Kwa taarifa: Babu hajaita mtu Loliondo bali wanaenda wenyewe!!

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
614
Kuna baadhi ya watu kila kukicha wamekuwa wakipinga shughuli anazoziendesha Mchungaji Mwasapile, sijui kwa nini watu wanapata shida na shughuli anazoendelea nazo mzee huyu, nilidhani watu wanaompinga mzee huyu wangeshangaa sababu zinazofanya maelfu ya watu waendelee kwenda Loliondo bila mashaka pamoja na ukweli kuwa kwa sasa kuna ugumu kufika eneo hilo kwa maana ya miundombinu.

Kinachoonekana pale Loliondo ni picha halisi ya jinsi watu wengi wanavyoteseka na kuhangaika na magonjwa magumu ya hatari, kama hujaugua au huna mgojwa anayesumbuliwa na magojwa hatari huwezi kujua ugumu na shida iliyopo kwa mgojwa na ndugu wanaomhudumia. kuna watu hivi tunavyoongea wameacha kazi, waume, wake hata imani zao ili kuwauguza ndugu zao. Hivi leo ukiambiwa kuna mtumishi wa Mungu anadawa inayoweza kumponyesha ndugu yako utapuuza? Ni mara ngapi watumishi mungu wametangaza kwenye vyombo vya habari kwa nguvu zote kuwa tupeleke wagonjwa, viwete, vipofu ili wapate uponyaji lakini mwisho wa siku tukarudi nao wakiwa na shida zao? watumishi hawa tuwaiteje? mungu si bado atabakia mungu tu?

Watuwengi kutokana na shida walizonazo/magojwa wamedhalilishwa na waganga wa kienyeji hata na baadhi ya watumishi ambao wanajifanya wananguvu za Mungu. Watu hawa ndiyo wale ambao hawajali shida na matatizo ya mtu wanachoangalia ni kuwahamasisha watoe hata kile kidogo walichonacho wakiambiwa kuwa ndiyo mungu atawaponya. Mzee Mwasapile hajaita mtu Loliondo na hana muda wa kuita mtu, Dawa anayotoa ndiyo itasema ukweli wa jambo hili. Mambo ya imani yanaenda kiimani hata hivyo kama moyoni mwako huna amani na "kikombe" anachotoa Mchungaji mwasapile hulazimishwi kwenda ila usijenge hoja ya kuwapinga wale wenye imani juu ya "uponyaji uliopo ndani ya kikombe hicho"
 
Wala hajaweka mabango kama akina Kakobe, Mwingira, Ndodi cjui upako Lwakatale !
Matokeo ya huduma yake yamemtoa !

Wanao piga kelele wengi ni wale wanao criticize kila kitu na wivu usio kuwa na maana!

Kama watu wanapona kelele za nini?
 
Sina ubaya na hii thread, ila naomba mods waziunganishe humu jamvini ili tuzichangie zote kwa pamoja, sasa zinakinaisha.
 
Yesu alipowalisha wale 5000 walianza kumfuata kila aendako makundi makubwa, akawastukia. Akawapasha kweli yao kuwa walimfuata si kwa sababu waliziona zile ishara alizofanya (miujiza) wakaamini, bali ni kwa sababu waligonga menyu wakashiba. Ndiyo hayo hayo ya kwa babu. Wee unafikiri mnamfuata kwa maelfu kwa sababu mmeona muujiza mkamwamini Yesu? Si ni kwa sababu mlikunywa kikombe mkadhani mmepona? Amin nawaambieni, kuna kikombe kinachofaa, kile kiletacho uzima wa milele.
 
Back
Top Bottom