Special agent.
Senior Member
- Aug 25, 2015
- 101
- 71
Duh? Mimi siamini kampuni za kibongo hata kidogo,hadi leo walioweka Pesa zao DECI zimepotea hawajalipwa,vp kuhusu hii Rifaro Africa? Hapana hii ni DECI nyingine.
Hii kampuni inajihusisha na uuzaji wa muda wa maongezi kwa njia ya kielectroniki kwa wateja wa mitandao yote.Wanasema changamkia fursa,simu yako jembe lako.Sasa wanachofanya wao ni kwamba wameeliminate superdealer,agent na retailers na kukuweka wewe kama ukijiunga nao ili ununue kutoka kampuni moja kwa moja na kumuuzia mteja.
Kwa hiyo wewe sasa ndio unakua unalipwa commission ambayo wangetakiwa walipwe hao watu uliowaeliminate.Malipo yao ni kwa week kila jumatano na tarehe 5 ya kila mwezi.Ukimuunganisha mtu akawa anatoa hiyo huduma utalipwa 20,000 nae akamuunganisha mwingine utalipwa 8000 na akimuunganisha mwingine utalipwa 5000,mwingine tena 3000 mpaka 2000.
Mtoa semina wake sasa jamaa wa kikenya anajua kuhamasisha balaa,anaongea ukweli sema anatoa ukweli nusu ili kuaminisha watu kua Mo Dewji utajiri wake unatokana na u-superdealer alionao wa vocha za voda, hapa ndio nikaona huyu jamaa yuko hapa kutapeli tu watu kwanini asiseme ukweli halisi?
Na cha mwisho sasa eti unahitaji kuwalipa 128,500 ili wakuunganishe uwe unaweza kuuza na kununua vocha kwa njia hii!!!Yani utajiri wote wanaoongelea upatikane hivi?Labda waseme wao ndio watapata utajiri ila sio wewe mteja wao.
Nimepata wasiwasi nao kusema na ukweli.Nitaendelea kuaminu kua kwenye utajiri kamwe watu hawaalikani na kutoleana siri kama hivi.
KUNA MTU KULE FACEBOOK WALL YAKE ALIANDIKA HIVI.
Network Marketing, mfumo wa kibiashara wa Kipyramid, athari zake kwa Nchi masikini hauna kipimo:
1)Baadhi ya Makampuni Hayaruhusu mtu kuwa na duka la bidhaa zao, bali unaruhusiwa kuwa mchuuzi, kutembezatembeza kama machinga
2) Vijana wengi wameacha Professions zao kama vile Udaktari, Ualimu, Uinjinia na kujikuta wakiwa busy kutengeneza Network zao,Matokeo yake Taifa lililoinvest mabilioni kuwatrain hawa watu likiwa halinufaiki nao, hii inafanya Taifa hilo liendelee kuwa tegemezi kwa Wataalam wa nje
3) Ni njia ya kijanja sana ya kujenga Monopoly, Makampuni mengi hutarget vijana wenye elimu na ambao wanakipato fulanifulani, Unapowaingiza hawa watu katika Network ni sawasawa na Unewabatiza au umewafanya kuwa wanachama, Hawa watakuwa loyal kwa network husika, na wataendelea kurecruit watu katika network hiyo na kuendelea kusambaza " Habari njema" ya products husika.
4) Ni pyramid Scheme ambayo eventually itacollapse, NI KWELI Wajanja waliowahi na kuingia mapema WANAPIGA HELA, ila tatizo ni vijana waliomaliza chuo wanaokuja katika link ya chini katika chain. Rate ya recruitment inadecrease kwa sababu market iko saturated, Je Commision za kuwalipa zitatoka wapi kama hakuna new recruits?, Eventually ina collapse!
5) Ni kweli wanalipa kodi serikalini, lakini kodi wanayolipa ni ndogo kuliko wanayokwepa!. Hakuna namna ambavyo Commision ya kila member inavyokuwa Taxed, kwa sababu wanavyolipana ni ngumu kutrace.
USHAURI WANGU
Vijana msitake utajiri wa "kiexponential", Tengenezeni utajiri kwa kutoa huduma na Kuzalisha, hii ya Kusubiri kulipwa kutokana na Kiingilio cha wanachama wapya katika chain yako ni kula pesa bila kuzalisha, na mimi binafsi nadhani ni Morally wrong!