Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Hey JF Members,

Ee bwana kuna mtu anaweza kunipa msaada wa mchanganuo wa kufuga kuku. naona soko la kuku ni kubwa sana. hii ni biashara ambayo soko lake liko tayari. hotels, functions, vibanda vya chipss.... Yeyote mwenye idea naomba msaada please!!!!!

Kwenye msafara wa mamab na kenge tumo Tunasikililizia
 
Fuga nguruwe wewee au fungua maduka manzese na Ubungo external kama upo ndarisalama.

kuku kichefuchefu!! wakipata ugonjwa usiku, mpaka ukiamka huna hata wa ushahidi.

Biashara zote unahitaji ku risk kaka kuku hawawezi kufa wote kama unafuata mashart uliyopewa.
 
Biashara zote unahitaji ku risk kaka kuku hawawezi kufa wote kama unafuata mashart uliyopewa
Umenena mkuu hata hao nguruwe wana magonjwa yao na siku hizi nasikia wanawaiba kwa urahisi kwa kuwapa dawa za kulevya- cha msingi ni uangarifu tu. kawaida kwenye risk kubwa ndipo kwenye faida zaidi.
 
Wa DSM ebu nambien tray moja ya mayai kuku wa kisasa ni sh ngap? na kienyeji ni sh ngapi, nitaingia apo muda si mrefu!

Tray ya kuku wa mayai ni 5500 na Tray ya kuku wa kienyeji ni 12,000. (Bei za DAR)

Sasa lets say una kuku wa mayai 2000 tu. Kawaida production si chini ya 75% so kadirio la chini you have
75/100 times 2000 = 1500 mayai kwa siku ambayo ni sawa na tray 50 ( Kila Tray ina mayai 30)
So tray 50 times 5500 = 275,000/=
Toa chakula chao ambacho wanakula gram 25 so average itakuwa mifuko 5 ya Layers Mash kwa siku @ 30,000 = 150,000/=
So Net sells per day itakuwa Tshs 275,000 - 150,000 = 125,000/= per day

Per month 125,000 times 30 days = 3,750,000/=

What if you expand your business three times - yaani uwe na kuku 6000? Net profit per month itakuwa 3,750,000 times 3 = 11,250,000 Per month. Je kuna haja ya kuajiriwa na mtu?

You can as well change the business kwani by 3 years utakuwa na mtaji wa kutosha kuwekeza kwenye kitu chenye low risk - lakini kwa kuanza ukiogopa risk utaishia kupigia magoti waajiri wako na kugombana nao kuhusu mshahara na marupurupu kila kukicha.
 
Fuso hesabu zako zipo karibu na ukweli ingawa kuna maeneo unahitaji kuboresha mfano chakula cha kuku (layers mash) wanakula 125gm na si 25gm. aidha kikawaida kuna gharama nyingine zaidi ya chakula mfano salary ya wafanyakazi na madawa. kuna mtu anawema kuwa principle inayotumika kukokotoa faida ni kuwa 50% ya ya gross ndo faida. baada ya kufanya mahesabu naona kuwa faida inatakiwa kuwa 50%x275,000 = 137,500/= but kutokana na uncertainities nyingi kufanya faida ya 125,000 kwa siku si mbaya na ni vizuri kupigia hesabu za chini!!.
 
Mkuu nimekusoma, ila kumbuka kwenye hesabu yangu nimetumia 75%, hapa ni kadirio la chini kabisa la production. Production inaweza kwenda hadi 85 - 90% kama unafuata masharti mazuri ya ufugaji. Kuhusu ulaji yes ni 125gms times 2000 = 250,000 ambazo ni sawa na 250kgs. Kila mfuko una 50kgs so unarudi pale pale mifuko 5 kwa siku kwa bei ya 30,000 unatumia Tshs 150,000/- kwa siku chakula tu.

Sasa hiyo percetage ya production inayobakia kufikia kwenye 85 or 90% (lets say 10% - 15%) ndiyo inakuja kwenye salaries na matumizi mengine. Kumbuka pia mbolea ya kuku inauzwa kiroba cha kilo 50 ni Tshs 1500. kwa mwezi unatoa viroba vya mbolea 100 kwa wastani, so una 150,000 mauzo ya mbolea hii pia inaweza kwenda kwenye madawa na kuongezea kwenye salaries na marupurupu ya wafanyakazi ili waipende kazi yao hence ku-maintain production.
 
Fuso ahsante kwa maelezo ya ziada, nitakutafuta tuweze kuchit chat kidogo!!

Nimependa mtazamo wako!!
 
Kuku wa kienyeji ni rahisi zaidi kuwafuga hasa kama huna nafasi ya kusinda nyumbani asbh-jioni. Kwani ukiamua kuwafuga kisasa (na inawezekana kabisa), unaweza kuanza na majike yanayokaribia kutaga, au vifaranga. Majike najua yanapatikana Tabata Chang'ombe ambayo ni kuku mfalme na Red Rhodes Island (sijui kama nimepatia order ya maneno lkn sijakosea herufi) na vifaranga vipo sehemu mbali mbali, kuna hapo tbt chang'ombe, Ruvu jkt (mchanganyiko), Kuna mama mmoja anaitwa Mama Mayunga ana kuku weusi kutoka mbeya, kuna Kilacha, na wenigne wengi. pia unaweza kununua kwa wafugaji wa mitaani, hasa nje ya mji kama Mkuranga, chanika nk.

Ufuagaji mzuri lkn ni gharama ni ufugaji wa ndani,

Faida:
  1. Sio rahisi magonjwa ya mlipuko kuingia hasa kutoka kwa kuku wa nje.
  2. Ni rahisi kujua tabia mbaya za kuku, mfano ulaji wa mayai,
  3. Ni rahisi kujua kuku waataga kwa muda gani yaani idadi ya mayai.
Hasara:
  1. Ni gharama, maana kuku hawajitafutii chakula inabidi ununue,
  2. ikitokea ugonjwa ukaingia bandani basi wote wako hatarini kuumwa.
mkakati:
  1. Dawa za magonjwa mbalimbali, vitamin na chanjo ni vitu ambavyo unatakiwa kuwa navyo karibu.
  2. Tenga kuku kutokana na umri ambao ni vifaranga sk 1-sk42, sk 42-sk180, na sk 180->, kwani kwa makundi hayo kuku hula vyakula tofauti.
  3. Muone afisa mifugo mara kwa mara hasa kuhusu chanjo na madawa, kama uko Dar ni vizuri ukaenda Farmers center, au Farmbase i maeneo ya ilala.
  4. Wanapokaribia kutaga andaa mipango ya utotoaji mfano unataka walalie au ukatotoleshe kwenye incubators ambazo zinapatiaka sehemu mbalimbali hapa Dar mfano Magomeni mt wa Idrisa.
  5. mara nyingi mayai ya kwanza huwa hayatotoleshwi kwa sababu inawezekana kuku hakupandwa na ni madogo sana kwa hiyo uza upate hela kulisha kuku au kula uongeze afya.
Kwaushauri wangu totolesha kwenye incubators kwani unapata vifaranga vingi kwa wakati mmoja gharama za ulishaji zanapungua pia kuku akinyang'anywa mayai hutaga haraka sana ndani ya wk mbili hivi tofauti na anayelalia maana akimaliza kutaga atalia siku 21 atalea siku 42, hlf atataga baada sk 14. Wakati ukimnyang'anya ataga tena baada ya wk mbili.
Usisahau kuwapa vitamini.

Au tafuta usaidizi wa kuchagua kuku walaliaji na waleaji ili kuku wengine waendelee kutaga kama kawaida.

Ni hayo tu kwa sasa.
 
Kuku wa kienyeji ni rahisi zaidi kuwafuga hasa kama huna nafasi ya kusinda nyumbani asbh-jioni.

Kwani ukiamua kuwafuga kisasa (na inawezekana kabisa), unaweza kuanza na majike yanayokaribia kutaga, au vifaranga. Majike najua yanapatikana tabata chang'ombe ambayo ni kuku mfalme na Red Rhodes Island (sijui kama nimepatia order ya maneno lkn sijakosea herufi) na vifaranga vipo sehemu mbali mbali, kuna hapo tbt chang'ombe, Ruvu jkt (mchanganyiko), Kuna mama mmoja anaitwa Mama Mayunga ana kuku weusi kutoka mbeya, kuna Kilacha, na wenigne wengi. pia unaweza kununua kwa wafugaji wa mitaani, hasa nje ya mji kama Mkuranga, chanika nk.

Ufuagaji mzuri lkn ni gharama ni ufugaji wa ndani,

Faida:
  1. Sio rahisi magonjwa ya mlipuko kuingia hasa kutoka kwa kuku wa nje.
  2. Ni rahisi kujua tabia mbaya za kuku, mfano ulaji wa mayai,
  3. Ni rahisi kujua kuku waataga kwa muda gani yaani idadi ya mayai.
Hasara:
  1. Ni gharama, maana kuku hawajitafutii chakula inabidi ununue,
  2. ikitokea ugonjwa ukaingia bandani basi wote wako hatarini kuumwa.
mkakati:
  1. Dawa za magonjwa mbalimbali, vitamin na chanjo ni vitu ambavyo unatakiwa kuwa navyo karibu.
  2. Tenga kuku kutokana na umri ambao ni vifaranga sk 1-sk42, sk 42-sk180, na sk 180->, kwani kwa makundi hayo kuku hula vyakula tofauti.
  3. Muone afisa mifugo mara kwa mara hasa kuhusu chanjo na madawa, kama uko Dar ni vizuri ukaenda Farmers center, au Farmbase i maeneo ya ilala.
  4. Wanapokaribia kutaga andaa mipango ya utotoaji mfano unataka walalie au ukatotoleshe kwenye incubators ambazo zinapatiaka sehemu mbalimbali hapa Dar mfano Magomeni mt wa Idrisa.
  5. mara nyingi mayai ya kwanza huwa hayatotoleshwi kwa sababu inawezekana kuku hakupandwa na ni madogo sana kwa hiyo uza upate hela kulisha kuku au kula uongeze afya.
Kwaushauri wangu totolesha kwenye incubators kwani unapata vifaranga vingi kwa wakati mmoja gharama za ulishaji zanapungua pia kuku akinyang'anywa mayai hutaga haraka sana ndani ya wk mbili hivi tofauti na anayelalia maana akimaliza kutaga atalia siku 21 atalea siku 42, hlf atataga baada sk 14. Wakati ukimnyang'anya ataga tena baada ya wk mbili.

Usisahau kuwapa vitamini.

Au tafuta usaidizi wa kuchagua kuku walaliaji na waleaji ili kuku wengine waendelee kutaga kama kawaida.

Ni hayo tu kwa sasa.

Tinya, well said

Thanks you for this useful post.
 
Taniya nashkuru kwa habarizako na ufafanuzi mzuri nimepata tamaa yakuwafuga hao kuku je kunauwezekano wakupata mawsiliano na haop jamaa wa tabata chang' mbe?
kuku wa kienyeji ni rahisi zaidi kuwafuga hasa kama huna nafasi ya kusinda nyumbani asbh-jioni.

kwani ukiamua kuwafuga kisasa (na inawezekana kabisa), unaweza kuanza na majike yanayokaribia kutaga, au vifaranga. Majike najua yanapatikana tabata chang'ombe ambayo ni kuku mfalme na Red Rhodes Island (sijui kama nimepatia order ya maneno lkn sijakosea herufi) na vifaranga vipo sehemu mbali mbali, kuna hapo tbt chang'ombe, Ruvu jkt (mchanganyiko), Kuna mama mmoja anaitwa Mama Mayunga ana kuku weusi kutoka mbeya, kuna Kilacha, na wenigne wengi. pia unaweza kununua kwa wafugaji wa mitaani, hasa nje ya mji kama Mkuranga, chanika nk.

Ufuagaji mzuri lkn ni gharama ni ufugaji wa ndani,

Faida:
  1. sio rahisi magonjwa ya mlipuko kuingia hasa kutoka kwa kuku wa nje.
  2. Ni rahisi kujua tabia mbaya za kuku, mfano ulaji wa mayai,
  3. Ni rahisi kujua kuku waataga kwa muda gani yaani idadi ya mayai.
Hasara:
  1. Ni gharama, maana kuku hawajitafutii chakula inabidi ununue,
  2. ikitokea ugonjwa ukaingia bandani basi wote wako hatarini kuumwa.
mkakati:
  1. Dawa za magonjwa mbalimbali, vitamin na chanjo ni vitu ambavyo unatakiwa kuwa navyo karibu.
  2. Tenga kuku kutokana na umri ambao ni vifaranga sk 1-sk42, sk 42-sk180, na sk 180->, kwani kwa makundi hayo kuku hula vyakula tofauti.
  3. Muone afisa mifugo mara kwa mara hasa kuhusu chanjo na madawa, kama uko Dar ni vizuri ukaenda Farmers center, au Farmbase i maeneo ya ilala.
  4. Wanapokaribia kutaga andaa mipango ya utotoaji mfano unataka walalie au ukatotoleshe kwenye incubators ambazo zinapatiaka sehemu mbalimbali hapa Dar mfano Magomeni mt wa Idrisa.
  5. mara nyingi mayai ya kwanza huwa hayatotoleshwi kwa sababu inawezekana kuku hakupandwa na ni madogo sana kwa hiyo uza upate hela kulisha kuku au kula uongeze afya.
Kwaushauri wangu totolesha kwenye incubators kwani unapata vifaranga vingi kwa wakati mmoja gharama za ulishaji zanapungua pia kuku akinyang'anywa mayai hutaga haraka sana ndani ya wk mbili hivi tofauti na anayelalia maana akimaliza kutaga atalia siku 21 atalea siku 42, hlf atataga baada sk 14. Wakati ukimnyang'anya ataga tena baada ya wk mbili.
Usisahau kuwapa vitamini.

Au tafuta usaidizi wa kuchagua kuku walaliaji na waleaji ili kuku wengine waendelee kutaga kama kawaida.

Ni hayo tu kwa sasa.
 
Tray ya kuku wa mayai ni 5500 na Tray ya kuku wa kienyeji ni 12,000. (Bei za DAR)

Sasa lets say una kuku wa mayai 2000 tu. Kawaida production si chini ya 75% so kadirio la chini you have
75/100 times 2000 = 1500 mayai kwa siku ambayo ni sawa na tray 50 ( Kila Tray ina mayai 30)
So tray 50 times 5500 = 275,000/=
Toa chakula chao ambacho wanakula gram 25 so average itakuwa mifuko 5 ya Layers Mash kwa siku @ 30,000 = 150,000/=
So Net sells per day itakuwa Tshs 275,000 - 150,000 = 125,000/= per day

Per month 125,000 times 30 days = 3,750,000/=

What if you expand your business three times - yaani uwe na kuku 6000? Net profit per month itakuwa 3,750,000 times 3 = 11,250,000 Per month. Je kuna haja ya kuajiriwa na mtu?

You can as well change the business kwani by 3 years utakuwa na mtaji wa kutosha kuwekeza kwenye kitu chenye low risk - lakini kwa kuanza ukiogopa risk utaishia kupigia magoti waajiri wako na kugombana nao kuhusu mshahara na marupurupu kila kukicha.

Sawa mkuu lakini umesahau kutuwekea na gharama za kuwalea hao kuku kwa wiki 20 kabla hawajataga. Kwa maana hiyo kuku 2000 wanakula wastani wa gm 80 kwa siku, watakula kilo 160 sawa na mifuko 4 ya 50kg kwa siku, so mifuko 4 x Tsh33,000 x siku 150 = 19,800,000. Pia usisahau uliwanunua kwa Tsh 2200 kila mmoja, yaani 2000 x 2200 = 4,400,000, so kabla hujaanza kufuga kuku 2000 uwe na milioni 25 kibindoni, hapo hujapigia garama za banda, chanjo, madawa, vifaa n.k...
 
Kuku wa kienyeji ni rahisi zaidi kuwafuga hasa kama huna nafasi ya kusinda nyumbani asbh-jioni.

Kwani ukiamua kuwafuga kisasa (na inawezekana kabisa), unaweza kuanza na majike yanayokaribia kutaga, au vifaranga. Majike najua yanapatikana tabata chang'ombe ambayo ni kuku mfalme na Red Rhodes Island (sijui kama nimepatia order ya maneno lkn sijakosea herufi) na vifaranga vipo sehemu mbali mbali, kuna hapo Tabata Chang'ombe, Ruvu JKT (mchanganyiko), Kuna mama mmoja anaitwa Mama Mayunga ana kuku weusi kutoka mbeya, kuna Kilacha, na wenigne wengi. pia unaweza kununua kwa wafugaji wa mitaani, hasa nje ya mji kama Mkuranga, chanika nk.

Ufuagaji mzuri lkn ni gharama ni ufugaji wa ndani,

Faida:
  1. Sio rahisi magonjwa ya mlipuko kuingia hasa kutoka kwa kuku wa nje.
  2. Ni rahisi kujua tabia mbaya za kuku, mfano ulaji wa mayai,
  3. Ni rahisi kujua kuku waataga kwa muda gani yaani idadi ya mayai.
Hasara:
  1. Ni gharama, maana kuku hawajitafutii chakula inabidi ununue,
  2. ikitokea ugonjwa ukaingia bandani basi wote wako hatarini kuumwa.
mkakati:
  1. Dawa za magonjwa mbalimbali, vitamin na chanjo ni vitu ambavyo unatakiwa kuwa navyo karibu.
  2. Tenga kuku kutokana na umri ambao ni vifaranga sk 1-sk42, sk 42-sk180, na sk 180->, kwani kwa makundi hayo kuku hula vyakula tofauti.
  3. Muone afisa mifugo mara kwa mara hasa kuhusu chanjo na madawa, kama uko Dar ni vizuri ukaenda Farmers center, au Farmbase i maeneo ya ilala.
  4. Wanapokaribia kutaga andaa mipango ya utotoaji mfano unataka walalie au ukatotoleshe kwenye incubators ambazo zinapatiaka sehemu mbalimbali hapa Dar mfano Magomeni mt wa Idrisa.
  5. mara nyingi mayai ya kwanza huwa hayatotoleshwi kwa sababu inawezekana kuku hakupandwa na ni madogo sana kwa hiyo uza upate hela kulisha kuku au kula uongeze afya.
Kwaushauri wangu totolesha kwenye incubators kwani unapata vifaranga vingi kwa wakati mmoja gharama za ulishaji zanapungua pia kuku akinyang'anywa mayai hutaga haraka sana ndani ya wk mbili hivi tofauti na anayelalia maana akimaliza kutaga atalia siku 21 atalea siku 42, hlf atataga baada sk 14. Wakati ukimnyang'anya ataga tena baada ya wk mbili.
Usisahau kuwapa vitamini.

Au tafuta usaidizi wa kuchagua kuku walaliaji na waleaji ili kuku wengine waendelee kutaga kama kawaida.

Ni hayo tu kwa sasa.

Asante mkuu kwa shule. Hata hivyo nahisi umekuwa general sana na unaweza kumpoteza mtu

1. Kuku wa kienyeji sio rahisi kufuga zaidi ya wa kisasa, kama wote wanafungiwa ndani...

2. Kufuga kuku wa kienyeji kwa kuwafungia ni hasara tupu kifedha kwani wakati kwa mfano kuku wa kisasa wa nyama anakuwa tayari kuliwa (kilo 1.5), baada ya wiki 6-7, kuku wa kienyeji anafikisha uzito huo wiki 16-24 kulingana na malezi, japo anakula chakula sawa. Yaani kuku wa kisasa anakula chakula cha sh 1500 - 2000 kufikisha kilo 1.5, wakati kuku wa kienyeji anakula cha sh 6000 - 8000 kufikisha uzito huo.

3. So kweli kuwa kuku wa kienyeji hashambuliwi kirahisi na magonjwa, badala yake kuku wa kienyeji wanaugua mara nyingi zaidi kwa kuwa wanaanguliwa katika mazingira (na mama au na incubator), ambayo magonjwa hayajathibitiwa, hivyo ni rahisi ama kutoka kwa mama au wakati wa kuanguliwa kifaranga akaambukizwa magonjwa kama collibasilosis, leukemia, marek nk ikilinganishwa na wa kisasa ambapo hatcheries nyingi ziko controlled na vyombo vya seriakali.

4. Kumtunza kuku wa kienyeji kwa nyama ni risk zaidi kwani katika hali ya kawaida kwa kila kuku 100 (wa kisasa na wa kienyeji), hufa kuku 5 kwa mwezi. Kwa maana hiyo kwa kuku wa kisasa 100 kwa wiki 6-7 wanakufa kuku hadi 7, wakati kwa wa kienyeji, kwa miezi 4-5 wanakufa hadi 25 ( 5 kwa mwezi) kwa kila kuku 100.

5. Kufuga kuku wa kienyeji kwa mayai ni hasara kifadha kwa sababu anataga hadi mayai 90 kwa mwaka (kama hutamruhusu kuatamia), wakati wa kisasa hutaga hadi mayai 280 kwa mwaka...
 
Sawa mkuu lakini umesahau kutuwekea na gharama za kuwalea hao kuku kwa wiki 20 kabla hawajataga. Kwa maana hiyo kuku 2000 wanakula wastani wa gm 80 kwa siku, watakula kilo 160 sawa na mifuko 4 ya 50kg kwa siku, so mifuko 4 x Tsh33,000 x siku 150 = 19,800,000. Pia usisahau uliwanunua kwa Tsh 2200 kila mmoja, yaani 2000 x 2200 = 4,400,000, so kabla hujaanza kufuga kuku 2000 uwe na milioni 25 kibindoni, hapo hujapigia garama za banda, chanjo, madawa, vifaa n.k...
Mkuu, kuhusu chakula hesabu zako si sahihi sana, kifaranga hakili msosi sawa na kuku mkubwa, hebu cheki mchanganuo huu,

Hebu tuone hesabu hii:
Kuwanunua 2000 @2400 = 4,800,000/=

Chakula:

Mwezi wa kwanza (Wiki 0- 4) average kilo 75 kwa siku ( Mfuko mmoja na nusu hii ni Stater) @ 34,000 = 51,000 X 30 days =1,530,000/=
Mwezi wa pili ( Wiki ya 5 - 8) average kilo 100 kwa siku ( Mifuko miwili finisher) @ 34,000 = 2,040,000/=
Glower (wiki ya 9 - 11) siku 14, kila siku mifuko 3 @28,000 = 1,176,000/=
Glower (wiki ya 12 - 18) siku 42, kila siku mifuko 5 @28,000 = 5,880,000/=
Layers (wiki ya 19 -23) siku 28, kila siku mifuko 5 @32,000 = 4,480,000/=

------------------------
15,070,000
add Manunuzi 4,800,000

------------------------

19,870,000

-------------------------

Wiki ya 19 wataanza kutaga kidogo kidogo mpaka wiki ya 24 utaanza sales ya 50% ikiongezeka kadri siku zinavyosonga. Kwa hiyo mtu anayetaka kuanza ufugaji kwa kuku 2000 anahitaji mil 20,000,000/=. Ukiweka na gharama za banda na uendeshaji hadi waanze kutaga ni lazima uwe na 27m- 30million.

shughuli pevu hii, nashauri anayeanza, ni vyema basi aanze na kuku 500 then aongeze taratibu taratibu huku akijifunza challenges.
 
TUKO na FUSO mahesabu yenu yanakaribiana!! it is true. you need a capital ukitaka kuanza ufugaji wa layers!!
 
Nimeambiwa huko Mkuranga unaweza nunua shamba ukafuga kuku unaweza pata maneja akakuangalizia shamba lako na kukupa business plan ya kujenga mabanda hadi kufuga na kulima pia.

Je, kuna mtu anafanya hivi huko?

Na ukiwa sio mtu wakusimamia mradi huu wakati wote itawezekana? najua ni kupata mtu unayemuamini ila sijui maana inavutia.

Naombeni ushauri nina hamu ya kufuga kuku jamani.

Na kama ndiYo kujenga mabanda wapi nitapata plans na etc kuweza jenga.

shukurani
 
Nimeambiwa huko Mkuranga unaweza nunua shamba ukafuga kuku unaweza pata maneja akakuangalizia shamba lako na kukupa business plan ya kujenga mabanda hadi kufuga na kulima pia.

Je, kuna mtu anafanya hivi huko?

Na ukiwa sio mtu wakusimamia mradi huu wakati wote itawezekana? najua ni kupata mtu unayemuamini ila sijui maana inavutia.

Naombeni ushauri nina hamu ya kufuga kuku jamani

Na kama ndio kujenga mabanda wapi nitapata plans na etc kuweza jenga

Shukurani

Mzuriweye kama kweli unataka kufanya ufugaji siriaz wa kuku, jipange sawasawa, ili ikiingia uingie kweli. Kwa mfano, kwa hali ya afya ya kuku Tz, simshauri mtu afuge kuku wa mayai kwenye banda ambalo sio la battery cage.

Kuhusu kumpata meneja, ambaye atakupa na bz plan, inaweza kuwa ngumu. Nakushauri utafute plan kwa wataalamu au wazoefu wa planning, then utafute meneja, umkabidhi pjan, umwambie aibadilishe kuwa vitendo.
 
Nimeambiwa huko Mkuranga unaweza nunua shamba ukafuga kuku unaweza pata maneja akakuangalizia shamba lako na kukupa business plan ya kujenga mabanda hadi kufuga na kulima pia.

je kuna mtu anafanya hivi huko?

na ukiwa sio mtu wakusimamia mradi huu wakati wote itawezekana? najua ni kupata mtu unayemuamini ila sijui maana inavutia.

naombeni ushauri nina hamu ya kufuga kuku jamani

na kama ndio kujenga mabanda wapi nitapata plans na etc kuweza jenga

shukurani
ufugaji wa kuku wa kisasa una risk kubwa, lazima uwe front mwenyewe vinginevyo unaweza kupata presha ukafa siku si zako.
 
Fuga nguruwe wewee au fungua maduka manzese na Ubungo external kama upo ndarisalama.

kuku kichefuchefu!! wakipata ugonjwa usiku, mpaka ukiamka huna hata wa ushahidi.
Kwani brig nguruwe hawafi au hawapati magonjwa mimi nafikiri kila kitu kina risk yake na tusiogope risk bila hivyo hutafanya kitu
 
Kwa watalaamu na wafugaji wazoefu.

Nini kuku wale weusi ( black Australorp) wako wiki ya 5, nilianza nao 130 na sasa wamebaki 90 maana wanakufa karibu kila siku lazima afe mmoja au wawili. wanaanza kuvimba macho na hatimaye kufa,. Daktari alisema ni ukosefu wa vitamini. nimewapa vitamin aina ya Introvit A pamoja na dawa ya typhoid lakini wapi. wanaendelea kufa tu!!

Hebu nipeni maoni, huo unaweza kuwa ugonjwa gani maana naona sijapata dawa muafaka. naambatanisha picha!!

Photo0006.jpg
 
Kwa watalaamu na wafugaji wazoefu.

Nini kuku wale weusi ( black Australorp) . wako wiki ya 5, nilianza nao 130 na sasa wamebaki 90 maana wanakufa karibu kila siku lazima afe mmoja au wawili. wanaanza kuvimba macho na hatimaye kufa,. Daktari alisema ni ukosefu wa vitamini. nimewapa vitamin aina ya Introvit A pamoja na dawa ya typhoid lakini wapi. wanaendelea kufa tu!!

Hebu nipeni maoni, huo unaweza kuwa ugonjwa gani maana naona sijapata dawa muafaka. naambatanisha picha!!

Hayo nadhani ni mafua makali aina ya Coryza, ndio hufanya macho hasa jicho moja kuwa hivyo. Hayana tiba isipokuwa unaweza kuwasaidia kupunguza kasi ya kufa kwa kuwapatia lishe nzuri na dawa za mafua makali kwa muda. Yaani dose ikiisha unawapumzisha kidogo unaanza tena. Pia waliozidiwa huwa inatakiwa kuwasafisha macho yao kutoa hayo matongotongo kama maziwa mgando kwa maji ya uvuguvugu yenye chumvi kidogo, kama utaweza. Coryza.... note that. Huwa inanisumbua mimi kwenye kuku pamoja na kwamba wanako nje na wana eneo kubwa sana la kuvunjari wanakula mchwa, panzi, vimajani na kila kitu. Sidhani sana kama ni ukosefu wa vitamin....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom