kwa wakaka wa kitanzania tu

Maisha kujipanga kweli. Japo umewaponda sana ila wamekuelewa.

We binadamu upo? nina kama wiki sijakutia machoni, well ujumbe umefika ila kiukweli hata wadada magari mnayoendesha kadi zipo kwa waliowapa magari siku ukiwa goigoi kwenye kutoa huduma unanyang'anywa gari unarudi kwenye daladala!

Sasa sijui yule wa kukopa na wa kuhongwa yupi yupo juu..........
 
maisha ya sasahivi yamejaa maigizo mwanzo mwisho.watu wanakufa na tai zao shingoni,ni pale inapofika mwisho wa mwezi na kukuta salio chini ya laki na nusu.mjini sasahivi kuishi kunahitaji akili nyingi sana na kujikubali mwenyewe.lakini ukitafuta gari ili uonekane mambo mazuri wakati linakuzuia kuendelea unajirudisha nyuma bila kujua
 
Smile ww! uko sawa lkn si unajua thamani ya nyumba na gari? mwenye gari anaonekana kuliko mwenye nyumba! mi naona ni maamuzi ya mtu,na ni ushauri mzuri!
 
Huyo ndo Smile bana,talking straight always,wape vidonge vyao,njiani ana mkoko,simu blacberry torch,kapanga na apartment mbezi,kijijini baba na mama yake ili asome waliuza ng'ombe,mbuzi hadi kuku pale kibaigwa nyumba yao imeezekwa kwa tope.
 
Hivi mwanamke anaekupenda anaweza kukubali kuona unadhalilika hapa mjini kwa ajili ya starehe kweli?
Mwanamke anaekupenda kweli lazima atakubali kukuvumilia na kukubali kusaidiana na wewe katika matatizo pia atakushauri kuhusumaisha. Ila kwa sababu mnapenda mauzo ndo ivo wanawake nao wanachungulia wallet wanokomba kilichopo wanawakimbia…utajijuna madeni yako
Na cha kusikitisha hata wanapokula na kupanda hayo magariyenu tunajua ni mkopo mtupu na tunajua unawasumbua na kuwapa pressure
Lakini kwa vile mmeamua kufa pressure kwa ajili yetutunashukuru
Ila mimi nimewaambiatu vile nawapenda hapa
''You never know with women''
 
jamani kwani hizo nauli za daladala ukizichanga haifiki hio hela ya mkopo wa gari???....mie najifunza driving sasa hivi na nikimaliza tu nanunua gari,sijali sina nyumba wala nini...maisha ni kuchagua kama kupo kwa kulala kunakucha shida ya nini? lol
 
Mkopo hutaki tena?
 
hapa umenena...kero za daladala hazivumiliki!!
 
Wao za kwao ni Salon, kujilemba, na kwenda kupeleka pesa upande wa wazazi wake halafu Mwanamume ufanye kazi ya kuligharamia janamke zima lenye kipato chake.

90% mkorogo na ulimbwende mwingine, 10% viwalo, mahitaji mengine yataji-solve yenyewe...
 
Asante bi dada Smile! Wazo zuri, hawa wakaka wanafikiri kuwa Na gari ndo kupendwa, kumbe wanapata vimeo tu.
 
Back
Top Bottom