Kwa kuwa mimi si muumini wa chama cha siasa lakini naipenda siasa.Tabia ya mawaziri wa CCM kutunisha misuli ya kutotaka kujiuzuru hata kama wanaboronga na kuipeleka nchi yetu katika maisha duni kwa wizi(Ufisadi) au uzembe wao basi kuna kila sababu ya chama mbadala hasa CDM kuichukua hii nchi.Haiwezekani waziri anasimama mbele ya wanahabari na kusema hawezi kujiuzuru kwa vile haoni kosa lolote wakati kuna ubadhirifu kwenye wizara yake.Hii ni dharau kubwa sana tena sana.Hivi hiki kiburi wanatoa wapi?