Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Mkuu, nataka kujua ni nyavu zipi nzuri kwa Kuweka kwenye Banda la kuku? Maana kuna aina nyingi sana za nyavu
 
Asante mkuu Kichwa Ngumu kwa elimu nzuri juu ya ufugaji wa kuku. Mimi mwenzangu anafuga kwa kiwango cha chini na ni kweli kama mfugaji anaweza kuzuia idadi ya vifo, basi faida ni wazi sana. Sijui kama unaweza kutoa miongozo ya utengenezaji wa chakula, maana kwa uzoefu wangu mdogo mwenzangu alipojaribu kutengeneza chakula mwenyewe gharama ilikuwa kubwa zaidi ya gharama ya kununua rejareja. Bahati mbaya sasa sina access ya mtandao, mara ukirudi nitakutumia kwa PM mchanganuo wa chakula. Ambacho nakumbuka ni mahindi ni kama kilo 850 kwa tani ya chakula (kuku wa nyama)

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Mheshimiwa Mzawa halisi,miongozo ya formula za uchanganyaji wa chakula ,utotoreshaji wa vifaranga,ufugaji bora wa kuku,magonjwa mbalimbali ya kuku,dalili zake na namna ya kuyazuia na kuyatibu na ujezi wa mabanda bora ya kuku tunayo.Unaweza ukanipm namba zako kwa maelezo zaidi.

Kilo 850 za mahindi katika tani ni kiasi kingi sana ndio maana gharama ya kujitengenezea chakula kinakuwa kubwa kuliko kile cha kununua.
 
Leo niuzungumzie ugonjwa wa mafua(Infectious coryza)

Mafua ni ugonjwa mojawapo unaoshambulia mfumo wa upumuaji wenye tabia ya kumfanya kuku kutoa kamasi puani,kupiga chafya,kichwa kujaa maji na kuvimba.Ugonjwa huu huwaathiri kuku,bata mzinga na kanga.
Mafua ni ugonjwa unaowapata jamii ya ndege wa umri wote lakini zaidi ni kwa wakubwa.Ueneaji wake ni kwa njia ya hewa na chanzo chake ni ndege wanaougua au waliougua.

KISABABISHI
Mafua ya kuku husabibwa na Kimelea(Bacteria) kiitwacho Haemophilus paragallinum

DALILI ZA MAFUA
Dalili za mafua huanza kuonekana kuanzia siku ya 3-10 toka kuambukizwa.Sehemu zinazodhihirika zaidi ni pua,macho,mapafu,koo na koromeo.
  1. Kuku kuzubaa na kuto makamasi wakati mwingine yenye damu.
  2. Kubadilika rangi ya mapanga(Comb and wattle) na kuwa ya rangi ya bluu
  3. Huvimba macho,hali inayosabababisha kuku kuziba jicho moja na wakati mwingine yote mawili
  4. Kuvimba mapanga na uso
  5. kukosa hamu ya kula na kupunguza utagaji
  6. Kuku kukoroma wakati wa kupumua
  7. Kuhara uharo wenye harufu mbaya hasa kama kuna maambukizi mengine ya vimelea
  8. Vifo ni vichache na kuku hupona baada ya wiki

NAMNA YA KUZUIA
  • Usafi wa mazingira na kuhakikisha hakuna vimelea wanaosababisha ugonjwa huu
  • Kuku wagonjwa watengwe mbali na kuku wazima
  • Hakikisha vifaranga wanaagizwa kutoka kwenye makampuni yanayofuata kanuni bora za ufugaji
TIBA
Mafua ni ugonjwa unaotibika,mfugaji unaweza kumwona afisa mifugo aliye karibu nawe ili akuandikie dawa sahihi ya kutumia.



Nataka kichwa na contacts zenu tafadhali. Nina mpango wa kumwanzishia mama yangu huu mtaji.
 
Mkuu nataka kujua ni nyavu zipi nzuri kwa Kuweka kwenye Banda la kuku? make kuna aina nyingi sana za nyavu

Mheshimiwa chasha nyavu nzuri za kuku ni zile nyavu za kawaida ambao wafugaji wengi wanazitumia,kifupi ziwe na matundu makubwa kwa ajili ya kuruhusu hewa safi kuingia na kutoka.
 
Mkuu, asante sana kwa elimu uliyotoa. Nimejifunza mengi maana mm tayari nafuga kuku aina ya chotara,vifaranga kutoka Malawi.
 
Sijui kama Mtaalam wetu Kichwa Mbovu ana source nyengine, najua kuna watu wanauza Mbezi kwa Musuguri.

Tram Almasi,mbezi kwa msuguri mnanunulia kwa nani,mimi kule namfahamu mheshimiwa mmoja anaitwa Mr Mrindwa anazalisha na kuuza vifaranga wengi sana wa malawi.

Kama kuna mwingine kwa mbezi msuguri sijajua. Sehemu nyingine nje ya Mbezi kwa Msuguri nina source nyingine nyingi, mfano Mbeya kuna watu nawafahamu wanajihusisha na biashara ya aina hii ya vifaranga wa Malawi.
 
Tram Almasi,mbezi kwa msuguri mnanunulia kwa nani,mimi kule namfahamu mheshimiwa mmoja anaitwa Mr Mrindwa anazalisha na kuuza vifaranga wengi sana wa malawi.Kama kuna mwingine kwa mbezi msuguri sijajua. Sehemu nyingine NJE YA Mbezi kwa msuguru nina source nyingine nyingi,mfano mbeya kuna watu nawafahamu wanajihusisha na biashara ya aina hii ya vifaranga wa malawi.

Mkuu hebu weka namba za huyi Mheshimiwa Mr. Mrindwa ili watu wawasiliane nae.
 
Mkuu hebu weka namba za huyi Mheshimiwa Mr Mrindwa ili watu wawasiliane nae

Unaweza ukanitafuta kwa namba zangu nikakupa namba za Mr Mrindwa then ukawasiliana nae.Nitafanya hivyo pia kwa yeyote mwingine anayehitaji namba zake.
 
Unaweza ukanitafuta kwa namba zangu nikakupa namba za Mr Mrindwa then ukawasiliana nae.Nitafanya hivyo pia kwa yeyote mwingine anayehitaji namba zake.

Vipi hawa jamaa wa Ben chicks make nilicheki website yao na wao wana kuku wa Malawi ila ni Chotara na wanauza vifaranga na Mayi pia ya kutotoresha, vipi wako vipi? na kabla ya kuomba namba vipi bei zke za vifaranga?
 
Mkuu, nashukuru kwa elimu murua ya ufugaji kuku. Hivi kuna madhara gani ya kufuga kuku wa kienyeji na wa kisasa ktk compound moja?
 
Vipi hawa jamaa wa Ben chicks make nilicheki website yao na wao wana kuku wa Malawi ila ni Chotara na wanauza vifaranga na Mayi pia ya kutotoresha, vipi wako vipi? na kabla ya kuomba namba vipi bei zke za vifaranga?

Kiukweli Ben chicks mheshimiwa chasha sijawahi kuwafuatilia kupata habari yao,nadhani ni kampuni changa ambayo bado haijapata kufahamika zaidi na wengi.Nashindwa kutolea mapendekezo, ila nitajaribu kuifuatilia niijue kwa undani zaidi kupitia website yao.Bei ya vifaranga weusi wa malawi na machotora wengine anaozalisha mr Mrindwa anauza kwa Tsh.1500 kwa kila kifaranga cha siku moja.
 
Mkuu nashukuru kwa eliju murua ya ufugaji kuku. Hivi kuna madhara gani ya kufuga kuku wa kienyeji na wa kisasa ktk compound moja?

Zaidi madhara yako kwenye upande wa magonjwa.KUKU wa kienjeji yeye ni mstahimilivu dhidi ya magonjwa ukilinganisha na kuku wa kisasa.Kama watafugwa kwenye compaund moja watakaoathirika ni kuku wa kisasa kwani magonjwa yatatoka kwa kuku wa kienyeji kwenda kwa kuku wa kisasa.

Kuku wa kisasa atakapopata hatokuwa na uwezo wa kustahimili hivyo kuku wengi watakufa. Kama utahitaji kuwafiga katika compound moja,hakikisha kuku hawa wanafugwa katika mfumo wa ndani tu yaani Intensive system, ambapo kuku wa kienyeji na wa kisasa wafugwe katika vyumba tofauti kabisa na wala wasichanganywe na mlangoni kuingia kwenye kila banda kuwe na dawa zilizochanganywa kwenye maji na kila atakeyeingia ndani atapaswa akanyage/aoshe miguu yake ili kuua wadudu visababishi vya magonjwa.
 
Zaidi madhara yako kwenye upande wa magonjwa.KUKU wa kienjeji yeye ni mstahimilivu dhidi ya magonjwa ukilinganisha na kuku wa kisasa.Kama watafugwa kwenye compaund moja watakaoathirika ni kuku wa kisasa kwani magonjwa yatatoka kwa kuku wa kienyeji kwenda kwa kuku wa kisasa.Kuku wa kisasa atakapopata hatokuwa na uwezo wa kustahimili hivyo kuku wengi watakufa.Kama utahitaji kuwafiga katika compound moja,hakikisha kuku hawa wanafugwa katika mfumo wa ndani tu yaani Intensive system,ambapo kuku wa kienyeji na wa kisasa wafugwe katika vyumba tofauti kabisa na wala wasichanganywe na mlangoni kuingia kwenye kila banda kuwe na dawa zilizochanganywa kwenye maji na kila atakeyeingia ndani atapaswa akanyage/aoshe miguu yake ili kuua wadudu visababishi vya magonjwa.

Hizo dawa ni zipi mkuu za kuchanganganya kwenye maji ili mtu akanyage?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom