwa makusudi).

Na kuna watu hapo juu naona wanahusisha makato ya PAYE na ulipaji wa mikopo. Jamani ivi ni vitu viwili tofauti! kwani wakati unaomba mkopo si uliingia mkataba na ukahaidi kulipa? sasa mambo ya PAYE hapo yanaingiaje?
Ebu acheni izo, rudisheni hela za watu.

Kwa taarifa yenu hata nchi tajiri duniani hawatoi elimu ya juu bure!

Na ninaenda kukagua hayo majina nikikuta ndugu yangu yeyote ambaye hajalipa......... watanitambua.
kama ukosemeshwa na loan board kaa kimya tunajua tunadaiwa tunajua tuliingia miktaba (binafsi ninazo copy za hiyo miktaba) tunajua tunatakiwa kulipa na tunajua KERO tulizopata mpaka tumegradruate na hiyo bodi ya mikopo issue kubwa kwanza na kero ambayo inaonekana kwa watu ni zimamoto ya bodi ya mikopo .personally lazima nipate FINANCIAL STATEMENT yangu tena kwanza waniwekee hivi kwenye net kama walivyopost jina langu liwe na deni lote na kiasi maana nilienda kukclear chuo kufuatilia vyeti vyangu bursar wachuo ananipa habari tofauti kwamba bodi kuna hela hawajamalizia halafu inaonekana walikuwa wanalipia percent less than ile ambayo nilikuwa nimeeandikiwa loan board niwazima moto sana
halafu hoja ya sisi kulipa ili wadogo zetu wasome hainamashiko uliza nikiasi gani kinadaiwa na bodi toka 1994-2009 . halafu unanishe na na pesa hawa MASHETANI wanazojiongezea POSHO ovyo ovyo ...
kinacho watia hasira watu wengi hasa graduate kwanza ni usumbufu wanaoupata kupata mikopo halafu wakigraduate shuruba wanayoipata kwenye kusaka ajira halafu unamwambia mtu atoe 8% ya msharahara wake alaah kama kusomesha mie nasomesha wadogo zangu inatosha sana kulipa hilo deni nimepunguza mkopaji loan board
halafu hiyo mikwara wanayo ichimba kwenye hilo tangazo wanafikiri tutaogopa ng'o kwame hatuogopi .
halafu wale wasio kwenye formal sector ambao wameamua kujiajiri wenyewe ambao hawajapata ajira watawatrace vipi ?
LOAN BOARD PUNGUZENI ZIMAMOTO KWA SASA HAPANA MPAKA NIONE USAFI FULANI ,ACHENI NIYASIKILIZIE ,ACHUNGU YA PAYE KWANZA DAAH
 
kumbe tulikuwa tunadanganyana hii hela ya bure!!!inakuaje sasa haya mambo!!maanake nakumbuka hata kama unalipiwa na mzazi washkaji wanakushawishi uchukue na mkopo kwakuwa si rahisi kuja kudaiwa kumbe sivyo!nimemind kinyama......
 
We mrembo unaongea kana kwamba hiyo mikopo ya elimu ya juu inakuja na guarantee ya kwamba unapomaliza kazi tu unapata kazi. Unajua watu wangapi ambao tangu wamemaliza mpaka sasa hawajapata kazi na hali ya kuwa wamechukua mikopo loan board?
Serikali imejiandalia mikakati gani ya kuwawezesha beneficiaries wote kulipa mikopo?
Ni kweli waliingia mikataba wao wenyewe ya kulipa mikopo hiyo lakini wanalipaje na kazi hamna? Au hata kama wamejiajiri unadhani vipato vyao vinawawezesha ku service hizo loans?
Hata kwenye mabenki huwa wana criteria zao za kumpa mtu mkopo ila sidhani kama kwa vigezo hivi vya loan board ni sawa kabisa kusema hawa jamaa walipe hali ya kuwa hawana nyenzo.
Think mara saba upate informed judgement before blabbing.
Anyway, that was just a food for thought.
Hali bado tete sana na especially huku tuendako loan board haina budi kujiandaa na bad debts
 
Nimejaribu kuipitia hiyo orodha naona ina mapungufu, kwa maana kuna watu ninawafahamu waliokuwa Private lakini wamewekwa kwenye hiyo orodha kama wanadaiwa na kuna watu (Mimi na wenzangu kadhaa) ambao tulishaanza kulipa siku nyingi lakini bado majina yetu yanaonekana kana kwamba hatujaanza kulipa. Naona walichokifanya ni kubandika majina ya wahitimu kutoka kwenye vyuo husika bila ya kujali kama ulikopa au laa!
Kazi tunayo
UKWELI AWANA DATA,WANATAKA WATU WAJIPELEKE WENYEWE NNA HAKIKA NA HILO kuna zaidi ya miaka 6 wakopaji rekodi zao bodi awana,na pia wanazo nyingi za miaka mingi tu zenye majina mawili na sio matatu. So hapo ndipo kuna kasheshe
 
hilo ni swala la kutoa taarifa tu. Nadhani ukusanyaji wa mikopo ni jambo zuri tu. Iwapo jina lako lipo kimakosa waandikie, na waelezwe kutangaza watu wanadaiwa wakati hawana deni ni kosa pia. Tuwasaidia ili utaratibu uimarike, pesa zikusanywe, zisaidie wengine
 
fedha zetu wenyewe tulipe wenyewe acheni ujinga nyie

Fedha ni za kwetu, lakini ni mfuko endelevu wa kuwezeshana kusoma. Pale unapopata kazi inabidi ulipe, ndio maana hamna interest huko! unakatwa deni lilivyo!
 
UKWELI AWANA DATA,WANATAKA WATU WAJIPELEKE WENYEWE NNA HAKIKA NA HILO kuna zaidi ya miaka 6 wakopaji rekodi zao bodi awana,na pia wanazo nyingi za miaka mingi tu zenye majina mawili na sio matatu. So hapo ndipo kuna kasheshe

Ni kweli data ni pungufu, lakini huu ndio mwanza. Wazalendo tuanze kujenga kasumba tu ya kutimiza wajibu. Kama umekopeshwa rudisha hata kama jina lako halimo. Labda, makazini waanze kuomba certificate of loan status!
 
Mimi sioni mantiki ya kulipa ilhali mwezi wa saba mwaka 2011 bunge la Jamhuri lilipitisha sheria ya makato ya kodi ya Skills and Development Levy (SDL) 4% kati ya 6% ya mishahara ya wafanyakati kwenda Bodi ya Mikopo. Swali kama wafanyakazi tunakatwa 4% kwenda kwenye Bodi ya mikopo je ni kwa nini mtudai teha ilihali tunaichangia bodi?, nafikiri wadau wengine ambao si wafanyakazi wangelipa na si kwa wafanyakazi.

Nawasilisha..
 
Back
Top Bottom