Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Mipango. Matahalani mie nilikuwa namsaka mtaalamu wa kufundisha ufugaji wa kisasa kwa kuku hawa kienyeji. Nimewasiliana na wadau wa Breakthrough business support kwa muda wamekuwa wakitoa sababu lukuki za kutopatikana na hatimaye hivi sasa hawapokei simu yangu! Maribuni na nyie wenzangu 0656 004001 ama 0656 004002.

Naomaba atafutwe mtaalamu atengeneze Darasa la weekend moja. Tuko tayari kumlipa!
Kwa anayetaka jinsi ya kufuga kuku wa nyama wa kisasa kwa kutumia gharama nafuu au project ya ufugaji wa kuku wa kienyeji (hii sijaifanyia kazi ila niliiandika) tuwasiliane thru funzadume@yahoo.com nitamsaidia jinsi ya kuwatunza na formula ya kutengeneza chakula.
 
Funzadume

NI vizuri ukaweka hiyo Elimu uliyoiandika kuhusu ufugaji wa Kuku ili utusaidie na sisi tuweze kupata Elimu hiyo kwani itatusaidia na sisis tuweze kufuga Kuku kama njia ya Kujiongezea Kipato . Si unajua tena Kipato cha Bongo ni Kidogo.

Please Tusaidie wan JF wenzako
 
Kitu cha kwanza kinachotakiwa uwe nancho ni determination, bila hilo hata kama utapata elimu ya ufugaji haitokusaidia kitu, kwa mfano hivi kuku wa kienyeji anahitaji elimu gani ya ufugaji?

Na ukiamua kufuga kuku wa kisasa kila wasambazaji wa vifaranga wana maelekezo ya ufugaji bora, kwa mfano ukifika waambie unataka kufuga kuku 500 na wewe ndiyo unaanza, wao watakupa mshauri wao ambaye ataku guide wewe kuanzia kibanda chako, ulishaji nk mpaka kuku wako watakaponza kutaga.
 
Elnino; kunahitajika elimu na hata hao guides ndio walimu wenyewe; kwenye huu ufugaji wa kienyeji kuna njia ya kisasa inatumika kuleta tija; mie nimefuatilia kupiatia vipeperushi lakini nilihitaji zaidi kupata mdau anayefanya shughuli hii nikajifunza kwa vitendo! Hivyo kama una nyanga zimwage hapa mkuu watu wachote kisimani!
 
Maskini Jeuri nimekusikia, mimi nafuga wa kisasa lakini nitafute Jtatu kuna sehemu naenda Jmosi kuangalia mashine ya kuangulia mayai ya kienyeji inayotumia mafuta ya taa - nikiipata pamoja na maelekezo yake nitakujulisha kwani hiyo itafaa sana kwa ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa njia ya kisasa.

Navyojua mimi kuku wa kienyeji wana kinga kubwa ya magonjwa (Immunity) kulinganisha na hawa wa kisasa kwa hiyo kuwafuga wa kienyeji ni kazi rahisi mno kwani ugonjwa wao mkubwa ni mdondo ambao una chanjo yake.

Umeshaanda business plan? PM kwangu nikupe ushauri.
 
Heshima kwako Mkuu.

Kiukweli ni kuwa hakuna utafiti wowote uliwahi kuonyesha kuwa kuku wa kienyeji wanaresist mdondo kuliko wa kisasa. Kinachotokea ni kuwepo kwa 'selection' katika population yao, kwa maana kuwa ugonjwa huu unapotokea huua kati ya asilimia 95-100 ya kuku wote. Endapo wataponea (pengine hawa 5%), huwa wamedevelop active immunity, na ugonjwa ukija tena hawaathiriki. (hii inaweza hata kutokea kwa kuku wa kisasa). Hata hivyo immunity hii hurithiwa na vifaranga lakini hudumu kwa wiki 3 tu baada ya kuanguliwa.

Hivyo kuku wa kienyeji wanahitaji chanjo ya mdondo (kideri), kila baada ya miezi mitatu. Kwa wanaweza kuwa na cold facilities, wanaweza kutumia chanjo ya La sota au I-2. Lakini kama huwezi pata friji, basi unashauriwa kutumia I-2 peke yake ambayo inaweza kutunzwa katika joto la kawaida kwa siku hadi 30.

Pamoja na mdondo, kuku wa kienyeji ni wahanga wakubwa wa magonjwa kama coccidiosis, fowl pox (ndui), na magonjwa ya kuhara (enteric bacterial infections). Pia wanasumbuliwa sana na minyoo, na upungufu wa vitamini A, hasa wakati wa kiangazi (dalili yake ikiwa ni macho kuvimba na kupofuka). Viroboto (hasa wa machoni) ni tatizo ambalo pia linahitaji uangalizi wa karibu kwani linapelea apotevu mkubwa kwa kuku hawa. Tatizo ambalo linasababisha upotevu wa vifaranga kwa zaidi ya 50% kwa kuku wa kienyeji ni wanyama na ndege wala kuku (predators). Kwa hiyo ujenzi wa banda na matunzo ya vifaranga yazingatie kuwaepusha na haya hasa katika wiki 6 za kwanza.

Uangulishaji mayai ama kwa kuku wenyewe au kwa mashine, hutegemea ubora wa mayai. Ubora huu hutegemea matunzo mazuri ya mayai. Hivyo mfugaji anapaswa kuhifandi mayai sehemu yenye hewa, kuhakikisha sehemu ya yai yenye hewa (ncha nene), inageuziwa juu daima, kutoruhu maji au unyevu kwenye mayai, na kuhakiksha kuwa mayai yanahifadhiwa bila kubebana (yai lisiwe juu ya jingine).

Matunzo sahihi ya chakula, dawa, virutubisho na nyumba, tanahitajika kwa mkazo tofauti katika makundi makubwa matatu ya kuku; yaani vifaranga, wanaokua na wakubwa.

Kwa wale ambao watahitaji kwa undani zaidi wanaweza kuwasiliana nami na kama watakuwa na chance ya kupita Morogoro, mitawapatia copy ya kitabu cha mwongozo cha "MISINGI YA UFUGAJI WA KUKU WA ASILI", kinachotolewa hapa chuoni...
 
Mkuu, hauwezi kuwa na soft copy ukatuwekea hapa mzeei? THANX!
 
Mipango matahalani mie nilikuwa namsaka mtaalamu wa kufundisha ufugaji wa kisasa kwa kuku hawa kienyeji............nimewasiliana na wadau wa Breakthrough business support kwa muda wamekuwa wakitoa sababu lukuki za kutopatikana na hatimaye hivi sasa hawapokei simu yangu!. Jaribuni na nyie wenzangu 0656 004001 ama 0656 004002

Naomaba atafutwe mtaalamu atengeneze Darasa la weekend moja. Tuko tayari kumlipa!

Mkuu hao breakthrough business support si walikuwa wanaendesha semina pale Millenium Tower? Kuna wakati niliona kipeperushi chao au ndio walikuwa wasanii tu?
 
Mkuu hao breakthrough business support si walikuwa wanaendesha semina pale Millenium Tower? Kuna wakati niliona kipeperushi chao au ndio walikuwa wasanii tu?

Haya sasa kazi kwetu weye ulipewa address ya Millenium Towers. Mimi nimepewa address ya Tandale! Dah:whistle:

Lakini sisi wenye nia tutafika tu!

Shukrani kwa Elnino kashajitolea hapa kuna nyanga za kutosha kuanzia!
 
Mr Tuko asante kwa ujumbe, Mimi ni mfugaji wa kuku wa mayai nilianza kufuga as a hobby 2008 July ili niwe busy hasa siku za weekend lakini production imezidi kiasi sasa nimeajiri vijana 4, uzalishaji ni tray karibia 100 kwa siku - ukweli biashara hii imenirudishia pesa zangu zote na sasa inaingiza kipato kiasi ambacho hata sikutegemea siku za mwanzo wakati nabuni business plan.

Project imepanuka kiasi sasa inabidi isajiriwe kama kampuni kamili mwakani - hapa lazima nitangaze ajira kwa bwana mifugo kama wawili hivi mmoja kwenye uchanganyaji wa chakula na mwingine kwenye magonjwa.

Kwa sasa mkuu wapo kuku 3000 wenye afya nzuri kabisa - na wengine wadogo 2000. Uchanganyaji wa chakula ni kitu muhimu sana kwani chakula ndicho kinatengeneza kinga ya kuku na prodution kuwa juu. kwa mfano sasa hivi nahitaji tani 6 kuwalisha kwa siku 14 tu kwa hiyo hapo unaweza kugundua mzigo uliopo.

Sijawahi kuhudhuria semina wala mafunzo yoyote ya ufugaji mimi nachofanya kama hobby yangu tu, kuna wakati daktari akikushauri na wewe changanya na uzoefu na akili zako mwenyewe ili kumaliza tatizo lililopo. Kuna mifano mingi ninayo ambayo bila kutumia reasoning yangu hii project ningeifunga.

Kwa hiyo rafiki yangu Maskini Jeuri kama kweli unaipenda kazi ya ufugaji as a hobby basi utafanikiwa sana, hii ndiyo siri ya mafanikio.
 
Kaka el-nino mie pia huwa na interest na ufugaji nikiamini kwa kutumia kijishamba changu hapo bagamoyo nitakuwa na reason ya kila weekend kwenda shamba na familia.

Sema nimekuwa na kiu sana ya kuwa na mashine ya kuangulia vifaranga na nyingi zinatumia umeme sasa ulivyosema ipo ya mafuta ya taa nimetamani kutimiza kiu yangu ili niinunue...inauzwaje na inauwezo wa kuangua mayai mangapi kwa muda gani...nisaidie mkuu information hizo ili nirudi kwenye mchanganuo wangu wa biashara .

DOKEZO: Kuku wa kienyeji aina ya kuchi au wale vishingo wakubwa ni biashara tosha na wana soko kubwa sanaa, tuchangamkie aina hiyo ya kuku..wanapatikana singida na Manyara.
 
Habari wadau,

Leo kwa mara ya kwanza ndo nimetumia jamii forum na nimeikubali 100% ina watu makini wapendao maendeleo!
sasa wadau mnaweza kueka info zaidi ya hiyo topic maana its very interesting!
 
kaka el-nino mie pia huwa na interest na ufugaji nikiamini kwa kutumia kijishamba changu hapo bagamoyo nitakuwa na reason ya kila weekend kwenda shamba na familia

sema nimekuwa na kiu sana ya kuwa na mashine ya kuangulia vifaranga na nyingi zinatumia umeme sasa ulivyosema ipo ya mafuta ya taa nimetamani kutimiza kiu yangu ili niinunue...inauzwaje na inauwezo wa kuangua mayai mangapi kwa muda gani...nisaidie mkuu information hizo ili nirudi kwenye mchanganuo wangu wa biashara ....DOKEZO...kuku wa kienyeji aina ya kuchi au wale vishingo wakubwa ni biashara tosha na wana soko kubwa sanaa...tuchangamkie aina hiyo ya kuku..wanapatikana singida na manyara

Kaka hapo kwenye kuku wa kienyeji wa kuchi na vishingo nimepapenda.Wana soko kweli hao? Bei yao na ya kisasa ipi inalipa?Wakuu naomba tu mtu mwenye habari hizo anitupie hapa Charleschami@yahoo.com. Nahisi nitapoteza hii post hapa.

Natanguliza shukrani.
 
kaka hapo kwenye kuku wa kienyeji wa kuchi na vishingo nimepapenda.Wana soko kweli hao?Bei yao na ya kisasa ipi inalipa?Wakuu naomba tu mtu mwenye habari hizo anitupie hapa Charleschami@yahoo.com.Nahisi nitapoteza hii post hapa.Natanguliza shukrani.
Kifupi kuku wa kienyeji wana soko (bei yao inalipa) kuliko wa kisasa!
Wengi wetu tuna elimu ya ufugaji wa hawa kuku wa kienyeji na wanalipa kwelikweli.
 
Kifupi kuku wa kienyeji wana soko (bei yao inalipa) kuliko wa kisasa!
Wengi wetu tuna elimu ya ufugaji wa hawa kuku wa kienyeji na wanalipa kwelikweli.

Mkuu hebu mwaga shule hapa ya ufugaji wa kuku wa kienyeji tuone kama tunaweza kupata ajira kipande hiyo
 
Kitu cha kwanza kinachotakiwa uwe nancho ni determination, bila hilo hata kama utapata elimu ya ufugaji haitokusaidia kitu, kwa mfano hivi kuku wa kienyeji anahitaji elimu gani ya ufugaji?

Na ukiamua kufuga kuku wa kisasa kila wasambazaji wa vifaranga wana maelekezo ya ufugaji bora, kwa mfano ukifika waambie unataka kufuga kuku 500 na wewe ndiyo unaanza, wao watakupa mshauri wao ambaye ataku guide wewe kuanzia kibanda chako, ulishaji nk mpaka kuku wako watakaponza kutaga.

Mkuu mimi nataka mbeu ya hao kuku, manake nimenza kwa hatua ndogo sana, nyumbani kwangu, nilijaribu kununua kuku wa kawadia sokoni, mara mbili wanakufa, labda kuna sehemu nakosea, kama ni chanjo, nikiwanunua tu siku hiyo hiyo nawapa na vitamin nawapa. hebu saidia hapa.

Mbegu ipi ni nzuri?
 
Mkuu mimi nataka mbeu ya hao kuku, manake nimenza kwa hatua ndogo sana, nyumbani kwangu , nilijaribu kununua kuku wa kawadia sokoni, mara mbili wanakufa, labda kuna sehemu nakosea, kama ni chanjo, nikiwanunua tu siku hiyo hiyo nawapa na vitamin nawapa. Hebu saidia hapa.

Mbegu ipi ni nzuri?

Kuku walioko sokoni au mbuzi anayepelekwa sokoni na wakulima wadogo ni wale ambao mkulima husika kagundua wana matatizo kwake, kama vile kudonoa mayai,kuua vitoto nk Mkulima makini hauzi mbegu bora hata siku moja,atafanya hivyo kama ana idadi kubwa sana au kabanwa.

Kujua source ya mbegu ni muhimu sana kwa kila mnyama unayetaka kumfuga.
 
Habari wakuu:

Bila shaka kuna watu ambao wanafuga kuku au walishawahi kufuga kuku. Naomba watu wenye uzoefu na maarifa kuhusu kufuga kuku wanipe mawazo, maana nataka kuanza kufuga kuku na sijawahi kufanya hivyo, hivyo nahitaji mawazo yenu wakuu.

Natanguliza shukrani zangu wakuu:

Mimi nilishawahi kufuga kuku na kwa kiasi fulani zimechangia kuniendeleza ki eleimu na kuwasaidia baadhi ya wategemezi - kuku nawakubali.

Ufugaji wa kuku inategemeana unataka wa aina gani (kisasa au Kienyeji) kwa kuku wa kisasa kidogo wanahitaji nguvu ya ziada na umakini wa hali ya juu wakati wakiwa wadogo na wanapokuwa kwa mazao bora. Vile vile kwa kuku wa kienyeji.

Kwa hapa nitatoa ushauri wa ju juu tu kwa kuwa taratibu zote za ufugaji ni nyingi kiasi kwamba kuandika hapa haitatosha, pia inategemeana unaishi wapi yaani maeneo ya baridi sana au joto.

Kwa kifupi, Ukitaka kufuga hasa wa kisasa wa mayai, chukua vifaranga vilivyozaliwa siku hiyo hiyo uanze kuvifuga wewe na si vile vilivyokaa juani kama pale buguruni kwa zaidi ya wiki1 au zaidi. Pia hakikisha unachukua vifaranga kwa mzalishaji ambaye anajali na si mchakachuaji kwa kuwa kama mazlishaji hakuwapa dawa fulani wakati wanataga mayai kuku wa kuzalisha vifaranga, vifaranga vinapozaliwa vinakuwa na ugonjwa wa kuzaliwa nao na vikifikisha miezi 3 vinakufa vyote kwa hiyo ni kuwa makini na utakaponunua vifaranga hivyo.

Ukifikisha vifaranga kutoka kwa aliyekuuzia unatakiwa uvipatie glucose ya kuku (Ya mifugo) na maji ya uvuguvugu kama unaishi mikoa ya baridi kama iringa au mbeya lakini kama dar hayahitajiki ya uvuguvugu. baada ya saa 2 unavipatia vitamini, vitamini hizo zipo za aina nyingi sana madukani kutokana na wazalishaji wengi na zingine inasemekana huwa ni feki inapaswa kuwa makini unaponunua, ila mimi napendelea Bidhaa za kutoka UFARANSA huwa ni nzuri zaidi.

Kwa maelezo zaidi ya ufugaji waweza kumtembelea mfugaji aliye karibu na wewe au hata daktari wa mifugo. Au MTAFUTE mwakilishi wa madawa ya kuku kutoka kampuni inayosambaza dawa za mifugo za LAPROVET, just I google tu, utamjua mwakilishi wa tanzania, ukimpigia simu hana kinyongo atakupa maelekezo ya kutosha.

Hata hivyo ufugaji wa kuku una tesa sana, kama hutafanya mwenyewe ukaajili msimamizi ambaye hayuko makin banda lote litateketea, halafu ukizembea kuwalisha watakonda na mazao hayakuwa mazuri na ndo mwanzo wa kuugua. Ukweli ni kwamba kuku wa kisasa wanakula balaa, yaani kama huna source nzuri ya pesa ya kununulia chakula cha kuku, bora usifuge, watakufilisi na mradi hautakuwa na matunda mazuri, kuku wanakula massaa 24, ila kuna rafiki yangu aliniambia wao kuku wao waliwazoesha kula mchana tu, na usiku walikuwa wakiwazimia taa. ukifanya hivyo utapata afueni, wanakula balaa.

Kwa kuku wa kienyeji ni rahisi zaidi, ukiwapa chakula cha kutosha na chanjo za kueleweka hawatakufa, kamwe na utapata faida nzuri zaidi.

Cha msingi katika ufugaji usizembee kuhakikisha unafuta taratibu zote za kutunza viumbe hawa, usikubali kumwachia mtu usiyemuamini kuwa atafanya unavyotaka na hata kama ni wa kisasa kienyeji jaribu kuwa na utaratibu wa kuwapa chakuala kwa muda fulani fulani na usipitilize hadi wazoee.

Pia usichelewe mpaka waanze kupiga makelele. La kuzongatia kabisa katika ufugaji wa kuku na mazao bora ni CHAKULA CHA KUTOSHA< UKIWEZA HILO HATA MAGONJWA HAYATAKUWA MENGI NA UTAFAIDI UFUGAJI WAKO.

Nawasilisha kama kuna sehemu nimekosea, hayo ni wawazo yangu naomba sahihisho tafadhali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom