Umeenda nje ya topic....nani amependekeza anamshitaki rais hapa?Impeachment is lawful procedure .Hujiulizi hata kwa nini wanahitaji idadi saini n.k kabla ya zoezi,,,,,,Mkuu MMM impeachment unayoirejea iko ibara ya 46A ile ya 46 inapiga marufuku kumshtaki Rais akiwa madarakani. Mkuu nadhani Wabunge kwa maana ya Zitto ameangalia vizuri vifungu hivyo na kugundua kwamba ni vigumu sana kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais. Ukirejea Ibara ya 46A (2) vifungu vidogo vya (a), (b) na (c) utagundua ilivyo ngumu kumshtaki Rais. Ila ukirejea ibara ya 53A na Ibara ya 52 hasa ibara ndogo ya 1 basi utaona mambo yale yaliyoongelewa Bungeni jana yanamhusu PM moja kwa moja na kwa mujibu wa ibara hizo ni rahisi kupiga kura ya kutokuwa na imani naye kwa mujibu wa Katiba. Hii itaonyesha hasira za wabunge kwa serikali na Rais itabidi awe makini kuanzia hapo.
Sasa kama kweli tatizo ni CCM, wewe unadhani mwenyekiti wa CCM anaweza akaliondoa tatizo hili?Hivi kweli wapo wanaiamini kuwa ccm inaweza kutawala vizuri ukibadilisha watu wachache?
Hivi kweli wapo wanaiamini kuwa ccm inaweza kutawala vizuri ukibadilisha watu wachache?
Kuvunja bunge na kufanya uchaguzi mpya ni hatua kali na yakishupavu lakini haitasaidia kwa sasa kwasababu system iliyowaweka madarakani waliopo leo bado inanguvu ileile yakuwarudisha. Wengi tunaamini serikali iliyopo madarakani imeingia kwa mgongo wa vyombo vya usalama.
Tukiitisha uchaguzi mwingine kwakutumia utaratibu wa 2010 (katiba na vyombo vya usalama) tusitegemee matokeo tofauti sana. Wananch wameamka wanaona maovu lakin kwa namna moja au nyingine vyombo vya usalama vinanufaika na waliopo madarakani ndio maana ni rahisi kurubuniwa au kuamrishwa kusimamia matakwa ya wezi/mafisadi/manyang'au au wahujumu uchumi.
Kubadilisha baraza la mawaziri peke yake hakutaleta matokeo mazuri sana na kubadilisha maisha ya mtanzania. Baraza la mawaziri libadilike na hatua kali zichukuliwe.
Umeenda nje ya topic....nani amependekeza anamshitaki rais hapa?Impeachment is lawful procedure .Hujiulizi hata kwa nini wanahitaji idadi saini n.k kabla ya zoezi,,,,,,
Kwani impechment kwa rais iko nje ya katiba?
MKJJ unasahau haba na haba hujaza kibaba?
Gharama ya kuitisha uchaguzi sasa hivi ni ndogo sana kulinganisha na gharama ya wao kuendelea kutawala kwa miaka mitatu iliyobakia!
Mawazo ya watu kama hawa ndiyo yanawapa upenyo hawa wezi. Mtu anaona kuitisha uchaguzi ni gharama, lakini ndege mbovu inayokodishwa kwa dola milioni 200 haoni kama inamgharimu zaidi. VIP Lounge inayojengwa pale uwanja wa ndege kwa dola milioni 8 haoni kama ni tatizo. Na kibaya zaidi, haya ni awazo ya mtu anayejiita revolutionary na msomi.