Kwa staili hii ya Sabodo naweza kabisa nikaamini CCM na CHADEMA lao ni moja

UP TO DATE: KADA WA CCM AIFADHILI CHADEMA.

Plz! jibu hoja sio kumzungumzia mtu mwengine,hili ni lenu wana chadema na viongozi wenu. sijawahi kuona mwanachama na kada wa chama tawala akifadhili chama cha upinzani. karibu litafumuka hilo.

Ukweli unauma

Kuna mengi hujawahi kuona wala kusikia inategemea na mahali ulipo na umri wako na pia uelewa ila kila kitu kinawezekana na sasa umeona mwenyewe kwamba Sabodo anatopa pesa Chadema na si mara ya kwanza .
 
UP TO DATE: KADA WA CCM AIFADHILI CHADEMA.

Plz! jibu hoja sio kumzungumzia mtu mwengine,hili ni lenu wana chadema na viongozi wenu. sijawahi kuona mwanachama na kada wa chama tawala akifadhili chama cha upinzani. karibu litafumuka hilo.

Ukweli unauma

Usipomjua adui yako huwezi kumshinda, na usipojua unaumwa maradhi gani kamwe huwezi pata tiba. CUF adui yenu ni ubinafsi wa Maalim Seif na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho, sasa kuja kwenye jumuisho kuwa aliyekiua CUF kule Zanzibar ni Chadema ni ujuha usio kipimo, ndiyo kamwe CUF haita fufuka kwani muuaji mnamtukuza kama mungu wenu huku mkitafuta mchawi Chadema. Calipso utake usitake CUF imekwisha, bora mngejua tatizo mngepata jawabu lakini kwa akili za kushikiwa kama unavyolalama hapa CUF KWISHNEY.
 
kaka mtu akisha tumia masaburi kuwaza basi anakuwa kesha isha kama KAFU wewe pita tu .

Jibu hoja kwa nn mnakwenda kumpigia magoti kada wa ccm awafadhili ? huu hamuoni ni udhaifu kwenye uongozi na vichwa vyenu ? tafuteni mfadhili mwingine ila sio kada wa ccm
 
"Siwezi kuondoka CCM ambako nimekuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka 40, CCM bado Chama kizuri, kina uzoefu wa kuongoza, isipokuwa ndani yake kuna baadhi ya viongozi hawaitakii mema, ndiyo maana wakati mwingine nakemea kwa kuwa siko tayari kuona Chama changu kikiteketea," alisema Sabodo. Alisema haoni chama mbadala cha CCM ambacho kinaweza kushika dola na kuongeza kuwa, “Vyama vyote vya upinzani havina uzoefu wa kuongoza nchi.”-Sabodo

controversial...!!!


 
Pamoja na kuwa mimi ni mpinzani na tokea nimepata fahamu zangu nimekuwa upinzani na sikuwahi hata siku moja kukishabikia CCM ktk maisha yangu kwa mengi walotufanyia na nimekua ktk harakati za upinzani kuhakikisha tunaliondoa dudu CCM muda wangu wote,lkn kwa staili hii ya Sabodo kwa kweli inanipa wasi wasi sana, na nakumbuka na niliwahi kuleta thread hapa miaka ya nyuma kuwa CCM inaitumilia CHADEMA kuimaliza CUF na niliwahi kutoa baadhi ya ushahidi,na nilisema ipo siku kwa mfumo huu Chadema itachukua nafasi ya pili na kuipiku Cuf,na nilisema hilo ndio lengo la CCM ktk harakati zake za kuimaliza Cuf kabisa kisiasa


Na kwa kweli CCM kwa hili wamefanikiwa,wanachoshindwa CCM ni kuwa znz hawawezi kabisa kuimaliza CUF na ndio maana safari hii wakawa hawana njia ya kufanya ila kukubali matakwa ya wananchi ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa,na ikiwa na hatua kubwa kwa Cuf ya kuchukua kabisa madaraka ktk uchaguzi mkuu ujao. Nathubutu kusema CHADEMA kwa hili la Sabodo kuna walakini,lkn mumezowea kukipakaza chama cha Cuf kuwa ni CCM-B kwa ajenda yenu ya pamoja na CCM kuimaliza CUF, lkn hili lenu la Sabodo mnalifanya kama hamlioni.


Nakumbuka mlikipakazia uongo Cuf inafadhiliwa na Rostam ili kuwaaminisha wananchi kua Cuf si chama cha upinzani,na mlifanikiwa kwa hili na mengine,lkn hakuna ushahidi mlotoa mpaka leo kwa kua ni uongo mtupu na hakuna kitu kama hicho.


Je! ingekuwa Cuf ndio wanafadhiliwa na Sabodo kama mnavofadhiliwa Chadema ingekuwaje? Naamini mungesema sana sana,lkn kwa kua kafadhiliwa CHADEMA mnapindisha mambo na kuleta tafsiri nyengine ili muaminike. lkn kwa hili la Sabodo kwa kweli CHADEMA hawana pakukimbilia,hilo mnalolifanya CHADEMA NA CCM kupitia Sabodo ni dudu kubwa sana na ufasadi wa hali ya juu ktk kuiangamiza democracy nchini kwa lengo lenu maalum lkna ipo siku litafichuka tu hili.

Sijawahi kuona siasa ya namna hii ila CCM na CHADEMA wana lao. Ajabu kwa Sabodo mara wameenda viongozi wa Chadema mara viongozi wa CCM. labda niseme pale ni transit.

Yetu macho ipo siku ukweli utafichuka. Kuna mengi yanafichwa na viongozi wa chadema na ccm.
Tofauti kati ya chadema na ccm ni majina tu mkuu. hilo kama hulijui basi kuanzia leo ujue hivyo. wanafanana kwa matendo yao, period!
 
Jibu hoja kwa nn mnakwenda kumpigia magoti kada wa ccm awafadhili ? huu hamuoni ni udhaifu kwenye uongozi na vichwa vyenu ? tafuteni mfadhili mwingine ila sio kada wa ccm
Nina wasiwasi na uwezo wa akili yako, hakika IQ yako inazidiwa na ile ya mbuzi. Kwanini usiwashauri viongozi wako wa CCM wamzuie kada wao kukifadhili chama kingine?ninani kakwambia viongozi wa Chadema walimpigia magoti Sabodo? Kwanini unajiita jina ambalo hata hulingani nalo?wewe ni Retarded Brain kenge usie fadhila!
 
Tofauti kati ya chadema na ccm ni majina tu mkuu. hilo kama hulijui basi kuanzia leo ujue hivyo. wanafanana kwa matendo yao, period!
Upo sahihi kabisa mkuu, na ushahidi ni kwamba CCM na Chadema kwa hiali yao walikubaliana kuunda serikali ya mseto huko Zanzibar! na wakalazimisha kuunda kambi rasimi ya upinzani katika bunge la muungano au vipi?
 
"Siwezi kuondoka CCM ambako nimekuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka 40, CCM bado Chama kizuri, kina uzoefu wa kuongoza, isipokuwa ndani yake kuna baadhi ya viongozi hawaitakii mema, ndiyo maana wakati mwingine nakemea kwa kuwa siko tayari kuona Chama changu kikiteketea," alisema Sabodo. Alisema haoni chama mbadala cha CCM ambacho kinaweza kushika dola na kuongeza kuwa, "Vyama vyote vya upinzani havina uzoefu wa kuongoza nchi."-Sabodo

controversial...!!!


Mzee Sabodo bwana wakati mwingine anachekesha, lakini nadhani umri wake unamsumbua, Kwani wakati wa uhuru 1960 TANU ilipata wapi uzoefu wa uongozi? mbona TANU ilikuwa na misingi bora ya uongozi kuliko hii CCM ya mafisadi.
 
Mkuu, kwa watuw anaoitakia mema CCM ni alzima wafanye kama anavyofanya Sabodo. Huyu bwana ameudhika sana na madudu aynayofanywa na chama hiki kikongwe ambacho kilistahili kuwa mfano wa kuingwa, lakini kimejigeuza kuwa mfano wa kuogopwa. sabodo anaipenda sana CCM na amegundua kuwa juhudi za kuwaambia wajirekebishe moja kwa moja haziwezi kufanikiwa. Ameramua kuisaidia Chadwema ili kuiamsha CCM, sasa kama CCM haiwezi kutambua hilo na ikaamka, hilo litakuwa ni kosa lao

Mzee Sabodo ameamua kuisaidia chadema ili iendelee kuimarika. Kuimarika kwa chadema kutaongeza changamoto kwa ccm na hivyo ccm itawajibika kuwahudumia wananchi kwa hofu ya kung'olewa na chadema.

Nadhani ametumia busara ya kawaida tu,asingeweza kuisaidia CUF ambayo tayari ni chama tawala kupitia mlango wa uani.
 
Mzee Sabodo bwana wakati mwingine anachekesha, lakini nadhani umri wake unamsumbua, Kwani wakati wa uhuru 1960 TANU ilipata wapi uzoefu wa uongozi? mbona TANU ilikuwa na misingi bora ya uongozi kuliko hii CCM ya mafisadi.

Mkuu hapo mzee sabodo ameamua kutoa controversial statement ili kujiweka katikati. Ila ukimfuatilia kwa makini utaona kwamba amesema hivyo baada ya kuona baadhi ya makada wa ccm wanaanza kumchachamalia. Kusema kwamba chadema haijakomaa kuweza kuongoza nchi ni katika kutuliza jazba za wanaccm waliokuwa wamefura!
 
chadema watakuwa na definition tofauti wakipewa fedha..

Upinzani bado sana..na opportunitistic tu hamna kitu hapo
 
Mimi nadhani ungetuonyesha hapa jinsi Sabodo anavyofanana na Rostam kwa wizi wa rasilimali zetu na ufisadi labda ungeeleweka, lkn kitu unachojaribu kusema hapa hakieleweki, labda ujaribu kuja na hoja inayoeleweka.
Ukweli ni kuwa ccm ni mafisadi hakuna abishaye. Kama ndivyo, Mzee Sabodo ni mwana ccm halisi, kwa ujumla ni fisadi kwani hata bahati nasibu aliyoiasisi mwaka 2007 kupitia shirika la Posta mafanikio yake mpaka leo hayajulikani . wajumbe wake akina mzee garus Abeid na Joseph Butiku ni mafisadi tu wa ccm. CDM mnapokea fedha batili ambayo mzee sabodo aliwachangisha wa tz kupitia bahati nasibu ya MNF. iko siku nitawauliza tena. If A=B, B=C, THEN A=C. NAWASILISHA, TUCHANGISHANE SISI MASKIN KUKIINUA CHAMA. FEDHA ZAO ZINANUKA.
 
Kwa kuwa chadema inatumia fedha za mwana ccm sabodo kuijenga na kuendeleza sera za chadema ina maana kuwa Chadema ina faidika, hivyo CCM inatumiwa na CHADEMA kwa masalahi ya Chadema hivyo, kwa hiyo CCM ni CHADEMA B and not the vise versa. Ndo maana wanaCCM wanalalamika, sisi wanachadema tunawapongeza viongozi wetu. Get it right.
 
toa uthibitisho unaoonyesha ccm walienda kwa sabodo na kwa uwazi kama cdm na ni wapi ccm wamekuwa wawazi kwa watu wanaokisaidia chama.
 
Sijawahi kuona siasa ya namna hii ila CCM na CHADEMA wana lao. Ajabu kwa Sabodo mara wameenda viongozi wa Chadema mara viongozi wa CCM. labda niseme pale ni transit.

Yetu macho ipo siku ukweli utafichuka. Kuna mengi yanafichwa na viongozi wa chadema na ccm.

Mkuu, kwa bahati mbaya sana sijkupata kabisa. Weka mambo wazi, ulikuwa unataka kusema nini hasa?
 
CCM na CDM lao ni moja kwasababu mbili kuu, Kwanza vyote vi nyama vya siasa,
Pili, CCM na CDM vina malengo ya kushika dola. Unlike CUF wao wanasubiri kuolewa
chama kilicho shika dola.
 
"Siwezi kuondoka CCM ambako nimekuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka 40, CCM bado Chama kizuri, kina uzoefu wa kuongoza, isipokuwa ndani yake kuna baadhi ya viongozi hawaitakii mema, ndiyo maana wakati mwingine nakemea kwa kuwa siko tayari kuona Chama changu kikiteketea," alisema Sabodo. Alisema haoni chama mbadala cha CCM ambacho kinaweza kushika dola na kuongeza kuwa, "Vyama vyote vya upinzani havina uzoefu wa kuongoza nchi."-Sabodo

controversial...!!!



Tumekwisha sema wengine humu ndani kidole na jicho CDM,fadhila ya ufadhili huu utaleta utata uko mbele ya safari.MSIPENDE VITU VISIVYO NA UZALENDO.HAKIKA MKIJITO MKASIMAMA UPANDE WA UZALENDO AMUHITAJI FEDHA KUJENGA CHAMA MNAITAJI WATU WALIOJITOLEA KUJENGA CHAMA.Rais mstaafu wa CUBA Fider Castro wakati anafanya Mapinduzi ya CUBA alifanya akiwa na watu wa 57 anatamka kuwa kama ingekuwa ni nafasi ya kufanya mapinduzi mala ya pili angefanya na watu 16 tu.
 

Hiii thread tuliijadili siku za nyuma huko:

Mfanyabiashara maarufu wa nchini, Mustapha Sabodo, ameahidi kumuunga mkono mgombea urais atakayependekezwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu ujao.

Sabodo alitoa kauli hiyo jana nyumbani kwake Dar es Salaam, katika hafla ya kukabidhi msaada wa kujenga visima 200 vya maji katika maeneo yote nchini yanayowakilishwa na wabunge 48 wa Chadema.

Alisema anakusudia kukichangia chama hicho kiasi kikubwa cha pesa, kisichopungua milioni 500, kwa sababu anakunwa na siasa zinazofanywa na Chadema katika kutetea maslahi ya wananchi.

Mbali na msaada anaoutoa kwa chama hicho kikuu cha upinzani, alisema anakusudia kukienzi kwa kujenga shule ambayo ataiita Chadema ili iwe kumbukumbu yake ya kudumu.

Leo tuna hii thread:


THURSDAY, 20 OCTOBER 2011 19:27 NEWSROOM


* Awakana CHADEMA, awaonya Watanzania

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Jaffer Sabodo, amesema hajahama na wala hana mpango wa kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho amekuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka 40.

Sabodo alisema baadhi ya kauli kali ambazo amekuwa akizitoa dhidi ya CCM, hazina maana kuwa anaichukia, isipokuwa zinalenga kukikosoa Chama ili kiendelee kuwa imara katika kuwaongoza Watanzania na kuharakisha maendeleo yao. Hayo aliyasema jana alipozungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati nyumbani kwake, Upanga, Dar es Salaam na kuwataka wana CCM na wananchi kwa jumla wasimwelewe vibaya.

"Siwezi kuondoka CCM ambako nimekuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka 40, CCM bado Chama kizuri, kina uzoefu wa kuongoza, isipokuwa ndani yake kuna baadhi ya viongozi hawaitakii mema, ndiyo maana wakati mwingine nakemea kwa kuwa siko tayari kuona Chama changu kikiteketea," alisema Sabodo. Alisema haoni chama mbadala cha CCM ambacho kinaweza kushika dola na kuongeza kuwa, "Vyama vyote vya upinzani havina uzoefu wa kuongoza nchi."

Alitoa toa wito kwa wananchi kutofanya makosa ya kufanya majaribio ya kuwapa ridhaa wapinzani kuunda serikali. "Nawaomba Watanzania wenzangu, tusifanye majaribio ya kuwapa CHADEMA au chama kingine chochote zaidi ya CCM kuongoza serikali kwa kuwa havina uzoefu, hatuwezi kufanya majaribio ya kuliweka rehani Taifa," alisema mfanyabiashara huyo.

Kuhusu msaada wa sh. milioni 100 alizotoa hivi karibuni kwa CHADEMA za kuchimba visima vya maji, alisema ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kuwa visima vitakavyochimbwa vitasaidia wananchi wote bila kujali itikadi zao za siasa.

Alisema amepanga kuchimba visima 200 katika majimbo yote nchini, bila kujali wabunge wa majimbo hayo wanatoka vyama gani kwa kuwa lengo lake ni kuwasaidia Watanzania na kutekeleza kwa vitendo Ilani ya uchaguzi ya CCM.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Chiligati alimshukuru Sabodo kwa kutoa msimamo wake huo kwa kuwa unamaliza minong'ono ya baadhi ya wanachama wa CCM na wananchi kwa jumla juu ya msimamo wa mfanyabiashara huyo ndani ya Chama.

"Nitawajulisha wanachama wenzako wa CCM na wananchi kwa jumla, kwamba bado uko nao kwa hali na mali ndani ya Chama chetu kwa ajili ya ustawi wa taifa letu, kauli yako imemaliza minong'ono kwamba umehama au una mpango wa kuhama CCM," alisema.
.

Wengine tukasema Michezo hiyo ya Chadema kwa demokrasia ya kweli ni kidole na Jicho.
 
Upo sahihi kabisa mkuu, na ushahidi ni kwamba CCM na Chadema kwa hiali yao walikubaliana kuunda serikali ya mseto huko Zanzibar! na wakalazimisha kuunda kambi rasimi ya upinzani katika bunge la muungano au vipi?
Naona umechanganya mambo,
cuf na ccm ni tofauti ndo maana zikalazimika kuunda serikali ya mseto
lakini matendo ya chadema na ccm ni yaleyale tu. mkuu labda nikuambie hivi nivigumu sana kutofautisha mwanaccm na chadema. angalia hata vyombo vya habari vinavyowabeba wote, ulishawahi kuliona hili huko nyuma kwa TLP, NCCR na CUF? Cheki hata Sabodo anatoa hela lakini hakuna wa kumuuliza, kumbuka sumaye alishasema ukitaka mambo yako yakuendee vizuri we isapoti ccm na ikiwezekana weka bendera kabisa, huoni sabodo anasapoti ccm B? Wote ccm na chadema waliiba kura igunga, wote walifanya fujo kama kuchoma nyumba moto, kumwagia watu tindikali na hata kuua. wewe unataka ushahidi gani ili uelewe?
 
Back
Top Bottom