Kwa wadau wote wa soccer

Mvina

JF-Expert Member
Aug 2, 2009
998
34
Nina wazo kwa wanaJF hasa wadau wa soccer ambao wangependa kwenda South Africa kushuhudia hata game moja kwenye michuano ya kombe la duania.Wazo langu kama kuna watu watakubaliana na nami na wapo interested kwenda tupeane mawili matatu ya msingi ya kufanya kabla ya kwenda na kama ikipendeza zaidi tukaenda kama JF members pamoja. Let me know if you are interested am planning for that..
 
Inacost kiasi gani return ticket Dar to Jberg? Ninahamu kweli ya kwenda japo kushuhudia game za kuanzia robo fainali...Ebu mvina kwa kuanzia tupeane Logistics kwanza then mambo ya cheap accomodation etc...
 
bora hiyo hela ya kwenda huko SA uitoe ichangie jf na uangalie tu katika luninga!
 
bora hiyo hela ya kwenda huko SA uitoe ichangie jf na uangalie tu katika luninga!
Ni mtazamo tu ndugu yangu wengine watasema heri hiyo hela tungepela kwa wahanga wa mafuriko kule Kilosa kwa ufupi mambo muhimu ya kufanya hayaishi.Kama nimefanya saving kwa miaka kadhaa kwa ajili ya hilo sioni sababu ya kutoenda.
 
Inacost kiasi gani return ticket Dar to Jberg? Ninahamu kweli ya kwenda japo kushuhudia game za kuanzia robo fainali...Ebu mvina kwa kuanzia tupeane Logistics kwanza then mambo ya cheap accomodation etc...
Tembelea kwenye website ya FIFA utaona ticket zina cost kiasi gani.Ukiangalia ni baro kununua 8 maana bei ni sawa na ya moja kama sijakosea.Mengine tutaendelea kupeana updates hapa hapa.
 
Miye nilitaka sana kwenda huko lakini crime rate ikanitisha sana, penye majaliwa naizengea 2012 Summer Olympic pale London.
 
Miye nilitaka sana kwenda huko lakini crime rate ikanitisha sana, penye majaliwa naizengea 2012 Summer Olympic pale London.
Suala la usalama nalo neno ila nadhani usalama utakuwa mkubwa sana kulingana na uzito wa suala lenyewe.
 
kila sehemu dunia hakuna usalama 100%ndio mana hakuna nchi isiyo na gereza,usalama umeimarishwa na hiyo soweto uliyokuwa unaisikia kitambo ambayo bongo na kwingineko duniani inatambulika kama uswahilini na matukio ya uhalifu,sasa imewekwa ulinzi wa kutosha na imeboreshwa ina watu wa matabaka ya juu zaidi,kati na maskini, na fainali soccer city uwanja mkubwa kuliko yote afrika sasa 94200 inabeba watu upo huko soweto fainali inapigwa hapo. na kingine na hata wewe mwenyewe lazima ujilinde mwenyewe,ni mfano hata bongo huwezi kujitembelea tandika kiholelaholela,eti kisa umeambiwa bongo nchi ya amani,hata huko uswisi yenyewe ukiingia mitaa ya watu wanakutamani inakuwa kama mwanaume kakosea choo kaingia choo cha kike nauli ni return maximum itakuwa usd 1500 na matumaini haitazidi hapo na ukiwahi mapema itakuwa nafuu.
 
Back
Top Bottom