Kwa uongozi huu soka la bongo litapaa kweli?

Orkesumet

Member
Jan 11, 2008
76
3
Katika ulimwengu wa sasa soka limekuwa ni biashara nzuri na yenye kuvutia uwekezaji kwa kiasi kikubwa tu. Klabu nyingi duniani zinajizatiti katika kuweka mifumo mizuri tu ya pesa, uongozi bora, uwekezaji katika timu za vijana na uwekezaji katika seniors. Kwani wachezaji wamekuwa ni assets kubwa katika vitabu vya timu (hope they qualify to be termed as biological assets). Nani alitegemea kuwa ipo siku mchezaji atauzwa kwa US$ 90 million!
Kwa upande wa tanzania, soka imetawaliwa na majungu tu! Uongozi uliokosa mwelekeo na wenye mtazamo wa kunyonya wachezaji kuliko hata kupe. Wengi wa viongozi wanafanya klabu kama "cash cow" na kuendeleza libeneke la ufujaji wa fedha za klabu. Ninasikitishwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wa klabu ambao wamekuwa mstari wa mbele kuwaadhibu wachezaji kwa kuwafungia kwa muda usiojulikana. Hivi kwa utaratibu kama huu kweli tuna nia nzuri ya kuinua kiwango cha soka na ari ya wachezaji ikiwa hatima yao ya kila siku ipo mikononi mwa viongozi na wala sio kanuni za klabu? Nchi zilizoendelea mchezaji hukatwa mshahara pale inapobidi au kuomba radhi nk. Wadau, tuwasaidie wachezaji wetu katika kuwashauri na hasa kabla ya kusaini mikataba yao na vilabu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom