Kwa wabantu mabadiliko yatachukua muda sana

Nakei

Member
Nov 10, 2010
44
11
Hapa tunajenga hoja, kama mtu ametofautiana na wewe usimtukane.
Tusijipe moyo kwamba nasisi tutafanya kama Misri, hawa jamaa wenye asili ya Kushitic wanamisimamo sio kama wabantu, ukimkosea atafanya juu chini hadi alipize na anaweza kukwambia amekusamehe lakini moyoni kwake bado analo. Mbantu ukimtishia kidogo anaogopa, pia tuna roho za kwanini, miaka mitatu iliyopita kulitokea machafuko South Africa watu weusi wanawaua weusi wenzao eti wanawachukulia ajira wakati ajira nyingi zimekamatwa na wazungu na wahindi, hawa wahamiaji weusi kazi wanazofanya ni hizi ndogo ndogo kama kazi za nyumbani na ukuli. Nahitimisha kwa kusema wengi wetu hapa jamiiforums ni wapiganaji kwenye ma computer lakini maandamano yakitokea tunajifungia maofisini au majumbani mwetu. Kwa wamisri wakinamama na watoto wameshiriki kwenye maandamo.
 
You have spoken bro! Kuthibitisha uliyoyasema hapo juu angalia wabantu walivyo wepesi ku-divide and rule? Ukimwaga pesa kidogo tu au hata chumvi, mbantu kwisha. Angalia bungeni na tabia za wabunge walioko ccm na ccm B! The list is endless! Akizidiwa anajificha kwenye ukabila, au kujuana!
 
Kwa nini nikutukane wakati unaongelea ukweli. Tunawatukana wendawazimu tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom