Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Mkuu na vipi hawa kuku wa Malawi mbona kuna watu wanadai ni pure kisasa na si wakienyeji kwa sababu hawaatamii? au ni watu wamewabadili kwa kuwapandikiza na wa kisasa?
 
Mkuu na vipi hawa kuku wa Malawi mbona kuna watu wanadai ni pure kisasa na si wakienyeji kwa sababu hawaatamii? au ni watu wamewabadili kwa kuwapandikiza na wa kisasa?

Kwa uzoefu wangu kuhusu hawa kuku ni kuwa sio pure breed na sio Pure wa Kienyeji I think ni cross breed cause uwezo wao wa kuatamia ni mdogo sana au wanaweza wasiatamie kabisa na mayai yao ni meupe sio kama kama ya kisasa (ambayo ni mekundu kiasi) lakini pia weupe wao sio kama ya kienyeji kabisa wanauwezo wa kuhimili magonjwa kiasi ukilinganisha na wa kisasa lakini uwezo wao sio Mkubwa sana kama wa Kienyeji. kichwa mbovu atakuja kueleza zaidi
 
Mkuu inamaana ukiwa na kuku wa kisasa wa Mayai pamoja na majogoo hao wayi yao hyawezo kitotoreshwa? nini kinashindikana?

Hao kuku wa kisasa wa mayai wakiwekewa majogoo, mayai yao yataweza kutotolewa isipokuwa vifaranga wake watakuwa wadhaifu na hufa hovyo kwa kuwa wao sio pure breed, ni hybrid

Hii hybrid ni kosaafu maalum iliyotengenezwa kwa ajili ya kutaga mayai tu na si vinginevyo. Ndio maana inashauriwa kama unahitaji kutotoa vifaranga inatakiwa upate parent stock ambao ni pure breed.

Kama utahitaji kutumia hybrid basi tumia majogoo yake kisha cross na kuku wa kienyeji hapo utapata machotara wazuri wenye uwezo wa kukupa tija kubwa.
 
Kuku mmoja wa mayai anahitaji kilo 60 za chakula toka kifaranga wa siku moja hadi anachoka kutaga.Katika kipindi cha miezi miwili ya mwanzo (Kuanzia wiki 0-8) kuku anahitaji kilo 2, Wiki ya 9-20 atahitaji kilo 6 za chakula na Wiki 22-80, atahitaji kilo 52 za chakula. Wiki ya 80 kuku mayai anatakiwa auzwe kwani anakuwa tayari amechoka hivyo kuendelea kumfuga anaongeza gharama ya ulishaliji na matunzo kwa ujumla.
 
Mkuu nimekupata Vyema, Vipi kuku chotara wanakuwa tayali kwa ajili ya kuliwa baada ya Miezi mingapi? au na wao ni kama kuku wa kienyeji miezi kumi.
 
Mkuu nimekupata Vyema, Vipi kuku chotara wanakuwa tayali kwa ajili ya kuliwa baada ya Miezi mingapi? au na wao ni kama kuku wa kienyeji miezi kumi,

Kuku chotara wanakuwa tayari kuliwa au kuuzwa baada miezi 4 au 5. Umbo lao na uzito wao unakuwa mkubwa kuliko kuku wa kienyeji.Kama utaamua kuwafuga kwa miezi sita ni dhahiri kuwa utawauza kwa bei kubwa kuliko kawaida.
 
Mkuu Invisible tunaomba msaada wako wa ku sticky hii post if possible please.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kichwa mbovu kwanza kabisa hongera sana kwa shughuli unayoifanya na naamini wengi sana wanaifaidika kutokana na uzoefu wako ambao unautoa, mimi nahitaji kuanza kuanzia mwanzo kabisaaaaa,nahitaji kufuga kuku kwa ajili ya biashara zaidi,sasa hapo nitaomba msaada wako zaidi kama itawezekana,je ni bora zaidi kuanza na kuku wengi au kidogo??na je nina eneo langu ambalo kwa kweli itabidi tu discuss zaidi ambalo labda naweza kujenga banda hapo ila hiyo sehemu umeme haujafika bado,je utashauri vipi hasa??after kujenga hilo banda ni kuweka solar au vipi??je kujenga banda kwa kuanza na kuku 500 je inaweza kugharimu kiasi gani??na kwa upande wa biashara ni bora kuuza kuku na mayai au unashauri vipi??na upo available kusaifiri mkoa wowote kwa ajili ya kukagua eneo na sehemu??na upande wa mauzo je yapo hasa??isije mwisho wa siku kila kitu kipo tayari sehemu ya kuuza unakosa,nadhani nina maswali mengi ila kwa leo niishie hapa naomba ungenisaidia kunijibu ili tuweze kuwasiliana zaidi......

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kichwa mbovu kwanza kabisa hongera sana kwa shughuli unayoifanya na naamini wengi sana wanaifaidika kutokana na uzoefu wako ambao unautoa, mimi nahitaji kuanza kuanzia mwanzo kabisaaaaa,nahitaji kufuga kuku kwa ajili ya biashara zaidi,sasa hapo nitaomba msaada wako zaidi kama itawezekana,je ni bora zaidi kuanza na kuku wengi au kidogo??na je nina eneo langu ambalo kwa kweli itabidi tu discuss zaidi ambalo labda naweza kujenga banda hapo ila hiyo sehemu umeme haujafika bado,je utashauri vipi hasa??after kujenga hilo banda ni kuweka solar au vipi? Je kujenga banda kwa kuanza na kuku 500 je inaweza kugharimu kiasi gani??na kwa upande wa biashara ni bora kuuza kuku na mayai au unashauri vipi? Na upo available kusaifiri mkoa wowote kwa ajili ya kukagua eneo na sehemu? Na upande wa mauzo je yapo hasa? Isije mwisho wa siku kila kitu kipo tayari sehemu ya kuuza unakosa,nadhani nina maswali mengi ila kwa leo niishie hapa naomba ungenisaidia kunijibu ili tuweze kuwasiliana zaidi.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Ndugu Papizo kwanza nikupongeze kwa maswali yako mazuri.
Umeuliza idadi ya kuku wa kuanza nao kama ni wengi au kidogo. Kwa swali hili nadhani kwanza itategemea na mtaji wako na uzoefu katika ufugaji.Inawezekana ukawa na mtaji mkubwa ukatosha kuanza na kuku wengi lakini huna uzoefu kwenye ufugaji wa hawa kuku matokeo yake kama utafuga kuku wengi watakufa. Ninachoshauri kama huna uzoefu ni vyema ukaanza na wachache ili kupata uzoefu kusudi utakapoingia kamili kwenye hii nyanja utakuwa tayari umegain uzoefu,au kama sivyo ni muhimu ukapata mafunzo ili utakapofuga kuku wengi hutakumbana na vikwazo. Kifupi ukianza na kuku wengi inalipa zaidi na kiwango kinachopendekezwa cha kuanzia angalu kuku 500 kama wewe unahitaji.Na kama unataka zaidi ya hapo basi ufugaji huo uende kwa awamu(batch)

Kuhusu eneo kutokuwa na umeme.Sikiliza, katika ufugaji wa kuku,umeme si mahitaji ya msingi sana kwa kuku.Kuku hasa anapokuwa kifaranga anahitaji zaidi joto na mwanga hasa katika kipindi cha wiki tatu za mwanzo.Baada ya hapo vitu hivyo havihitajika tena. Kwa ajili ya joto na mwanga kwa sehemu ambayo hakuna umeme, kuna vyanzo vingine vinaweza kutumika,mfano kwa ajili ya kupata mwanga unaweza kutumia taa ya za chemli,na kwa kwa ajili ya kutoa joto,unaweza kutumia majiko ya kawaida ya mkaa.

Kuhusu gharama ya kujenga banda lenye uwezo wa kuchukua kuku 500,hapo itabidi uwaone watu wa uthamini wa majengo, mimi ninachoweza kukupa ni eneo la square mita ambalo kuu 500 wanahitaj. Kimsingi square mita moja huchukua kuku 6,kwa idada ya kuku 500 unaweza kupata eneo linalohitajika kwa kurejea post za nyuma,ila kama hutaelewa utaniuliza.

Kwa upande wa biashara ipi inalipa zaidi kati ya kuku wa mayai au nyama,kuku wote wanalipa.Kuku wa nyama wanawafaa zaidi wale wenye mitaji midogo na wanapenda kuongeza mitaji yao kwa harakaharaka. Wenye mitaji mikubwa ufugaji wa kuku wa mayai unawafaa zaidi.

Kuhusu availability yangu kusafiri mkoa wowote kwa ajili ya kutembelea kukagua miradi na kushauri nk,niko available kwa yeyote anayenihitaji. Ndiyo kazi yangu ninayaifanya siku zote kuwaanzishia watu miradi ya ufugaji ,kuwaongoza na kuwasimamia mpaka watakapoweza kusimama wenyewe.

Na mwisho umeongolea masoko,masoko yapo tena mengi,ingawa changamoto iliyopo kwa sasa ni kuwa bei ya mayai hairidhishi sana ukilinganisha na bei ya chakula,ingawa kwa bei iliyopo haileti hasara. Pia kuna kipindi baadhi ya mikoa soko la mayai huwa lina sumbua kidogo kwa kuwa soko la mayai huwa mara nyingi linakuwa kama la msimu hivi na huwa siachi kuwashauri kuwa kama ni mfugaji na unaifanya kama kazi,ni muhimu ukawa na chumba maalum ambacho unakuwa umekiwekea aircondition na kuseti nyuzi joto 13-20 kwa ajili ya kuhifadhi mayai kwa muda mrefu.
 
Ndugu Papizo kwanza nikupongeze kwa maswali yako mazuri.
Umeuliza idadi ya kuku wa kuanza nao kama ni wengi au kidogo.Kwa swali hili nadhani kwanza itategemea na mtaji wako na uzoefu katika ufugaji.Inawezekana ukawa na mtaji mkubwa ukatosha kuanza na kuku wengi lakini huna uzoefu kwenye ufugaji wa hawa kuku matokeo yake kama utafuga kuku wengi wakafa.Ninachoshauri kama huna uzoefu ni vyema ukaanza na wachache ili kupata uzoefu kusudi utakapoingia kamili kwenye hii nyanja utakuwa tayari umegain uzoefu,au kama sivyo ni muhimu ukapata mafunzo ili utakapofuga kuku wengi hutakumbana na vikwazo.Kifupi ukianza na kuku wengi inalipa zaidi na kiwango kinachopendekezwa cha kuanzia angalu kuku 500 kama wewe unahitaji.Na kama unataka zaidi ya hapo basi ufugaji huo uende kwa awamu(batch)

Kuhusu eneo kutokuwa na umeme.Sikiliza, katika ufugaji wa kuku,umeme si mahitaji ya msingi sana kwa kuku.Kuku hasa anapokuwa kifaranga anahitaji zaidi joto na mwanga hasa katika kipindi cha wiki tatu za mwanzo.Baada ya hapo vitu hivyo havihitajika tena.Kwa ajili ya joto na mwanga kwa sehemu ambayo hakuna umeme, kuna vyanzo vingine vinaweza kutumika,mfano kwa ajili ya kupata mwanga unaweza kutumia taa ya za chemli,na kwa kwa ajili ya kutoa joto,unaweza kutumia majiko ya kawaida ya mkaa.

Kuhusu gharama ya kujenga banda lenye uwezo wa kuchukua kuku 500,hapo itabidi uwaone watu wa uthamini wa majengo, mimi ninachoweza kukupa ni eneo la square mita ambalo kuu 500 wanahitaj.Kimsingi square mita moja huchukua kuku 6,kwa idada ya kuku 500 unaweza kupata eneo linalohitajika kwa kurejea post za nyuma,ila kama hutaelewa utaniuliza.

Kwa upande wa biashara ipi inalipa zaidi kati ya kuku wa mayai au nyama,kuku wote wanalipa.Kuku wa nyama wanawafaa zaidi wale wenye mitaji midogo na wanapenda kuongeza mitaji yao kwa harakaharaka.Wenye mitaji mikubwa ufugaji wa kuku wa mayai unawafaa zaidi.

Kuhusu availability yangu kusafiri mkoa wowote kwa ajili ya kutembelea kukagua miradi na kushauri nk,niko available kwa yeyote anayenihitaji.Ndiyo kazi yangu ninayaifanya siku zote kuwaanzishia watu miradi ya ufugaji ,kuwaongoza na kuwasimamia mpaka watakapoweza kusimama wenyewe.

Na mwisho umeongolea masoko,masoko yapo tena mengi,ingawa changamoto iliyopo kwa sasa ni kuwa bei ya mayai hairidhishi sana ukilinganisha na bei ya chakula,ingawa kwa bei iliyopo haileti hasara.Pia kuna kipindi baadhi ya mikoa soko la mayai huwa lina sumbua kidogo kwa kuwa soko la mayai huwa mara nyingi linakuwa kama la msimu hivi na huwa siachi kuwashauri kuwa kama ni mfugaji na unaifanya kama kazi,ni muhimu ukawa na chumba maalum ambacho unakuwa umekiwekea aircondition na kuseti nyuzi joto 13-20 kwa ajili ya kuhifadhi mayai kwa muda mrefu.

Mkuu ninaswali hapo kwenye kuhifadhi mayai muda mrefu, vipi mbna huwa nasikia mayai yaliyo rutubiswa ndo anatakiwa kuhifadhiwa kwa muda huo ila ambayo hayajarutubiswa hayana shinda, hapo sanasana ni mayai wa kuku wa kienyeji,

na kuna sehemu nilisoma zile njia za kuua mbegu kwenye yai na kulifanya liishi muda mrefu endapo huna mpango wa kuatamisha hayo mayai
 
Mkuu ninaswali hapo kwenye kuhifadhi mayai muda mrefu, vipi mbna huwa nasikia mayai yaliyo rutubiswa ndo anatakiwa kuhifadhiwa kwa muda huo ila ambayo hayajarutubiswa hayana shinda, hapo sanasana ni mayai wa kuku wa kienyeji,

na kuna sehemu nilisoma zile njia za kuua mbegu kwenye yai na kulifanya liishi muda mrefu endapo huna mpango wa kuatamisha hayo mayai

Ninachokifahamu mayai yakikaa muda mrefu yanaharibika kwa maana ya ule ubora wake.Tunaposema kuharibika kwa mayai ni kule kuachana kwa kwa kiini kile cha katikati.Unapolipasua yai linakuwa linamwagika kama maji. Kwa wateja wanaojua mayai,akinunua yai akalipasua na likaonyesha dalili hizo wataja hawarudi tena.Ndio maana tunashauri ili kumaintain ubora wa yai linatakiwa lihifadhiwe kwenye air condition. Pia tunatumia kwa ajili ya mayai ya kutotoresha kwa ajili ya kumaintain fertility ya mayai.
 
Ninachokifahamu mayai yakikaa muda mrefu yanaharibika kwa maana ya ule ubora wake.Tunaposema kuharibika kwa mayai ni kule kuachana kwa kwa kiini kile cha katikati.Unapolipasua yai linakuwa linamwagika kama maji.Kwa wateja wanaojua mayai,akinunua yai akalipasua na likaonyesha dalili hizo wataja hawarudi tena.Ndio maana tunashauri ili kumaintain ubora wa yai linatakiwa lihifadhiwe kwenye air condition.Pia tunatumia kwa ajili ya mayai ya kutotoresha kwa ajili ya kumaintain fertility ya mayai.

Sasa kama mayai ya Kutotoresha unayatoa mbali inakuwaje hapo? make unaweza nunua mayai Dar na ukapeleka Arusha kwa ajili ya Kuatamisha sasa hapo si inakuwa ni risk sana?
 
sasa kama mayai ya Kutotoresha unayatoa mbali inakuwaje hapo? make unaweza nunua mayai Dar na ukapeleka Arusha kwa ajili ya Kuatamisha sasa hapo si inakuwa ni risk sana?

Kama mayai unayatoa Dar na kuyapeleka Arusha hayana shida kwani mayai ya kutotolewa yana uwezo wa kukaa mpaka siku 14 katika joto la room temperature.Ingawa yai likikaa chini ya siku kumi uwezo wake wa kutotolewa unakuwa mkubwa zaidi ukilinganisha na mayai yaliyokaa kwa siku 14.Risk kubwa iliyopo ya kusafirisha mayai kutoka Dar hadi arusha ni namna ya kuyasafirisha kwa usalama ,maana yai la kutotolewa halitakiwi liwe na cracks
 
Kama mayai unayatoa Dar na kuyapeleka Arusha hayana shida kwani mayai ya kutotolewa yana uwezo wa kukaa mpaka siku 14 katika joto la room temperature.Ingawa yai likikaa chini ya siku kumi uwezo wake wa kutotolewa unakuwa mkubwa zaidi ukilinganisha na mayai yaliyokaa kwa siku 14.Risk kubwa iliyopo ya kusafirisha mayai kutoka Dar hadi arusha ni namna ya kuyasafirisha kwa usalama ,maana yai la kutotolewa halitakiwi liwe.

Mkuu sijakupata make umeishia njiani, vipi network imekata?

Ya najua inatakiwa si chini ya siku 14, Sema ishu iko kwene uamnifu make unaweza enda kununua mayai mtu akakuambia yana siku Mbili kumbe yana wiki mbili na zaidi,

Na mimi naona usalama zaidi ni kuwa na mayai yako mwenyewe kwa ajili ya Kutotoresha na si kununua ya mtaani
 
Mkuu sijakupata make umeishia njiani, vipi network imekata?

Ya najua inatakiwa si chini ya siku 14, Sema ishu iko kwene uamnifu make unaweza enda kununua mayai mtu akakuambia yana siku Mbili kumbe yana wiki mbili na zaidi,

Na mimi naona usalama zaidi ni kuwa na mayai yako mwenyewe kwa ajili ya Kutotoresha na si kununua ya mtaani

Sorry mkuu nime edit.

Unachosema mheshimiwa uko sahihi kabisa,mtu unapotaka kufanya biashara ya utoreshaji wa vifaranga,ni muhimu kwanza ukaanda parent stock yako itakayokusaidia kupata mayai uliyo na uhakika nayo. Kutegemea mayai kutoka sehemu nyingine kila siku utakuwa unatengeneza hasara kwani wafanyabiashara wengi ambao wanauza mayai ya utotoreshaji si waaminifu hata kidogo.
 
nimevutika na nimependa sana ushauri wako,ukizingatia mimi ni mwanafunzi wa chuo,na nategemea sana niweze kujiajiri mwenyewe ila nilikua sijajua niende kwenye field gani maana najihisi sina kipaji na sina uwezo mkubwa ila nimevutika na mraadi huu wa ufugaji kuku,mimi naitaji kujua haya yafuatayo

(1)jinsi gani nitapata elimu ya ufugaji wa kuku wa kienyeji na wapi kwa garama zipi,kwa sasa hivi mi nipo chuoni zanzibar ila naitaji kujua kwakua nipo kwenye semester ya mwisho na nikimaliza narudi home dar na kuelekea kijijini kwetu tayari kwa kulitumikia taifa kupitia kujiajiri kama hivyo,
 
Mkuu kama mayai yataweza kuhifadhiwa kwenye aircondition kama ulivyoeleza hapo juu yanaweza kukaa muda gani bila kuharibika?
 

Similar Discussions

30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom