Ciril
JF-Expert Member
- Jan 10, 2011
- 8,558
- 7,156
Nimemsikiliza kwa makini sana waziri kivuli wa wizara ya katiba na sheria Mh. Tundu Lissu.
Nilisikitishwa sana na kauli ya Lissu kwamba Zanzibar iamue ni aina gani ya muungano wanataka endapo wataendelea kuwa kwenye muungano.
Hii ni kauli hatari kwa maslahi ya taifa letu. Mwalimu alishawahi kusema kwamba viongozi walifilisika hutafuta kujihalalisha kwa makundi.
CHADEMA inataka kujihalalisha kwa upuuzi wa utanganyika, tuwakatae hao jamani!
Hivi pana tatizo gani kuwauliza watu wanautaka muungano wa aina gani?Baa ambazo wamiliki wake ni kutoka bara huwa zinachomwa kila siku inaripotiwa katika vyombo vya habari.Tafsiri ya matukio Kama haya nnayafananisha na moto unaowaka ndani Ila kwa sasa tunauona moshi ukifoka.Majadiliano ni muhimu sioni ubaya hapo