kwa wadada wenye wachumba tu

Smile

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
15,347
11,610

UNAPOKUWA NI MCHUMBA WA MTU, HASWAKWA YULE AMBAYE UNAFIKIRI AU UNATEGEMEA ATAKUWA MUMEO,, NI VIZURI KUZINGATIABAADHI YA VIPENGELE HUSIKA VYA KULETEA HESHIMA YAKO KWENYE KIPINDI CHA MAHUSIANO

1 Usivaenguo za kuacha maungo yako wazi, usipende kutoka bila kumjulisha, unapotoka kwaruhusa yake au kwa kumpatia taarifa, hakikisha unaporudi unampa taarifa,usipende kufanya simu yako private sana, unapoongea na simu hakikisha baadhi yamaongezi yako ambayo sio delicate anayasikia, usipende kuwa mficha simu na kuwana vitu vya siri siri mpaka akakushtukia

2 Anapokutambulisha kwa marafiki zake, usionekane kuwafurahia sana walemarafiki zake , na wala usihitaji simu zao, akitaka kukupatia simu, mwambienitachukua kwa my (mchumba wako) Usipende kuwa na marafiki wa kike ambao niwale walioshindikana, au viruka njia, au wasiofaa hata kutambulisha.. Muonyesheunajali wazazi wako tangu mwanzo kabisa, kila kitu ukiongea usiache kuzungumziamzazi wako kwa njia moja au nyinginge

3 Unywaji wa pombe si jambo bora kwa msichana ambaye anategemea kuwa mamaBora, unashauriwa usipende sana kukaa bar au kunywa pombe , ni vizuri ukitolewaout na mpenzi wako akupeleke maeneo ambayo yana hadhi yako, na si mahali ambaokuna wingi watu, au mahali ambapo kila mwanamke anaingia,, ziko sehemu nzuriambazo zina ustarabu na si ghali sana, usipende mabaaa ya uchochoroni, hukondiko mnaopoibiwa waume zenu, kwani wanawake machangu wamejaa tele nahuwakodolea mimacho

4 Unapokuwa na mpenzio mahali popote, usipende kumsifia mwanaume mwingineyeyote kuwa ana gari zuri, kazi nzuri, au anavaa vizuri, hata kunukia vizuri,hii inamfanya mpenzio ajishushe hadhi, wakati wowote uwe tayari kumsifia yeyekama yeye, hii inamsaidia kumtia moyo na kuongeza juhudi kwenye kilaanachokifanya, Ni vizuri kumuonyesha kuwa kila kitu chake unakipenda, na kilaanachofanya amejitahidi, kama kuna kumkosoa au kumrekebisha basi kuna mahaliambapo au siku ambayo ni rasimi kumwambia kila unachofikiri kitamsaidia

5 Usiwe mstari wa mbele kumsapoti pale anapokuambia kuhusu udhaifu wa nduguzake, wazazi wako au boss wake, Tumia akili ya ziada kutoa mchango wako kwenyekila kitu atakachokushirikisha, ,, kumbuka yeye ni mume tu na kwenye mapenziyake yamejigawanya kwenye maeneo mengi, .. kazi, wazazi, ngudu, marafiki nk..hivyo usifikiri wewe peke yako ndiye unayehitaji upenzi wake..

6 husninyo swiitlady,afrodenzi lizzy ,firslady ,kongosho endeleeni

 
huo ndo mwanzo wa mapenzi ya kuigiza.

Be who you are, show who you are... kama wako wako tu hata ukafanya hayo yote hapo juu kama ndio tabia zako ulizozaliwa nazo au ulikokuzwa nazo.
kwa iyo unataka kusema huwezi kujifunza kitu kizuri ? kwamba kama umezoea mabaya uendelee nayo vile wewe ni wa mabaya tu? mabadiliko ni muhimu kila mahali
 
huo ndo mwanzo wa mapenzi ya kuigiza.

Be who you are, show who you are... kama wako wako tu hata ukafanya hayo yote hapo juu kama ndio tabia zako ulizozaliwa nazo au ulikokuzwa nazo.
..This is it. Na ndio moja ya sababu ndoa nyingi kuvunjika now days. Mwanamke anaigiza mkiwa wachumba, mkiingia katika ndoa ndio anakuwa yeye halisi, unakunjua makucha. Just Be Who U're.
 
Kwa nini watu wanachukulia mabadiliko kama kujifanyisha? Kwani mtu huwezi kufanya mabadiliko ya dhati?
 
Hii ni kuvaa ngozi ya kondoo wakati ndani ni mbwa mwitu
Be your self na haya mambo ya kupretend kuwa uko hivi kumbe uko vile hayana nafasi kabisa
Naamini katika msimamo au katika hali halisi ya kuwa mimi ni mimi na kile ninachofanya kwa wakati huo niko right na sifanyi kumfurahisha mtu na hilo ndio la maana
 
Kwa nini watu wanachukulia mabadiliko kama kujifanyisha? Kwani mtu huwezi kufanya mabadiliko ya dhati?



MAbadiliko yapo mkuu na sio kufanya jambo ili umfurahishe fulani
Kama kuna simu zako za siri ambazo huwezi kuongelea mwanamke wako akiwepo unaweza kufukia mashimo kwa muda ukiwa nae na bado tabia yako ukaendelea nayo ukiwa alone
Kama umeamua kubadilika kweli fanya kile ambacho moyo wako unafurahia kufanya na sio kujificha kwa mwavuli wa kusema nisionekane mbaya
 
Kwa nini watu wanachukulia mabadiliko kama kujifanyisha? Kwani mtu huwezi kufanya mabadiliko ya dhati?
Mimi nimemaanishamabadiliko ya dhati mimi sijazungumzia kuigiza .sijui wadau wametoa wapihilo?hivi kuna mtu anaezaliwa na tabia flani? Zote ziwe nzuri au mbayatunajifunza hapa hapa dunian
 
Kama uko kwenye ndoa kuna ubaya gani kufanya mabadiliko ya dhati yatakayomfurahisha mwenza wako?

Inategemea na aina ya mabadiliko
Kuna mabadiliko positive yes yanakubalika kwa wakati wote
Ila kuna mabadiliko negative na ambayo mwenza wako anaweza kuyakubali
Ila isipretend kwa mwenzako wala usitake kuvaa ngozi ya kondoo wakati wewe ni mbwa mwitu
Nakubali kuna mambo ambayo kweli ukishakuwa kwenye mahusiano inabidi uyaache na kuyazika na kubadili hata style ya maisha yako
Ila muhimu isiyafanye shingo upande kuona kwamba umelazimishwa na mahusiano hayo ndo maana umeamua kubadilika
badilika kwa kuwa umeamua na sio kwamba kuna forces behind inayokufanya ubadilike
 
Back
Top Bottom