maoniyangu
Member
- Jul 9, 2011
- 53
- 4
kuna tabia imezuka na inazidi kushika kasi siku hadi siku ya vijana kudharauliana kwa kutumia vyama. tabia hii imekuwa ikionyeshwa sana na vijana walio chadema, utasikia oh "kijana aliye ccm akapimwe akili" au "msomi alie ccm ana matatizo ya akili". kwa kweli mimi naona sio sahihi kwa sababu, kwanza kila mtu anao uhuru wa kushabikia au kuwa mwanachama wa chama anachokipenda. pili hakuna chama kilichosajiliwa kwa ajili ya vijana. hatuwezi wote kuwaza au kuwa na mtazamo sawa, hivyo tusilazimishane kuwa chama fulani.
hili taifa kwa sasa limeshakosa mwelekeo, cc vijana ndio tunaoweza kulikomboa, kunahitajika mapinzuzi katika kila nyanja(elimu, siasa, maisha n.k) . sasa kama tutaendelea na hii hali ya kudharauliana kwa kweli hatutofika kokote. hawa wazee wanatutumia na tusipokuwa makini wataendelea kututumia. nashauri vijana ndani na nje ya vyama vyetu tuungane ili tuweze kulikomboa taifa letu. hawa wazee hawana uchungu na hii nchi, kwanza wameshaila vya kutosha, pili mda wao si mrefu. nchi hii ni yetu sisi vijana.